Nyamtoroka, heshima mbele!!!!!!Ndugu zangu baada ya kusikia mama Meghji karudi kuwa mtunza hazina wa CCM kichwa changu kimepata simanzi na Taifa tulilonalo, kwa lugha nyingine watanzania muelewe kesi zote za EPA ni danganya toto kama CCM imerudi kumuamini huyu mama ambaye ndie alikuwa singnatory mkubwa wa fedha za EPA, naomba mwandishi yeyote wa habari akikutana naJK amuulize DR. Balali gavana wa zamani wa BOT yupo wapi? kweli watanzania mnashikwa masikio sasa.
Naomba kuuliza na kuweka historia vizuri. Sehemu kubwa ya wizi wa EPA ulifanyika mwaka 2005, na fedha hizi zinadaiwa kumweka madarakani rais J.K. Safu ya uongozi ya mwaka 2005 katika CCM, Mwenyekiti alikuwa Mkapa, Makamu bara Malecela, Zanzibar akiwa Karume. katibu wake alikuwa Mangula na idara ya fedha na uchumi ilikuwa chini ya Marehemu Salome Mbatia. Kipindi kile Zakia Megji hakuwa katika kamati kuu ya chama bali alikuwa waziri wa maliasili na utalii. Najua naye ni mchafu sana hali iliyopelekea kuondolewa uwaziri wa fedha. Ila mwaka 2005 nadhani hakuhusika, huo ni uelewa wangu, kama ni tofauti naomba ufafanuzi.
Masaiti.....