BAKWATA na Mauaji Arusha

BAKWATA na Mauaji Arusha

Asante Kikwete kwa Huduma nzuri za afya kila sehemu ya nchi hii.

Bigirta kwanza tuambie hapa ni wapi? Tanzania kweli? Pili sikatai umaskini umezidi Tanzania lakini ndio maana kuna watu wanaitwa wanasiasa na sio viongozi wa kiroho. Wakitaka wavue majoho yao waingie ulingoni venginevyo sikubaliani nao.
 
Fundi mchundo

Kwakweli unayoyasema mengine yana ukweli kwamba lugha kali za kidini zinaweza kupelekea migogoro ndani ya nchi yetu. Ila the Padre Lwambano alivyoitoa hiyo kauli ilikuwa kama anatoa maagizo kwa serikali iwashughulikie waislamu. Na kumbuka Lwambano alitoa hilo tamko tarehe 8 February, 1998 , mapambano yakatokea few days later tarehe 13th February 1998. Rais awamu ile ambaye Mkapa bila kushauriwa vizuri akatoa amri ishughulikiwe hiyo hali. Haya sio maneno yangu ni huyu Aziz kama anavyosema hapa:-

Few people can doubt that Lwambano appears to have been encouraged by the public and official
endorsement the Catholic clergy had received with regard to their grievances against Muslim preaching.
That endorsement had come from a fellow Catholic in the person of the President of Tanzania. On 4
January 1998 at Tabora during celebrations of the Western Diocese of the Moravian Church, President
Mkapa declared war on “people who go about distributing cassettes, booklets and convening meetings
where they insulted and ridiculed other religions” (Daily News, 5 January 1998). It is relevant that Muslim
preachers are the only people using cassettes and booklets, in addition to public debates, in the propagation
of religion

Na maaskofu wameendelea na tabia yao hii ya kujiona wao ndio wasemaje wa wananchi na wako juu kuliko viongozi wengine wa kiroho. Na hili ndio linalowafanya wajisahau mpaka waingie sasa katika siasa jambo ambalo litawatokea puani. Na jamaa amelitahadharisha kama anavyosema tena hapa:-

It is my considered opinion that the response by the CCM government is religiously biased and prejudiced. Given the fact that the Catholic clergy had failed to prove their charges of blasphemy in a mediation meeting of Bishops and Sheikhs convened by former President Mwinyi in1993, President Mkapa’s move of unilaterally embarking on using state power to remedy a grievance of his Church leaders without giving Muslims the right of reply suggests nothing but religious bias. Catholics are after all expected to follow whatever the hierarchical church says!

Sasa Pengo should have apologies to muslim for the comments of his fellow member au kama hilo ameshindwa basi kwa kushindwa kukemea matumizi ya nguvu zisizo na msingi kwa raia waliokuwapo pale mwembechai ambao wengi wao hawakuwa katika sehemu ya ule uharamia wa kutaka kuchukua ule msikiti wa mwembechai. But kwakuwa serikali ilikusudia kutoa message kwa waislamu wakaamua kufanya wapendavyo ili kutoa message kwa waislamu wote kuwa hili jambo halikubaliki na maaskofu wakaa kimya kama vile hawaoni na hapa siko pamoja nao kwa hili.

Mkuu Mdondoaji. Padri Lwambano ametoa tamko tarehe 8 FEBRUARI 1998 ambalo Rais Mkapa aliitikia tarehe 4 JANUARI 1998! Hivi hii kweli inaingia kichwani? Huyu Aziz na Njozi ni wale wale wenye extremists ambao wanataka kulaumu kanisa kwa kila ovu linalousibu UMMA wa kiislamu. Hivi kweli unataka kuamini kweli Rais Mkapa alikuwa akipokea maagizo kutoka kwa padri wake wakati wa uongozi wake? Si utakuwa sawa na wale walioamini kuwa Mwinyi (na Kikwete) wanapata maagizo kutoka Iran na Saudia? Wote mtakuwa hamna maana.

