Ballali aibuka na kujibu

Status
Not open for further replies.

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
614
KUNA habari kwamba aliyekua Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Daudi Ballali, ameibuka na kujibu mapigo akidai kwamba yote yanayotokea ni kujaribu kumtoa KAFARA na kwamba HAJAWAHI KUHUSIKA NA UFISADI WOWOTE. Anasema ana ushahidi mkubwa wa watu ambao walimtumia na wanajijua.

Nafuatilia:
Taarifa zaidi KESHOOOOO!!!!!!
 
watu walidhani tunawatania.. chess.. juu ya chess.. watu waende kusoma raiamwema.co.tz pale juu kuna kaujumbe...
 
Lete habari.
Asibakishe kitu chochote, ataje kila mhusika, na kama kuna ushahidi wa makaratasi nao autoe. Hii itasaidia kulisafisha taifa letu toka kwa hawa wahujumu.
 
Serikali ya JK itapona kweli? Maana naona ni mwendo wa makombora kwa makombora. Hapa kesi yake inabidi iende kwenye mahakama za kimataifa ambako hakitafichwa kitu, hata JK anaweza kuitwa vile vile!
 
KUNA habari kwamba aliyekua Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Daudi Ballali, ameibuka na kujibu mapigo akidai kwamba yote yanayotokea ni kujaribu kumtoa KAFARA na kwamba HAJAWAHI KUHUSIKA NA UFISADI WOWOTE. Anasema ana ushahidi mkubwa wa watu ambao walimtumia na wanajijua.

Nafuatilia:
Taarifa zaidi KESHOOOOO!!!!!!


Hivi huyu jambazi balali anataka tuamini kwamba yeye ni msafi kiasi kwamba yeye ni "KAFARA na kwamba HAJAWAHI KUHUSIKA NA UFISADI WOWOTE." Hivi ni vichekesho kubwa zima, well educated and experienced economist likawa linatumwatumwa ovyo tu linakubali. Halafu eti yeye ni kafara!!!!!!!!!!!!!!!!??????
 
KUNA habari kwamba aliyekua Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Daudi Ballali, ameibuka na kujibu mapigo akidai kwamba yote yanayotokea ni kujaribu kumtoa KAFARA na kwamba HAJAWAHI KUHUSIKA NA UFISADI WOWOTE. Anasema ana ushahidi mkubwa wa watu ambao walimtumia na wanajijua.

Ninaweza kukubali kwamba jamaa alitumiwa na alitegemea serikali ingemlinda ili yasimpate makuu, lakini sasa naona ngoma imekuwa nzito, baada ya kutumiwa na umuhimu wake kuisha, jamaa hao hao wakaamua kumtosa na kumbebesha mzigo wote. Sasa picha ndo inaanza na ninahisi itakuwa tamu sana!
 
Nyie watu wa ajabu sana. Yaani mnashabikia kitu kilicho obvious, kwamba Balali hakuwa peke yake.Kuna yale makampuni 22 na kuna wengine sisi hatujatajwa. What is news there? Hata hivyo, sijapata kuona mwizi anayesema yeye kweli ni mwizi na sijapata kuona mwizi kwenye mpango wa wezi wenzake akawa tayari kufa peke yake bila kutaja wenzake. Mbona mnajionyesha vilaza kwa kushabika jambo ambalo ni la kawaida na ambalo hata mtoto wa miaka minne angelitegemea.
 
Hivi huyu jambazi balali anataka tuamini kwamba yeye ni msafi kiasi kwamba yeye ni "KAFARA na kwamba HAJAWAHI KUHUSIKA NA UFISADI WOWOTE." Hivi ni vichekesho kubwa zima, well educated and experienced economist likawa linatumwatumwa ovyo tu linakubali. Halafu eti yeye ni kafara!!!!!!!!!!!!!!!!??????

Nyambala:
Taratibu ndugu. Hapa JF hakuna anayejua uhalifu wa huyo Balali au wa hao mafisadi hadi sasa, wote ni watu wa kushukiwa tu. Kwa hiyo tuvute subira; pengine mambo yatanyooka vizuri sasa tujue mbaya wetu ni nani hasa.
 
