Mzimu wa Balali waibuka "twitter" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzimu wa Balali waibuka "twitter"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 24, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Katika hali ambayo inaonesha kuweza kuja kulitetemesha taifa kupita kiasi mtu anayejiita "Daudi Balali" ameanza kuzungumza kupitia mtandao wa Twitter akijaribu kuwaamsha Watanzania kuwa taarifa za kifo chake zilikuwa za uongo na kuwa huko aliko yu mzima salama salimini. Daudi Balali "huyo" alianza kuandika kwenye mtandao huo wa intaneti ambao umekuwa maarufu duniani kwa kuweza kutoa taarifa za watu mbali kwa haraka zaidi na kwa maneno machache zaidi.

  [​IMG]


  Balali alianza kuandika mwezi Disemba tarehe 6 mwaka jana kwa maneno machache tu akisema kuwa "Its time to go home" yaani "Wakati wa kwenda nyumbani umefika". Kwa maneno hayo machache mtu huyo ajiitaye Balali alianza pole pole

  kudokeza kuwa taarifa ambazo serikali ilizitoa kuwa "amefia" Marekani hazikuwa na ukweli wowote na kuwa ilikuwa ni sehemu ya njama za kimataifa za kumnyamazisha kufuatia kuibuliwa kwa wizi mkubwa katika Benki Kuu ya Tanzania wakati yeye alipokuwa Gavana wa Benki Kuu.


  Daudi Balali alikuwa ni Gavana wa Benki Kuu baada ya kuletwa nchini na aliyekuwa Rais wa Tanzania Bw. Benjamin Mkapa kuwa Mshauri wa Rais pale Ikulu. Baada ya muda mfupi Ikulu Balali alipewa nafasi ya kusimamia taasisi kubwa kabisa ya fedha nchini ambayo ina wajibu wa kusimamia uchumi wa Tanzania yaani Benki Kuu. Ilikuwa ni chini ya Gavana Balali wizi wa aina mbalimbali ukihusisha magenge ya kimataifa ya mitandao ya kihalifu ambayo yalikuwa yanafanya kazi nchini kwa kushirikiana na wanasiasa, wataalamu na wana usalama mbalimbali.

  Katika ya kashfa zote kubwa ambayo ilionekana kutishia usalama wa nchi na utawala ulio madarakani ni ile inayojulikana kama Kashfa ya EPA. Wakati wa Gavana Balali makampuni mbalimbali nchini yaliwasilisha Benki Kuu hati za kujitambulisha kuwa yamepewa haki ya kisheria ya kufuatilia madeni ya makampuni ya nje ambayo yalikuwa yanaidai Benki Kuu ya Tanzania kutokana na sababu mbalimbali za kiuchumi. Makampuni hayo ya Kitanzania yalipatiwa taarifa za ndani ya madeni hayo na watu kutoka ndani ya Benki na yakafanikiwa kukusanya baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara nchini ambao waliunda kwa haraka haraka makampuni feki ya kudai madeni hayo kwa "niaba" ya makampuni ya kigeni.

  Katika hali ambayo ilishtua Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Fedha ya Deloitte and Touche ambayo iligundua kutokupatana kwa taarifa mbalimbali za makampuni hayo. Kampuni hiyo iliandika taarifa yake kwa Gavana kuelezea kutokupatana huko na kushangazwa ni jinsi gani watu wa Benki kuu walishindwa kuona tofauti hizo. Hata hivyo katika hali ya kushangaza kampuni ya Deloitte and Touche iliondolewa kufanya kazi hiyo.

  Hata hivyo siri ilikuwa tayari wazi. Makampuni 22 yalijipeleka Benki Kuu na kuwasilisha vielelezo mbalimbali vya ulaghai na watu wa Benki Kuu wakiwa na akili timamu na wenye elimu ya juu kabisa wakawapatia kiasi cha dola milioni 133 kwa urahisi kabisa. Waliochukua fedha hizo wakazibadilisha huku wengine wakizihamisha nchini. Kampuni maarufu kati ya hizo 22 ni kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo peke yake ilichotewa zaidi ya dola milioni 40 kutoka Benki Kuu!