Padri Lambano kama raia yeyote alitoa duku duku lake kuhusu hali ya kutisha iliyotanda Tanzania katika miaka ya mwisho ya 90. Tulikuwa hatujazoea maneno ya chuki kutamkwa wazi wazi baina ya jamii yeyote nchini mwetu ukiondoa kwa hao tunaowaita wahindi. Hivi leo ukilalamikia vibaka wanaotishia usalama katika nchi yetu na baadae polisi wakafanya operesheni na kuua baadhi yao utawakubalia kweli wale watakaodai kuwa uliwaamrisha hao polisi kuua na kudai lazima uwaombe msamaha?

Huku kuandama Kanisa kutokana na yale yaliyotokea Mwembechai ni uonevu na kukwepa responsibility. Mlitakiwa kuwakemea wale walioleta mihadhara ya chuki na ksababisha uhasama mkubwa katika misikiti yenu, Mwembechai ukiwa mmoja wao. Kama hamtaki kulaani mauaji yaliyotokea Arusha lakini msijitetee kwa kuyafananisha na yaliyotokea Mwembechai, Pemba na Unguja. Hivi leo utaweza kulaani mapdri na maaskofu kukemea uovu pale wanapouona kwa vile tu mnatofautiana dini? Mimi ningedhani ungewahimiza viongozi wako waungane nao badala ya kuzinduka pale tu mdini mwenzao anapodhulumiwa. Hii Tanzania ni yetu sote na kilio cha mmoja wetu lazima kiwe chetu sote.

Amandla.......
 
Bigirta kwanza tuambie hapa ni wapi? Tanzania kweli? Pili sikatai umaskini umezidi Tanzania lakini ndio maana kuna watu wanaitwa wanasiasa na sio viongozi wa kiroho. Wakitaka wavue majoho yao waingie ulingoni venginevyo sikubaliani nao.

Wanasiasa ni watumishi wetu na tuna kila haki ya kuwakosoa pale wanapokosea bila kujali kama tumevaa majoho, kanzu au la. Tutakapozuiwa kufanya hivyo ndiyo mwisho wa demokrasia katika nchi hii.

Amandla....
 
CCM wakibanwa kwa maovu yao wanakimbilia kwenye karata ya udini, na JK baba yao ndo kawafundisha huo mchezo sasa hawaoni hata haya, kwani ukiwa kiongozi wa dini na haki ya kutoa maoni na taarifa kwa jamii kuhusiana na uovu uliotendeka? naomba msaada wa kisheria jamani? freedom of speech and assembly inawabana viongozi wa dini kutokemea uovu?

CCM wanatakiwa wajirekebishe haraka sana hizi tricks za mgonjwa wetu wa taifa za name calling will cost ccm badly! JK na Makamba wataondoka na hakika mgombea wao in 2015 might be a christian, hawa ma sheikh wanaowatumia wataawapigia kura CUF as they alwys do,, and JK anavyo watukana viongozi wa dini za kikristo ni kuwapush away wakristo from ccm. their strategy is bad strategy it may work for now but it will cost ccm big time in the near future.
 
Jamani hii dini ina matatizo, hebu angalieni wakristu wanavyo fanyiwa Misri,Iran hata Nigeria siku ya kuamkia mwaka mpya hii hali haiwezi kuvilika lazima mabaliko yaletwe
 
1. Wakati Maaskofu wakidai hawamtambui meya, BAKWATA wanasema wao wanamtambua
na kama yupo ambaye haridhishwi na uchaguzi aende mahakamani na iwapo matokep
yatatenguliwa, BAKWATA wapo tayari kufanya kazi na yeyote atakaye chaguliwa.