Nyie watu wa ajabu sana. Yaani mnashabikia kitu kilicho obvious, kwamba Balali hakuwa peke yake.Kuna yale makampuni 22 na kuna wengine sisi hatujatajwa. What is news there? Hata hivyo, sijapata kuona mwizi anayesema yeye kweli ni mwizi na sijapata kuona mwizi kwenye mpango wa wezi wenzake akawa tayari kufa peke yake bila kutaja wenzake. Mbona mnajionyesha vilaza kwa kushabika jambo ambalo ni la kawaida na ambalo hata mtoto wa miaka minne angelitegemea.

I smell KADA MPINZANI in making. Yule aliyekuwa katika kundi la watu wa ajabu. Endelea FISADIST- I mean FISI DUST

Asha
 
Ushirika wa wachawi huwa haudumu....na sasa wataanza kutajana mmoja baada ya mwingine.Nasubiri reaction ya DOUBLE FISADI (WA NGONO NA FEDHA) LIYUMBA(note the RED COLOUR).Kwa kupigwa chini u-DAP wa BoT ni sawa kabisa na kuziba mirija yake ya fedha alizokuwa anatumia kuulia dada zetu wenye tamaa ya fedha.Pengine hasira za demotion hiyo zinaweza kupelekea naye akaamua kuropoka...just thinking aloud.
 
eti nilikuwa natumiwa? mpuuzi sana huyu na bora aje aseme ukweli tujue who/where is the money? akiwa mkweli wananchi tunaweza kumpa immunity maana atakuwa ametusaidia kuondoa mafisadi wengi sana
 
hapo ndipo utakapokuwa mwanzo wa kunguka kwa dola ya wanamtandao.kuna siri kubwa katika Ripoti ya CAG.Mie nilipatwa kusimuloiwa tu jinsi ilivyoandikwa.Ila kwanini CAG asijiuzuru.?kwa kumdanganya Rais??kwanini aliwatetea baadhi ya watu.naamini blaali ataweka mambo wazi na CAG ataibika.

Halisi,So we should wait for Special Edition Magazine Kesho??au
 
"Viazi tulichimba wote, mwenzangu kanisemea kwa baba na baba kanidunda dunda na kunitilia ndani ya kichaka". Haya ndivyo yalivyo wanabodi, Balali na wengine wote waliohusika ni wezi kwani kwa pamoja walijua kabisa wanafanya kitu kibaya na hakuna aliyethubutu kumwaga siri. Balali alisaini na kupitisha malipo hayo badala ya kupelekewa makaratasi hayo mezani kwake, wote ni wezi hakuna mwenye nafuu. Hapa mpaka kieleweke hawa jamaa watatajana ile na kurukana ile mbaya. Bila shaka ndiyo mwanzo mkubwa wa kusambaratika kwa CCM. Wapinzani kwa ujumla kwanini kusifanyike kwa maandamano nchi nzima ya kumuunga mkono aliyefichua bomu hili na kulaani vikali wizi na uzembe wa CCM?. Kwanini Spika, wajumbe wa kamati ya fedha na baadhi ya wabunge wa CCM wasijiuzulu tokana na kwamba wao walikuwa watetezi wakubwa wa wizi huu pale bungeni?. Hivi ni kweli Jakaya haoni umuhimu wa kuwafukuza kazi meghji na mramba pamoja na mkaguzi mkuu wa serikali?.Hivi kweli Jakaya kwanini asitoe amri tu ya kukamatwa kwa wahusika wote na kuwekwa ndani tokana na ukweli kwamba ushaidi tayari ameshapewa na kampuni iliyofanya ukaguzi huo, imerahisisha kazi kwa kumtajia ni makampuni yapi yamehusika na yamelipwa kiasi gani, na ni nani anayemiliki kampuni hizo. Kuna haja tena ya kuwagiza watu kufanya uchunguzi juu ya uchunguzi?.
 
Nyambala:
Taratibu ndugu. Hapa JF hakuna anayejua uhalifu wa huyo Balali au wa hao mafisadi hadi sasa, wote ni watu wa kushukiwa tu. Kwa hiyo tuvute subira; pengine mambo yatanyooka vizuri sasa tujue mbaya wetu ni nani hasa.

Ndio mkuu kalamu, mimi namuhukumu huyu jamaa in the court of public opinion na sidhani kwamba in any how atakuwa ni innocent! the guy is proffesional na hivyo basi hata kama alitumwa ethically angeweza kuestablish namna na kuamua in favor of his proffesionalism. Kwa mzazingira ya kibongo ni ngumu, lakini unapokuwa kwenye ofisi nyeti kama ile lazima ujue unafanya nini!!!!!!!
 
tulikuwa tunamtegea aanzwe kuimba mapema sana huyo balali, hivi kachelewa mbona!
 