  Kuibuliwa kwa kashfa hiyo ambako kulipigiwa kelele vikali na viongozi wa upinzani Tanzania kulielekea kutishia watawala ambao walijitahidi kutafuta namba ya kukabiliana kwani ukweli ulikuwa ni mgumu kuukana. Kwamba, kuna fedha zilichotwa Benki Kuu hakukuwa na shaka; kwamba makampuni yaliyochotewa fedha hizo yalikuwa ni feki hakukuwa na shaka; kwamba

  kulikuwa na njama ya hali ya juu kufanikisha hilo bila kushukiwa na vyombo vya usalama nalo halikuwa na shaka. Serikali ikajikuta iko kwenye matatizo.


  Lakini kilichounganisha vitu vyote ilikuwa ni taarifa iliyotolewa na kundi lisilojulikana ambalo kwa mara ya kwanza liliwachorea Watanzania picha ya mtandao wa uhalifu wa kiuchumi (economic criminal ring) ambao unafanya kazi Tanzania. Taarifa hiyo ilionesha kuwa mtandao huo unahusisha wafanyabiashara kadhaa wa Kitanzania pamoja na watendaji wa ngazi za juu serikalini ambapo kinara alikuwa ni Gavana wa Benki Kuu Bw. Daud Balali. Taarifa hizo zilidakwa na wapinzani na Dr. Wilbrod Slaa wakati huo akiwa Mbunge wa Karatu alihoji juu ya taarifa hizo katika Bunge ambapo mwanzoni aliyekuwa Spika Bw. Samwel Sitta alijaribu kupuuzia kuwa ni taarifa za "mtandaoni".


  Hata hivyo, madhara yalikuwa yamekwisha fanyika. Pamoja na juhudi zote za serikali kujaribu kupuuzia na kuonesha kuwa siyo jambo kubwa ilikuwa vigumu kuwashawishi Watanzania kuwa madai ya wapinzani na Watanzania wengine yalikuwa ni ya "kisiasa" tu na ya "kutafuta umaarufu". Hatimaye, Gavana Balali aliitwa Dodoma ambako alikutana na viongozi mbalimbali. Hiyo ilikuwa ni baada ya kufanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alikanusha kabisa kuhusika na wizi huo na kudai kuwa kilichokuwa kinaelekezwa kwake ni njama za "wafanyabiashara" ambao hawakufurahia alivyokuwa anasimamia Benki Kuu.


  Alipotoka Dodoma kwa ndege ya Serikali Balali "alitoweka" nchini. Siku chache baadaye taarifa zikatangazwa kuwa amepelekwa Marekani kwa matibabu japo siku ya kuondoka na namna alivyoondoka hakuna ambaye alikuwa tayari. Na huo ndio ulikuwa mwisho wa Balali kuonekana Tanzania. Taarifa zikaanza kutokea kila baada ya siku chache juu ya maendeleo ya "hali" yake huku nchi ya Marekani ikitoa ofa kwa serikali ya Tanzania kuwa kama wanamtaka Balali ingeweza kumsaidia kumleta nchini. Serikali haikuwaomba Marekani kufanya hivyo.


  Kama wiki moja hivi kabla ya "kifo" chake taarifa za mpango wa geresha ya kifo zilivuja kutoka vyanzo vya ndani sana ambavyo vilidokeza kuwa Balali alikuwa atangazwe kuwa amekufa kwa "ule ugonjwa" na atazikwa huko huko "Marekani". Na kweli siku chache baadaye taarifa kuwa Balali amefariki dunia zilitangazwa na kama ilivyokua kwenye mambo mengine taarifa hizo hazikukubaliana. Serikali ya Tanzania ilitangaza kuwa Gav. Balali ambaye alikuwa analipiwa matibabu na serikali alikuwa amefia kwenye "hospitali moja huko Boston" japo taarifa zilizotolewa kwenye "msiba" huko Washington DC zilidai kuwa amefariki katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Georgetown ambako alisomea miaka kama arobaini iliyopita.