2. Wote wamelaani matumizi ya nguvu kubwa yaliyofanywa na Polisi

3. Wakati BAKWATA wakisema mambo ya wanasiasa tuwaachie wanasiasa, maaskofu
wanafanya siasa za wazi kabisa na inaonesha wanahamu ya kuvua majoho yao na
wameacha kauli mbiu yao ya kila siku kuwa tusichanganye dini na siasa.

WANAJAMII KATI YA TAASISI HIZI MBILI, IPI INANUKIA JAPO KIDOOGO HARUFU YA UDINI?
 
Kwa wakristo kutomtka Kikwete, nadhani lina ukweli ndani yake. Tazama hata humu JF, ni wakristo wangapi wanomponda Kikwete ingawa ni wazi kabisa kuwa Kikiwete ni kiongozi mzuri, mchapa kazi na ameifikisha mbali Tanzania katika miaka hii mitano.

Hivi Zomba unamtindio wa ubongo nini? au unalipwa kiasi gani mpaka unakuwa kipofu kiasi hicho?
Ngungu yangu muogope mungu moto upo.
 
MASKOFU NA MASHEHE, KABLA YA WADHIFA WAO KWANZA NI WATANZANIA HIVYO KUKEMEA MAOVU HAKI YAO

Nashangaa sana harufu ya udini anayoweza mtu kulazimisha katika hoja ya MAASKOFU KULE MJINI ARUSHA ni upi huo hasa? Maana mpaka dakika hii MAASKOFU wametangaza wazi kwamba hawamtambui MEYA WA CCM JIJINI ARUSHA, ambaye naye ni MKRISTO SAWASAWA na hao Maaskofu, KWA KUZINGATIA JINSI ALIVYOINGIZWA OFISINI KIMABAVU.

Kimsingi MAASKOFU walisema wazi kwamba wanachokipinga kwa meya huyu wa CCM wala si maovu ya kuwa mwana-CCM, si maovu ya UKRISTO wake isipokua MAOVU WANAYOYAKEMEA ni sheria na taratibu za uchaguzi zilivyopindishwa kumuingiza madarakani kupitia mlango wa nyuma.

Sasa viongozi wetu wa kiroho wasipokemea maovu kama haya, ukimya wao juu ya jambo hatari kama hili tafsiri yake ni kwamba wameunga mkono huo uchafu na ubakaji wa DEMOKRASIA, ndivyo watu mnavyotaka????????????????

Kama shida ni kuhusu vifo vya raia wa Tanzania na hata yule wa nchi rafiki na jirani Kenya, nadhani mtu asijaribu kuziba wengine midomo. Mauaji ya pemba 2001 vingozi wa dini walipiga kelele sana na kuikemea serikali ya Mhe Mkapa wakisema nguvu nyingi kupita kiasi imetumika dhidi ya wananchi. Katika kundi hilo kulikwepo Mashehe, Maaskofu, Mapadri na Wachungaji kwa mchanganyiko wake.

Hivyo kutokana na ukweli huu ambao iko mikononi mwao waandishi wa habari mpaka leo hii, ni matumaini yangu kwamba hauna maana yoyote kutaka kutuambia ya kwamba kama kilio cha Watanzania hakikusikilizwa tulipoipigia kelele mauaji ya Pemba basi leo hii raia tunapouaua tusiseme kwa sababu kule hatukusilizwa vile vile.

Pia, sitaki niaminishwe ya kwamba mweka hoja hii anajaribu kutuambia kwamba MAUAJI YA KINYAMA ARUSHA kwa vyovyote vile yalitekelezwa na MTU AU WATU anaowajua yeye ILI KUSAIDIA KUMLIPIA KISASI CHA MAUAJI YA PEMBA leo hii hivyo anaona hadi sasa ngoma ni droo na wala kusilalamike mtu?