Daudi Ballali, ameibuka na kujibu mapigo akidai kwamba yote yanayotokea ni kujaribu kumtoa KAFARA na kwamba HAJAWAHI KUHUSIKA NA UFISADI WOWOTE. Anasema ana ushahidi mkubwa wa watu ambao walimtumia na wanajijua.

kwa hiyo kwa kusema hivi anamaanisha nini? Ana maana anakubali yeye ni kilaza na kazi ilimshinda siku nyingi au anataka kutuonyesha kuwa hana hatia na si fisadi ila ameonewa tu na angependa aendelee kuwa Gavana ili aendeleze kazi yake ya ukuwadi - wamtumie!
 
Mawaziri wahojiwa

Mwandishi Wetu Januari, 16, 2008



HALI si shwari ndani na nje ya Serikali kuhusiana na matukio ya Benku Kuu (BoT) na sasa imebainika kwamba baadhi ya wanasiasa, wakiwamo mawaziri, wa sasa na wa zamani, wanatuhumiwa kuhusika na ufisadi ndani ya benki hiyo.

Habari za ndani ya Serikali zinaeleza kwamba tuhuma hizo zimetokana na ukweli kwamba baadhi ya wanasiasa na watendaji waliojificha nyuma ya wafanyabiashara, wamenufaika na fedha zilizopotea ndani ya BoT.

Habari zinasema kati ya watuhumiwa hao, ni mawaziri wawili, ambao wamewahi kuwa karibu na aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk Daudi Ballali, ambaye wiki iliyopita alitangazwa kufukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete.

Mawaziri hao waliopata kufanya kazi na Dk. Ballali, taarifa zinasema, kwa muda sasa, wamekua wakichunguzwa na vyombo vya dola na siku za karibuni walihojiwa kwa mara kadhaa na vyombo hivyo.

Raia Mwema imetajiwa majina ya mawaziri hao lakini kwa kuwa haikufanikiwa kuwapata waeleze undani wa tuhuma hizo, haitawataja.

Lakini vyanzo kadhaa vya habari vinasema wenyewe walishitushwa sana na hatua hiyo ya kuhojiwa hasa ikizingatiwa kwamba mmoja wao ana nguvu kubwa ndani na nje ya Serikali na ilibidi ahakikishiwe kwamba uchunguzi huwa unafanywa kujiridhisha, hata kama mtuhumiwa anajiamini kuwa si mhalifu.

“Ni kweli wazee hao wamekuwa wakichunguzwa kwa muda mrefu hasa baada ya nyaraka nyingi kuwagusa moja kwa moja. Baada uchunguzi kufikia hatua muhimu ndipo walipoitwa kuandika maelezo yao, jambo ambalo wahusika wanasema halijawapendeza kabisa,” anasema kiongozi mmoja serikalini.

Pamoja na wanasiasa hao, vyombo vya dola vimekuwa vikiimulika Wizara ya Fedha na Waziri wa Wizara hiyo, Zakia Meghji, ameelezwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye amepania kusafisha maeneo nyeti ya uchumi.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kwamba kabla hata ya kutolewa kwa ripoti ya wakaguzi wa nje wa kampuni ya Ernst and Young, Rais Kikwete, alikwisha kujulishwa kuhusiana na hali ilivyo ndani ya taasisi za fedha na idara za Serikali zinazohusika na uchumi wa Taifa.

“Rais aliamua tu kuanzia na BoT ambayo ndio mhimili mkuu wa uchumi wa Taifa, lakini anafahamu kwa undani kila eneo la kiuchumi na anafahamu kwa kila kitu kuhusu watendaji wanaohusika katika kuhujumu uchumi wa Taifa,” anaeleza mtoa habari wetu ndani ya Serikali.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, muda si mrefu Rais Kikwete atafanya mabadiliko mengine ndani ya taasisi kadhaa zinazohusiana na uchumi, kazi ambayo anaifanyia utafiti wa kina kabla ya kufanya maamuzi ili kuepuka kinachoelezwa kuwa ni “kutopenda kufanya makosa ama kumuonea mtu”.