  Katika hali ambayo ilitarajiwa (na kinyume na desturi ya misiba mingi ya Watanzania) mwili wa Balali haukuoneshwa kuagwa na hakuna mtu yeyote wa nje (asiye mwana familia) ambaye amewahi kuonesha aidha Balali akiwa mgonjwa hospitali au mwili wake ukiwa unaagwa. Na kinyume na kawaida nyingi za Watanzania wanaofariki nje ya

  nchi mwili wa Balali haukurudishwa nchini kwa mazishi. Taarifa nyingine ambazo zimekuja miaka karibu miwili tangu taarifa za kifo cha Balali zitolewe zimedokeza kuwa Balali aliruhusiwa kutoka hospitalini na kwa miezi mitatu alikuwa akiugulia nyumbani. Hizo nazo zilikinzana na taarifa za serikali kuwa Balali alikuwa ameugulia hospitali hadi mauti yalipomkuta.


  Hivyo, kuibuka kwa "Balali" kunaelekea kuibua mjadala mwingine kabisa kama kweli alikufa kama ilivyotangazwa au alitoweshwa na kufichwa mahali akiahidi ukimya. Maandishi ya Balali wa mtandao wa "twitter" yanaonesha kuwa kama kweli ndiye Balali wa BoT basi huko aliko amechoshwa. Dalili ya hali ya kutokukubali (defiance)

  ya Balali wa twitter inatukumbusha jinsi alivyojitokeza hadharani kuzungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa juma la pili la mwezi Julai 2007 akikanusha vikali madai kuwa alihusika na wizi wa EPA.


  Baadhi ya watu wanaamini kuwa ilikuwa ni maneno yake yale ya hadharani ambayo yaliwashtua wahusika mbalimbali kuwa Balali hakuwa tayari kubebeshwa zigo la Kagoda na kama wangemuachilia kwa hakika angemwaga ugali, kumwaga mboga, kuvunja masufuria na kuchoma jiko!


  Maandishi ya Balali wa twitter yanaonesha kuwa ni mtu ambaye anaamini amedhulumiwa haki yake ya kusema ukweli na kuwa huko aliko anajuta kuondoka Tanzania katika mazingira ya alivyoondoka. Akiandika siku ile ya kwanza ya Disemba 6, 2011 Balali wa twitter anaandika "I didn't die, I'm not dead" kwamba "sikufa, niko hai". Baadaye aliandika "I miss home" na kuwa "the Big 6 and the Architect said I died" akimaanisha kwamba anatamani kurudi nyumbanio na kuwa Vigogo 6 pamoja na "Mtaalamu" ndio waliosema kuwa amekufa. Aliongeza pia kudai kuwa hakukuwa na jinsi yoyote ya yeye kwenda kinyume na weledi wa fani yake na kuisaliti nchi ambayo anaipenda kutoka moyoni.


  Hata hivyo akidokeza kwa mbali kile kinachowezekana kuwa ni sababu ya yeye kutokea hadharani sasa Balali wa twitter anasema "they ripped me off" akimaanisha kwamba hao watu waliomsababishia kukubali kuondoka nchini wamemuingiza mjini. Akiwaita watu hao "wao" anasema wanauwezo wa kuchagua rais, kutafuta fedha na kuzitumia na kutangaza watu kuwa wamekufa. Balali wa twitter amedai kuwa kama atakufa sasa kabla ya lengo lake kutimia bado siri aliyo nayo itawafikia wananchi. Inasadikiwa kuwa wapo watu wachache sana ambao Balali huyo amewafuata na kuwapa sehemu ya taarifa aliyonayo kwa masharti kuwa wakae nazo na wazitoe tu kama atashindwa kufika nyumbani katika muda aliouweka.


  Balali huyo amedai kuwa hao waliomsababishia atoweke nchini waliamini kuwa hana madhara yoyote kwao na kuwa wanajua kwamba yuko hai japo hawajui yuko mahali gani. Katika maandishi yake ametuhumu vyombo vya habari kuwa navyo vinatumika kiufisadi kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya juu kabisa.