Mwisho, imekuaje mtoa mada umekwepa kujiuliza maswali yote ya msingi hapa; Je, MASHEHE NA MAIMAMU kukaa kimya bila kukemea mauaji ya kinyama Arusha hadi kujitokeza tu kutetea Mhe kwa sura nyingine ya ajabu ajabu tu inamaana wanayo agenda gani?????????
 
tatizo la hawa wenzentu ni hili ELIMU, ELIMU, even they don't know what they are talking, externally they pretend to know well
mentally they are poor, let me ask them, why they keep quite while Dowans inalipwa? na bei ya umeme imepanda, they are too
shallow to argue with them
 
Kuna kila dalili kwamba Chama cha mapinduzi CCM kimeamua kutumia BAKWATA mkoani Arusha kupingana na kauli ya maaskofu ya kutomtambua meya wa Arusha. Bakwata wametangaza kumtambua meya na kua tayari kushirikiana nae. Hata hivyo katika kile kinachoashiria Bakwata kutumiwa na CCM, viongozi hao walitoa kauli za kujichanganya huku kiongozi mmojawapo akiunga mkono kauli ya mary chatanda kwamba kumtambua au kotomtambua meya sio kazi ya viongozi wa dini bali ni suala la kisiasa. Lakini wakati sheikh huyo akitamka maneno hayo kiongozi mwingine wa kiislamu aliyekuwpo kwenye kikao hicho alisema wao wanamtambua meya wa Arusha aliyetangazwa na mkurugenzi na kwamba wako tayari kushirikiana naye. Ni wazi tamko hilo limetolewa kwa makusudi ya kuwapinga maaskofu ambao juzi walitoa tamko la kutomtambua meya wa Arusha na kutokua tayari kushirikiana nao. Inakuaje wanasema kumtambua au kotomtambua meya sio kazi ya viongozi wa dini halafu baadae nao wanasema wanamtambua meya wa Arusha na wako tayari kushirikiana nao????? Na je walikua wapi siku zote kutoa tamko la kumtambua meya wa Arusha hadi maaskofu watoe kauli ya kutomtambua meya huyo???
 
Hayo ndio madhara ya viongozi wa dini kuingia katika siasa...leo hii Maaskofu wanasema hawamtambui Meya....kesho Masheikh wanasema hawamtambui raisi. There are responsibilities that come with being a leader of a particular group, that freedom of speech has consequences when you are a leader especial when you know the strength of faith and believes...ningesema mimi, who cares 🙂....Madhara yake mtayaona maana lets not under estimate the power of faith when used irresponsibly. It's one thing to condemn the killings but taking a political stance ?? I do not Agree

1) It started before elections...the Kakobe and likes

2) It continued after elections...

3) Then the issue in Rukwa....

4) Now Arusha....

Are you following the trend...??
 
ukitaka kujua hulka ya ndg zangu Waislam ni kujiuliza ni nchi gani ya Kiislam ina demokrasia yaani vyama vingi nina uhakika katika zoote hazizidi nne! na kati ya hizo ni Turkey ambayo kila mtu anajua jinsi inavyonyanyapaliwa ati si nchi ya Kiislam kisa hawafuati Sharia law! hapo ndipo utajua demokrasia si tija kwa walio wengi ndani mwa mioyo yetu! It was juast a matter of an opportunist kushika hatamu awatumie kama mwendawazimu Kikwete anavyofanya...
 
watatoa nyingi tu. Saa hii PIUS MSEKWA kasema hategemei kila mtu atoe kauli. Wazee watalishughulikia wenyewe na sio vinginevyo. Tusubiri kauli rasmi ya wazee hao na sio kazee kenye jazba Makumbo
 
MASKOFU NA MASHEHE, KABLA YA WADHIFA WAO KWANZA NI WATANZANIA HIVYO KUKEMEA MAOVU HAKI YAO

Nashangaa sana haufu za udini anazoweza mtu kulazimisha hapa kwa MAASKOFU MJINI ARUSHA nchini ni upi huo hasa? Maana mpaka dakika hii MAASKOFU hawamtambui MEYA WA CCM JIJINI ARUSHA, ambaye naye ni MKRISTO SAWASAWA na hao maaskofu.