Pamoja na kuwa ni hivi karibuni tu Rais Kikwete aliagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuongoza timu ya wataalamu akisaidiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, kulikuwa na kazi iliyokwisha kuwa imeanza kufanywa na vyombo hivyo ndani ya BoT na maeneo mengine nyeti kiuchumi.

“Kabla hata ya Rais kutoa maagizo hayo, alikuwa anafahamu kwamba vyombo vyake vilikuwa vimekwisha kuanza kazi ya kuchunguza kwa makini maeneo yote yanayogusa uchumi na kinachosubiriwa sasa ni hatua dhidi ya wahusika na miezi sita aliyoitoa kwa wahusika kuchukuliwa hatua ni mingi mno kwani wako watakaofikishwa mahakamani hivi karibuni,” anasema ofisa huyo.

Wiki iliyopita maofisa wa idara mbalimbali za Serikali walikuwa makini zaidi katika kuchunguza viongozi na watendaji wa zamani na wa sasa katika Serikali na asasi zake ikiwamo BoT na baadhi wameonyesha mwanga mkubwa wa kupatikana ushahidi dhidi yao.

Mbali ya mawaziri hao, maofisa waandamizi wa asasi kadhaa za Serikali ikiwamo BoT, nao wamekwisha kufanyiwa mahojiano ya kina na vyombo hivyo vya Serikali ikiwa ni miezi kadhaa baada ya Gavana Ballali kuhojiwa kwa nyakati tofauti kabla ya kusafiri kwenda Marekani kwa matibabu na hatimaye kudaiwa kujiuzulu kabla ya Rais Kikwete kumuondoa madarakani.

Imeelezwa kwamba baadhi ya wanasiasa mwanzoni hawakufurahishwa na hatua hiyo ya Gavana Ballali kuhojiwa kiasi cha kutaka hatua hiyo isitishwe lakini mahojiano hayo yakaendelea baada ya kupata kibali kutoka kwa Rais Kikwete akiwataka watendaji ndani vyombo vya upelelezi kuendelea bila “kuogopa ama kumuonea yeyote.”

“Wanasiasa hao walihojiwa na kwa kweli wana taarifa muhimu sana zinazoweza kusaidia kutoa fundisho kwa wanasiasa kuacha kabisa kuchezea fedha za umma kwa kutumia vibaya madaraka wanayopewa na sheria ama kanuni,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Habari zaidi zinaeleza kwamba Mkurugenzi mmoja wa BoT, amekua akichunguzwa na kwa sasa amekwisha kufanyiwa mahojiano mara kadhaa na sasa huenda akachukuliwa hatua za kiutawala ama kufikishwa mahakamani na pengine vyote kwa pamoja.

Sakata la BoT lilianza kufukuta kwa muda mrefu kupitia vyombo vya habari vilivyokua vikihoji hasa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo na matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia mifuko na dhamana kwa wakopaji wakubwa ambao walianza kuonyesha dhahiri kuwa ukopaji wao ulikuwa wenye shaka kubwa.

Baada ya kujadiliwa kwa muda na vyombo vya habari, jina la BoT lilianza kuingia pole pole ndani ya vikao rasmi ikiwa ni pamoja na vikao vya Bunge ambako Mbunge wa Karatu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, aliongeza kasi ya waandishi wa habari kujua undani wa matumizi mabaya kupita kiasi ya fedha ndani ya Serikali kupitia Benki Kuu na Hazina.

Dk. Slaa alifikia hatua ya kutaka kuwasilisha hoja binafsi akitaka kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza matumizi mabaya ya kutisha ndani ya BoT, hoja ambayo iligonga mwamba hata kabla ya kuwasilishwa na badala yake kambi nzima ya Upinzani kuamua kuanza kutoa baadhi ya vipengele katika mikutano ya hadhara.

Hata hivyo, wakati Dk. Slaa akizungumzia BoT ndani ya Bunge, tayari Serikali kupitia Waziri wa Fedha, Zakia, ilikwisha kutangaza kufanya uchunguzi wa kuhusu matumizi ya fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) lakini bila kufanya uchunguzi katika maeneo mengine pamoja na kuwa maeneo hayo yamekuwa yakichunguzwa na vyombo vya dola.

Baada ya kauli ya Meghji, Serikali kupitia ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali Ludovic Uttouh (CAG) iliajiri mkaguzi wa nje, kampuni ya Ernst and Young, ambayo ilianza kazi Septemba, 2007 na kukamilisha Desemba, 2007. CAG aliikabidhi ripoti ya wakaguzi hao kwa Rais Kikwete Januari 7, 2008.