  Balali huyo amedai kuwa ameandaa mpango wa kina ambao anaufuata wa kuweza kulipua mambo yote ambayo bado yamewakalia wananchi kama kivuli. Ameahidi kufunua gharama halisi ya Minara Miwili ya Benki Kuu, Jinsi Benki Kuu inavyofanya kazi, EPA, Magavana "halisi" wa Benki Kuu, Mkataba wa Rada na mambo mengine kem kem. "Nina mpango wangu kamili ambao ni lazima niufuate na hivyo sina haja ya kuharakishwa kufanya lolote; nitaamua mwenyewe nifanye nini na vipi" amedai Balali huyo wa twitter na hivyo kufanya wahusika mbalimbali kuanza kuwa na matumbo moto hasa kama itathibitka kuwa ni kweli anayezungumza ni Balali aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

  Akionekana kuwa anatekeleza mpango wake Balali huyo wa twitter alianza kuhesabu siku zilizobakia hadi mpango wake huo kutimizwa. Tarehe 9 Disemba (Siku ya Uhuru) alitangaza kuwa zimebakia siku 308 hadi tukio fulani ambalo amelidhamiria litatokea. Haijulikani kama ni siku ambayo yeye mwenyewe atajitokeza hadharani au siku ambayo nyaraka mbalimbali zinazohusiana nay eye zitawekwa hadharani. Siku 308 tangu Disemba 9, 2011 ni tarehe 12 Oktoba, 2012.

  Vyovyote vile ilivyo, wazo kwamba suala la Ballali halikufikia mwisho unaoeleweka linaacha uwezekano mkubwa wa watu wa aina mbalimbali kuweza kujitokeza na kufanya lolote wakijua tundu kubwa lililoachwa wazi na serikali baada ya kuonekana kushindwa kabisa kujua la kufanya juu ya Ballali. Lakini kinachotisha zaidi ni swali lisiloepukika "vipi kama ni kweli huyu ni Ballali"


  Chanzo: FikraPevu.com
   
 2. D

  DOMA JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Itafahamika tu mkuu
   
 3. ze encyclopedia

  ze encyclopedia JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 271
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  penye ukweli, uongo utajitenga. ole wao watumiao madaraka yao vibaya., mungu wa ibrahim atawaadabisha tu. na malipo ni hapa hapa
   
 4. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Lazima tukubali kifo cha Ballali hakiaminiki kutokea. Kibaya zaidi ilikuwa kuridhika kwa urahisi juu ya kifo chake kwa ndugu na hata mjane wake Anna Mganda, na baadaye Shemeji yake wa VoA Emmanuel Mganda kujibu kwa ukali kabisa alipotakiwa aeleze yaliyotokea huko aliko US ktk Tanzanet.

  Eti alizikwa US, eti hata nchi haikuwakilishwa, eti hata hatukuona picha za mazishi, eti hata mama yake hakupewa tiketi ya kuhudhulia mazishi! Tangulini mbongo awe cremated hata kama ni maskini kafiri?
  -------------------------------------------------------

  Ballali surfaces on `Twitter`

  Source: :: IPPMEDIA

  Nearly four years since it was controversially announced that he had died in the United States, the former Bank of Tanzania Governor, Daudi Ballali has a ‘ghost' emerging on twitter, strongly refuting the news that he is dead.

  [​IMG]
  Former Bank of Tanzania Governor, Daudi Ballali


  Taking advantage of the illness surrounding and finally the purported death of the former Governor, a man calling himself Daudi Ballali has been twittering for three months now, attracting about 236 tweets (postings), 808 following and 1,151 followers.

  He first emerged on twitter on December 6, 2011 with just a few words' "It's time to go home", before he wrote that the news about his death was a total lie aimed at silencing him on what he knew about various corruption scandals that rocked the Bank of
  Tanzania about six years ago.

  He termed the news about his death an international racket to silence him, indicating that if these claims are accurate then
  Dar es Salaam didn't act alone.

  He has promised to drop a bombshell that would shock the government in a few months, adding that it's time to tell the truth about what really is happening.

