Thanks for your inquiry, the thread you are after is currently being updated but it is also on hold pending verification. All your posts are in safe hands. It will be brought back once ready. Thank you and have a good day!Mwanakijj samahan..thread ya ufisadi ATCL siioni...nimepost kidogo link ikaunganishwa kwa admin..vipi tena kulikoni...
Naomba uwasiliane tena na sources zako. Balali hajaongea na haja"authorize" yeyote kuongea kwa niaba yake.
Mdogo wa Ballali ambaye anaishi naye Boston, Marekani ameliambia gazeti hili kuwa kaka yake ambaye sasa anaendelea vyema
Mkuu Jasusi,
Heshima mbele sina osurce zaidi ya hiyo hapo juu, una maana hawa magazeti wanadanganya kumbe?
Kuna ujumbe ulipelekwa jana kwa Balali.. subirini hii wiki inayokuja.. unapocheza chess hakikisha unamlinda King! CCM wamesahau hilo..
FMES,
Naomba uwasiliane tena na sources zako. Balali hajaongea na haja"authorize" yeyote kuongea kwa niaba yake. Wakati utafika, Balali ataongea. Believe me!
1. Hiyo chess yhao inatusaidia nini sisi wananchi wa kawaida?
2. Yeye kama anawajua waliomlazimisha kuchota pesa zetu basi awataje, haya mambo ya chess ni ujinga mtupu.
3. Kama mtu ni clean na huna cha kuficha kwanini ujifiche?
4. Ballali huyo huyo aliyeenda bungeni akadanganya, kwenye vyombo vya habari akadanganya, mnampa benefit of doubt kwa misingi ipi?
5. Hawa viongozi wetu wanatuchezea kweli kweli. Kama kilichotokea kwenye mashamba yake si dalili tosha kwamba muda wa ubabaishaji unafika mwishoni. Asipoangalia wananchi watafanya mabaya hata zaida ya hayo.
6. Wenzake wamesema yeye ndiye kachota, anasubiri nini kuweka ukweli wake wazi?
Mkuu Jasusi,
Ni kweli tunajua Ballali hajasema lakini pia tunajua kuna cordinated efforts toka upande wake ku SPIN habari kwa faida zake.
Naomba uwasiliane tena na sources zako. Balali hajaongea na haja"authorize" yeyote kuongea kwa niaba yake. Wakati utafika, Balali ataongea. Believe me!
Mwanakijiji,
Hiyo chess yhao inatusaidia nini sisi wananchi wa kawaida? Yeye kama anawajua waliomlazimisha kuchota pesa zetu basi awataje, haya mambo ya chess ni ujinga mtupu.
Kama mtu ni clean na huna cha kuficha kwanini ujifiche? Yeye aitangazie dunia kwamba ana rudi na hana cha kuogopa na kuomba ulinzi ili asidhuriwe.
Kinachofanyika sasa ni mafisadi kuchezeana chess bila heshima yoyote kwa wananchi ambao ndio waliwakabidhi hivyo vyeo na ndio wameumia kwa ujinga wao huo.
Ballali huyo huyo aliyeenda bungeni akadanganya, kwenye vyombo vya habari akadanganya, mnampa benefit of doubt kwa misingi ipi?
Hawa viongozi wetu wanatuchezea kweli kweli. Kama kilichotokea kwenye mashamba yake si dalili tosha kwamba muda wa ubabaishaji unafika mwishoni. Asipoangalia wananchi watafanya mabaya hata zaida ya hayo.
Wenzake wamesema yeye ndiye kachota, anasubiri nini kuweka ukweli wake wazi?
Hapo yuko tayari kumlinda Mkapa kwa nguvu zote.
But also we are reading that, Gavana ni mtumwaji tu na wanaSiasa kutekeleza mambo;
.......................the mode of operation of the BOT is not well known to many especially in this forum. Kama kweli JK aliestablish kuwa Balali alibenefit kutokana na kuhalalisha hizo pesa basi balali is corrupt. ..................!
Maneno mazito sana hayo ndg IO
1. Operation ya BoT
2. Who is corrupt within BoT?.................... (at this instance Balali ni culprit) why kwa sababu yeye ndio Accounting Officer wa BoT
Tujue ya kwamba Acoounting Officer wa BoT (Balali) hufanya kazi yake kwa ushauri/mapendekezo toka kwa wasaidizi (kuanzia senior officers yaani Directors mpaka manaibu wake) + Bodi ya BoT, na wakati mwingine yeye mwenyewe hutoa directives....
sasa tatizo limetokea ni kutokana na
1. directives zake yeye kama Gavana au
2. kutokana na mapendekezo ya Officers below him (this includes him) au
3. Bodi ya BoT
kwa hiyo utaona kila sehemu Balali yupo kwa ni rahisi kum-pinpoint yeye kutokana na maelezo hapo juu
Huko nyuma niliwahi kuuliza Gavana anaripoti kwa nani? Rais?, Waziri? au PS? Bodi? na je Gavana kama anapewa directives je hizo directives hutoka kwa nani kati ya watu hao hapo?
Tukisha-establish hiyo chain then tutajua nani alifanya nini kwa madhumuni gani. Mpaka sasa hivi watu ambao uteuzi wao ilibidi UTENGULIWE (maana isiwe balali peke yake) nafikiri ni
Gavana....huyu tayari
Wakurugenzi wake wahusika
Naibu/Manaibu Gavana
Bodi ivunjwe na itakayoteuliwa iwe na wajumbe wapya.....thus inabidi akina PS nao uteuzi wao utenguliwe.......ofcourse bila kumuacha Waziri Mramba