Kimsingi MAASKOFU walisema wazi kwamba wanachokipinga kwa meya huyu wa CCM wala si maovu ya kuwa mwana-CCM, si maovu ya UKRISTO wake isipokua MAOVU WANAYOYAKEMEA ni sheria na taratibu za uchaguzi zilivyopindishwa kumuingiza madarakani kupitia mlango wa nyuma.

Sasa viongozi wetu wa kiroho wasipokemea maovu kama haya, ukimya wao juu ya jambo hatari kama hili tafsiri yake ni kwamba wameunga mkono huo uchafu na ubakaji wa DEMOKRASIA, ndivyo watu mnavyotaka????????????????

Kama shida ni kuhusu vifo vya raia wa Tanzania na hata yule wa nchi rafiki na jirani Kenya, nadhani mtu asijaribu kuziba wengine midomo. Mauaji ya pemba 2001 vingozi wa dini walipiga kelele sana na kuikemea serikali ya Mhe Mkapa wakisema nguvu nyingi kupita kiasi imetumika dhidi ya wananchi. Katika kundi hilo kulikwepo Mashehe, Maaskofu, Mapadri na Wachungaji kwa mchanganyiko wake.

Hivyo kutokana na ukweli huu ambao iko mikononi mwao waandishi wa habari mpaka leo hii, ni matumaini yangu kwamba hauna maana yoyote kutaka kutuambia ya kwamba kama kilio cha Watanzania hakikusikilizwa tulipoipigia kelele mauaji ya Pemba basi leo hii raia tunapouaua tusiseme kwa sababu kule hatukusilizwa vile vile.

Pia, sitaki niaminishwe ya kwamba mweka hoja hii anajaribu kutuambia kwamba MAUAJI YA KINYAMA ARUSHA kwa vyovyote vile yalitekelezwa na MTU AU WATU anaowajua yeye ILI KUSAIDIA KUMLIPIA KISASI CHA MAUAJI YA PEMBA leo hii hivyo anaona hadi sasa ngoma ni droo na wala kusilalamike mtu?

Mwisho, imekuaje mtoa mada umekwepa kujiuliza maswali yote ya msingi hapa; Je, MASHEHE NA MAIMAMU kukaa kimya bila kukemea mauaji ya kinyama Arusha hadi kujitokeza tu kutetea Mhe kwa sura nyingine ya ajabu ajabu tu inamaana wanayo agenda gani?????????

Kama hataki kuyaelewa hata haya uliyoyaandika basi yeye mtoa mada ndio mdini wa moja kwa moja. Relations alizojaribu kuziweka haziendani moja ya jukumu kubwa la viongozi wa kiroho ni kukemea maovu yote yanayojitokeza katika jamii yalizopo na hili la Arusha ni haki yao.

Siasa ni maisha ya kila siku kwa kila mwananchi hivyo haijarishi wewe ni nani na unafanya nini kwa namna moja ama nyingine ni lazima ushiriki katika siasa.
 
Nafikiri kamuza unajaribu kulazimisha mambo hapa. Lazima tuelewe kuwa Tanzania ni nchi ya wote, wakristu na waislamu na hata wasio na dini. Tunapojadili kuhusu mstakabali wa nchi tuepuke chuki za kidini. Sisi sote ni ndugu, tunaishi pamoja, tunakula pamoja. Baadhi yetu katika familia kuna udugu wa damu baina ya wakristo na waislamu. Hawa watu wa nje wanaojaribu kutuletea chuki tusiwape nafasi. Kilichofanya na serikali arusha kilaaniwe na wote.
 
Mtoa mada, japo sikubaliani na swala la maaskofu kuingilia mambo ya siasa kwa sababu zinazoweza kuleta machafuko nchini. Ulichofanya hapo ni uchochezi wa kidini.
 
Back
Top Bottom