  The Twitter Balali comments indicate that he is a bitter man who has been denied the right to put the record straight by telling the truth, and wherever he is he regrets to have moved from
  Tanzania in the circumstances he did. Writing first on December 6, 2011, the Twitter Balali remarks, "I didn't die, I'm not dead."

  Later he wrote, "I miss home. The Big Six and the Architect said I died." He insisted that there was no way he could have gone against the norms of his profession and betrayed the country which he deeply loves.

  Commenting on what could possibly be the motive for his coming out from the cold now, the Twitter Balali says, "They ripped me off." Referring to the culprits as ‘they,' he says they have the wherewithal to make a president, to secure funds and to declare people as dead.

  The Twitter Balali claims that should he die now before fulfilling his objective, the secret he harbours will still be known to the people. It is believed that there are very few people whom Balali approached and gave part of the confidential report he has on condition that they should keep it and only divulge if he fails to get back home in the period he has set for himself.

  The Twitter Balali claims that those who engineered his disappearance from the country believed that he would be completely harmless to them, and that they know he is alive although they don't know precisely where he is. In his comments he accuses the media of complicity in embezzlement and thievery from the very bottom to the highest level.

  The Twitter Balali claims that he has got a grand plan in store to lay bare secrets which are yet to be known by the people. He has pledged to reveal the actual cost of the BoT Twin Towers, how the central bank operates, EPA, the actual central bank ‘governors,' the radar contract and a few other matters.

  "I have a grand plan laid out and which I must follow. I don't have to be rushed into doing anything; I'll decide myself when to do what and how," claims the Twitter Balali, thereby sending a number of the culprits into panic, especially if it should turn out that the writer is indeed the former BoT governor.

  In an apparent move to implement his grand plan, the Twitter Balali started a count-down of days to go before he embarks on its fulfillment. On December 9, 2011 (Independence Day) he said there were 308 days to go before a certain incident was to happen.

  It is not known for sure whether it is the day he would appear in public or the day sensitive documents in his possession would be laid bare. The 308 days from December 9, 2011 falls on October 12, 2012.

  However one looks at it, the idea that the Balali affair did not reach a well-defined target finality leaves plenty of room for people with various schemes and designs to emerge and put them in motion in cognizance of the vacuum created by the government after its being seen to have failed to know what to do with Ballali. But what is even more scaring is the inevitable question: "What if this man is truly Balali?"

  Last week he gave the wake up call to Tanzanians saying they should stand firm to stop the plunder of the country's natural resources, which was being done by international companies with assistance of some local officials.
  A preliminary survey conducted by the Guardian on Sunday has established that the man calling himself Daudi Ballali is indeed tweeting from United States because his IP address uses the America country code.

  However, many of his followers online are puzzled, believing that the former central bank governor didn't die as claimed by the government while a minority doesn't believe him at all until given tell-tale evidence.

  On 9th of December 2011, the day Tanzania marked its 50th year of independence, the ‘new' Ballali wrote on his tweeter page saying there were still 308 remaining days before something big happens in the country.

  In calculation it means October 12, 2012 will be the deadline or the date set for the so called ‘something big' that he promised will happen in Tanzania.

  So far no statement has been issued by the government to refute the claims made by the man calling himself the late Ballali.

  On June 7, 2009
  The Guardian on Sunday reported exclusively about a row which is simmering between Daudi Ballali's widow and the Bank of Tanzania (BoT), whom Mrs Ballali said should foot $37,000 (Sh49.9m) in unsettled bills for the late central bank governor's medical treatment.

  According to sources within Ballali's family, during his treatment in the United States between October 2007 and May 2008, Ballali's total medical bill totaled around $85,000.

  Although the main portion of the bill – which was predominantly incurred when Ballali was admitted to a Boston hospital for a haphazardly explained illness – had already been paid by the family's health insurance policy and the remaining $37,000 was outstanding bill.

  The $37,000 covered nursing services provided by the hospital after Ballali was discharged but was still kept under special care at his home.

  Ballali remained under home nursing care for about three months before passing away on May 16, 2008.
  Ballali's widow, Anna Mganda Ballali, sent the medical invoices to BoT management in March, 2009 year, but the bank has so far declined to pay the bills.