Anaeleza Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo kuhusu maoni ya Rais Kikwete juu ya ripoti hiyo: “ Amesikitishwa na kukasirishwa na taarifa ya kuwapo vitendo vya ukiukwaji wa makusudi wa sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni ya nje vilivyofanywa katika taasisi muhimu na nyeti kama vile BoT.”

Rais Kikwete alimuondoa madarakani Dk. Ballali na kuagiza kwamba hatua za kisheria na kiutawala zichukuliwe dhidi ya makampuni na watu waliohusika na upotevu huo.

Rais Kikwete alimteua Profesa Benno Ndulu, ambaye Raia Mwema lilimtaja mara kadhaa kuwa mmoja wa waliokuwa wakitajwa akiwatangulia wengine, kuchukua nafasi ya Dk. Ballali.

Rais Kikwete aliagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ikutane mara moja kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya maofisa wote wa benki, walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara kwa taifa.

Mbali ya kusitisha shughuli za EPA na kuagiza vyombo vya dola kuwashughulikia wahusika, Rais Kikwete alimuagiza Mwanasheria Mkuu kuhakikisha kwamba fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa na Luhanjo alisema kwa wale ambao wamezibadilisha fedha hizo katika rasilimali, serikali itachukua rasilimali hizo kufidia fedha.

Makampuni 22 yametajwa kuhusika na upotevu wa zaidi ya Sh. bilioni 133, kutokana na ama kutokuwapo kumbukumbu za kuonyesha makampuni hayo ama kuwapo kwa nyaraka za kughushi na mengine kukosa uhalali wa kulipwa fedha hizo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ukaguzi katika mwaka wa fedha wa 2005/2006 uliochunguzwa, katika mwaka 2005 yalifanywa malipo ya jumla ya Shilingi 133,015,186,220.74 kwa Makampuni 22 ya hapa nchini. Makampuni hayo ni: Bencon International Ltd., VB & Associates Company Ltd., Bina Resorts Ltd., Venus Hotel Ltd., Njake Hotel & Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd., Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd., Changanyikeni Residential Complex Ltd., Kagoda Agriculture Ltd., G&T International Ltd., Excellent Services Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd., Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas (T) Ltd., Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na KARNEL Ltd.

Taarifa ya Ikulu ilieleza kwamba ukaguzi umebaini kwamba kati ya fedha hizo, kiasi cha Shilingi 90,359,078,804.00 zililipwa kwa makampuni 13 ambayo yalitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizo batili na za kugushi na hivyo makampuni hayo hayakustahili kulipwa chochote.

Makampuni hayo yametajwa kuwa ni: Bencon International Ltd., VB & Associates Company Ltd., Bina Resorts Ltd. of Tanzania, Venus Hotel Ltd., Njake Hotel & Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd., Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd., Changanyikeni Residential Complex Ltd., Kagoda Agriculture Ltd.

Ukaguzi umeendelea kubaini kuwa makampuni tisa ambayo yalilipwa jumla ya Sh. 42,656,107,417.00 hayakuwa na nyaraka za kuonyesha stahili ya malipo na hivyo kuwafanya wakaguzi washindwe kuhakiki uhalali wa malipo hayo.

Makampuni hayo yalitajwa kuwa ni: G&T International Ltd., Excellent Services Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd., Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas (T) Ltd., Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na KERNEL Ltd.

Wakati huo huo Makampuni mawili, yaani, Rashtas (T) Ltd na G&T International Ltd., kumbukumbu zake za usajili katika daftari la Msajili wa Makampuni nchini hazikuweza kupatikana.


http://www.raiamwema.co.tz/08/01/16/1.php
 
Malala Hoi Mungu Si Wa Balali. Pdidy....wala Wa Mwanakijiji,,,
Niliomba Wapendwa Tujaribu Kufunga Siku Mungu Atajibu Mamombi Yetu Na Hivi Ndivyo Anavyoanza Na Amin Usiamin Uwe Msilamu Mkristo Mpagani Tuzidi Kusali Mambo Yanakuja Mengi Tu,,kuna Vigogo Wengine Watangaza Nao Walilazimishwa Kusign Kama Mama M.....na Wengineo Na Ndipo Watakapomtaja The Real One,,,
Ushindi Lazima
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom