BAKWATA na Mauaji Arusha

BAKWATA na Mauaji Arusha

Kama polisi ni zaidi hapa nchini sasa tutajuana huku uraiani.

Polisi na ndugu zao wote hatutawapa ushirikiano tena huku uraiani popote pale, hatutafanya biashara yoyote na nyie na hata ukilazimisha lifti kwenye gari yangu kuna uwezekano mkubwa nikabamiza gari langu mwenyewe kwa upande uliko ili ufe sawa na raia wenzetu mliowaua kiunyama Arusha.

Tangu sasa polisi hata kama ni ndugu yangu toka nitoke tusijuane na mtoto wangu yeyote atakayejiunga na jeshi hili alaaniwe na afe mara moja hata kabla hajamaliza mafunzo hayo.
 
This was bound to happen, Maaskofu walipoingilia siasa na kutoa such a statement it was totally wrong. This statement if it was made by a group of people wether affiliated with political parties or not, this would have been OK!

NOW ITS THE TIME TO STOP RELIGIOUS LEADERS TO MAKE POLITICAL STATEMENTS BEFORE ITS TOO LATE OR WE ARE BOUND TO START KILLING EACH OTHER !!!!
acha ujinga au ficha uppuzi wako usije ukadharaulika, ni dini gani isiyokemea mauaji? angekuwa ni slaa anatawala halafu mauaji kama arusha yalitokea kanisa lingekaa kimyaa?, labda nikukumbushe robert gabriel mugabe ni mkatoliki pure, lakini yeye na kanisa katoliki ni mwiba, kwa kuwa ni jambazi la kisiasa, nenda kasome kuhusu arch bishop ncube na mugabe. kanisa lina support tsavanigai ambaye hata dini yake haijulikani simply tu anatenda haki. sasa watu wenye akili fupi kama wewe tayari unaanza kuyatazama mauaji ya arusha kwa jicho la udini. watu kama nyie ingekuwa enzi za makaburu mlikuwa mnafungiwa magurudume shingoni halafu mnachomwa moto. shame on you
 
huu ni upupu!!! Wewe unaishi dunia gani aisee? Huoni aibu kuleta bandiko kama hili hapa? Wewe ni mdini na udini hatutakaa tuupe nafasi tanzania kwani udini ni sumu kupita kiasi. Kupanda mbegu za udini ni kuyatafuta yale yaliyotokea rwanda kati ya wahutu na watutsi ila sisi hapa itakuwa ni kati wa wakristo na waislamu. Ng'oa hii mbegu mbaya ya udini kutoka kwenye jamii ya watanzania kwani ni hatari na mbaya kuliko ukoma!!! Wewe unasema hayo na umesahau kwamba meya wa arusha aliyekataliwa na viongozi wa dini ya kikiristo ni mkristo mwenzao vipi angekuwa ni muislamu hapo tena si ingekuwa ni balaa? Umepewa akili itumie kuchambua mambo na wala usije hapa kuweka mabandiko kwa ajili ya kuwafurahisha waliokutuma!!!!

nani ali-engineer mauaji ya rwanda? Kumkataa meya wa arusha ni kama adhabu kwa wote walio/wanaom-support jk. Ukweli unabaki palepale, kanisa lina hisa na cdm. Udini wangu uko wapi? Tusikariri kwamba kila anaekosoa dini fulani ni mdini. Hata padri karugendo huwa anakosoa mwenendo wa kanisa. Naye ni mdini? Umepewa akili ufikiri, fikiri sasa

umepewa akili na utashi wa kuchambua mambo usiwe kama juha asiyefahamu kutofautisha mambo
 
acha ujinga au ficha uppuzi wako usije ukadharaulika, ni dini gani isiyokemea mauaji? angekuwa ni slaa anatawala halafu mauaji kama arusha yalitokea kanisa lingekaa kimyaa?, labda nikukumbushe robert gabriel mugabe ni mkatoliki pure, lakini yeye na kanisa katoliki ni mwiba, kwa kuwa ni jambazi la kisiasa, nenda kasome kuhusu arch bishop ncube na mugabe. kanisa lina support tsavanigai ambaye hata dini yake haijulikani simply tu anatenda haki. sasa watu wenye akili fupi kama wewe tayari unaanza kuyatazama mauaji ya arusha kwa jicho la udini. watu kama nyie ingekuwa enzi za makaburu mlikuwa mnafungiwa magurudume shingoni halafu mnachomwa moto. shame on you

Wewe ndio mpuuzi kwa sababu hakuna asiyekemea mauaji, na issue sio kukemea mauaji kama utavyotaka kuipindisha. Walichofanya Maaskofu sio kukemea mauji tu, wameingia katika siasa na hilo halipingiki. Sasa kama wewe ni kipofu kwa sababu ya imani yako siwezi kukusaidia, lakini mwenye kuona ataona hilo nililosema hapo juu..
 
Kwa wakristo kutomtka Kikwete, nadhani lina ukweli ndani yake. Tazama hata humu JF, ni wakristo wangapi wanomponda Kikwete ingawa ni wazi kabisa kuwa Kikiwete ni kiongozi mzuri, mchapa kazi na ameifikisha mbali Tanzania katika miaka hii mitano.
 
Wewe ndio mpuuzi kwa sababu hakuna asiyekemea mauaji, na issue sio kukemea mauaji kama utavyotaka kuipindisha. Walichofanya Maaskofu sio kukemea mauji tu, wameingia katika siasa na hilo halipingiki. Sasa kama wewe ni kipofu kwa sababu ya imani yako siwezi kukusaidia, lakini mwenye kuona ataona hilo nililosema hapo juu..

baada ya umoja wa viongozi wa dini ya kikristo, kutoa tamko la kutomtambua Meya ya jiji hilo kwa tiketi ya CCM, Gaudence Lyimo.
 
Tatizo lingine kubwa ni maaskofu kuingilia siasa, na hii inaonyesha wazi kabisa na haipingiki. Wao, siasa ya nini?
 
Wana siri ya pamoja, lengo likiwa ni kuhakikisha wanashika nchi ili kanisa liendelee kushika hatamu na UTAMU wa nchi hii. JK kawanyang'anya utamu kupitia MoU kati ya kanisa na serikali. JK alitaka awanyime utamu baada ya mwaka jana kutaka mali zinazoingizwa na makanisa nchini zilipiwe kodi. Leo wanasema hawamtambui Meya Arusha kisa mauaji. Mbona hawakumtambua Rais baada ya mauaji ya januari 21 ambapo watu 27 waliuawa na wanawake kubakwa. AU NI SIASA ZA UZANDIKI?
wewe ni muislamu?
 
KAUMZA....kuna tafsiri tatu juu ya wewe na ujumbe wako huu.

1. Wewe ni fisadi au unafaidi matunda ya ufisadi unaotekelezwa na CCM
2. Wewe unaweza kuwa na tatizo la kusoma, kuelewa, kufikiri na kuoanisha mambo
3. Wewe ni mdini na udini wako umeuweka wazi bila kificho.

Therefore, without hesitation, I call this a MALEVOLENCE

Mkiambiwa ukweli mnang'aka na kuhamaki hii inaonyesha ni vipi mlivyo.
 
Viongozi wa dini wana haki ya kutoa matamko pale wanapoona inabidi, ila wanatakiwa wayatoe kwa utashi na uhuru wao. Lakini kama wanayatoa kwa maelekezo ya wanasiasa, hapo kuna tatizo na ni ujinga! Hawatakiwi kufuata tu upepo bila kujua unaelekea wapi!
 
Kwa wakristo kutomtka Kikwete, nadhani lina ukweli ndani yake. Tazama hata humu JF, ni wakristo wangapi wanomponda Kikwete ingawa ni wazi kabisa kuwa Kikiwete ni kiongozi mzuri, mchapa kazi na ameifikisha mbali Tanzania katika miaka hii mitano.

hapo kwenye nyekundu umenivunja moyo sana Great thinker Zomba,
Hivi wakristo wa humu JF unawajuaje au unaposoma comments za mtu anapompinga JK basi wewe moja kwa moja una mjudge kama ni Mkristo?
 
Hao viongozi wa hiyo dini wote wakuja tuu! (VYASAKA) watatumiwa sikuzote na hao punguani.
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, kinatuhumiwa kuanza mchezo mchafu wa kuufanya mgogoro wa uchaguzi wa Meya wa jiji la Arusha uliosababisha vifo vya watu watatu, kuwa wa kidini.

Habari za uhakika kutoka ndani ya chama hicho, zimebainisha kuwa katika kufanikisha njama hiyo, baadhi ya viongozi wamefanikiwa kuwashawishi baadhi ya masheikh jijini Arusha, kutoa tamko la kulaani vurugu na kupinga kile wanachodai kuwa ni viongozi wa dini kujiingiza katika siasa.