  Confusion reigned in the country when reports surfaced in May, 2008 that the former BoT boss had passed away in the US. Even close family members kept his death a secret before the government made an official announcement a week later.

  Ballali's remains were buried in Washington, D.C. on May 23, 2008 at a private funeral arrangement supervised by the De Vol Funeral Home after his body was cremated.

  Mourners from different parts of the world sent in condolence messages through a guestbook posted on the funeral home's website.

  However no Tanzanian diplomat attended the funeral let alone viewing the body, a move that cast doubt about the reports on Ballali's death. Some people questioned why the death of a high profile civil servant like Ballali was treated as a state secret, leaving the issue ensnared in controversy.

  According to government reports Ballali, who was fired as central bank governor in January 2008 amid a spate of revelations on how massive amounts of cash were paid out from the External Payments Arrears (EPA) account, died on May 16, in a Boston, Massachusetts hospital.

  The former BoT chief left the country late 2007 for medical treatment but neither official information on his ailment nor the hospital where he was being treated were released.

  His departure to the US coincided with the start of a special, government-ordered BoT audit that uncovered the EPA scandal and triggered a sequence of events that culminated in his sacking by President
  Jakaya Kikwete.  By ERICK KABENDERA, The Guardian
   
 5. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  nimeona tweets za huyo tweeter balali, na whichever way it goes (whether the actual balali is dead or alive), it is gonna create a hell of a 'tweet-quake' around
   
 6. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Only in Tanzania.
   
 7. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Lie!!!!!he passed away!!
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  nayeye kma yuko hai si ajitokeze aje kusema ukweli asife na dhambi.
   
 9. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,658
  Likes Received: 5,248
  Trophy Points: 280
  mbona hata walio sema ukweli dhambi.... bado zinatafuna mifupa yao.. B4 our resources turn into dust, then them first zey will turn to dust. Lord av mercy on us (poorer)
   
 10. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mtaruka na kukanyagana sanaana.......:lol::lol::lol::lol:!
   
 11. remon

  remon JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 295
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  km ni kweli huyo mtu anajiita balali , na akajitokeza na kutoa hiyo report basi kichwa cha kikwete na watu wake ni halali yetu...... f...k tz gorv
   
 12. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mh. anna Mganda, baba mwanaasha ,manumba wao wanasemaje? kuhusu hili ni kweli mshikaji yupo alive! hata hilo kombora analodai ataliangusha si litakanushwa tu then wabongo tutatulia! kama songea tumekaa kimya,Kama arusha tumekaa kimya mgomo wa madaktari nao tumeuchuna, posho za wabunge nazo tumeuchuna si na hilo tutauchuna tu. HIVI HAMJUI KUWA WATZ tusio viongozi ni Misukule
   
 13. a

  afwe JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  I am sure time will tell!
   
 14. ERASTO SYL

  ERASTO SYL Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Whether it is true or not.Mie nina swali: Kwa kuwa nchi ya wenzetu ina uwezo mkubwa wa kutunza taarifa za ki-uhamiaji na wageni wanaoingia na kuishi nchini mwake,Hivi kwanini Serikali ya USA isiombwe kutoa ushahidi wa tukio hili?Kwa nini nchi yetu isiombe investigation ya kujua kama yu hai au la? Tukumbuke huyu alikuwa ni HIGH RANKED GOVERNMENT OFFICIAL tuna haki za kupata taarifa CLEARLY AND CLEAN kuhusu kila kitu HATA KAMA MIAKA IMEPITA MINGI TAYARI.
  Naomba kuwasilisha!
   
 15. B

  Bandio Senior Member

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania nchi ya pekee.
   
 16. Hercule Poirot

  Hercule Poirot JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,195
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Hii imekaaje wadau............
   
 17. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tanzania nchi ya ajabu?
   
 18. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Haaaaa wapi balali ibuka tu mkubwa usiogopeeee!!!
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kashapewa fungu lake hawezi kujitokeza kamwe, si unajua serikali yetu kwenye maovu haikosi hela
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  ibuka tu balali labda mkuu ataachia madara kwa kashifa ya kifo chako
   
Loading...