Mpango wa kuwatumia baadhi ya Waislamu kuingilia mgogoro huo ulianza tangu juzi, siku moja baada ya umoja wa viongozi wa dini ya kikristo, kutoa tamko la kutomtambua Meya ya jiji hilo kwa tiketi ya CCM, Gaudence Lyimo.


Maaskofu hao pia waliaani kitendo cha polisi kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kuvunja maandamano yaliyoandaliwa na Chadema kupinga mchakato wa uchaguzi huo.


Juzi jioni baadhi ya wanaCCM waonekana wakiwa kwenye harakati za kuwaalika waandishi wa habari kuhudhuria mkutano wa mashekhe uliofanyika jana mchana jijini Arusha, kulaani tamko la maaskofu.


"Kesho mashekh wanatoa tamko....Huu ni mgogoro wa kidini, maaskofu hawamtaki Kikwete ndio sababu wanampinga hadi Meya...Hali hii itatufikisha pabaya,"alisema kiongozi mmoja wa CCM (jina tunalo).


Kama ilivyodokezwa na viongozi hao wa CCM juzi, jana baadhi ya masheikh wa Msikiti Mkuu wa Arusha, waliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutoa tamko la kulaani vurugu, ghasia na uvunjifu wa amani uliotokea wakati wa maandamano ya Chadema.


Katika tamko hilo ambalo nakala imesambazwa kwa jeshi la polisi, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Usalama wa Taifa, Mkuu wa wilaya ya Arusha, Ofisi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Ofisi ya Meya wa Arusha na Ofisi ya Mkurugenzi, lililosomwa na Imamu wa msikiti huo, Mohamed Hambali Waislamu hao walisema tukio hilo liliwaathiri sana.


"Tumeshindwa kufanya ibada zetu msikitini kwa amani na utulivu, uharibifu wa mali ikiwa pamoja na kuchomwa moto majengo, kutupiwa mawe msikitini na watoto na wazee kuathirika," inasomeka sehemu ya tamko hilo.


Tamko hilo, pia lilisomeka "Sisi viongozi wa dini ya Kiislamu tunawakumbusha wenzetu kwamba hatupaswi kuingilia maswala ya kisiasa kwa kutoa matamko ambayo yatapelekea uvunjifu wa amani."


Kauli hiyo, ambayo inaungana na kauli ya Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, aliyoitoa juzi, inaaminika kuwa ililenga kuwasema maaskofu ambao walitoa tamko la kutomtambua Meya wa CCM kutokana na kuchaguliwa bila kufuata utaratibu.


Tamko hilo, liliendelea kusema, " sisi viongozi tunatakiwa tuwe washauri wa kiroho na kusisitiza amani iliyopo. Ni vyema watu wakafuata kanuni na sheria za nchi kama inavyosomeka katika katiba ya nchi.


Taarifa hiyo, ilinukuu ibara ya 19(2) inayosomeka,"Kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi na shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya mamlaka ya nchi"


Tamko hilo la kwanza la aina yake kwa Waislamu wa Arusha ambao kwa miaka mingi wamekuwa na misuguano na serikali ilieleza kuwa, waislamu watatii mamlaka iliyochaguliwa kwa mujibu na kanuni za nchi.


"Tunatambua ibara 107(1) mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakuwa ni Mahakama." ilisomeka taarifa hiyo.


Mwisho taarifa hiyo, ilitoa pole kwa wote walioathirika katika maandamano hayo yaliyofanyika juma iliyopita jiji Arusha ikiwamo familia za watu waliofariki dunia kwa kupigwa risasi za moto.


Hata hivyo mwenyekiti wa Kamati ya Msikiti Mkuu wa Arusha, Abdulaziz Mkindi, alikanusha tamko hilo kutolewa kwa shinikizo la CCM.


"Hili ni tamko letu sisi hatutumiwi na CCM wala serikali....Sisi waislamu wa Arusha Mjini tumeathirika sana na hizo vurugu na tunataka amani," alisema Mkindi ambaye alikuwa pamoja na Imamu Hambali.

Udini ni kichaka cha kuficha udhaifu wote. Jk analaumiwa kutokana na kushindwa kuongoza nchi. Hachukiwi kwa sababu ya uislam wake.
 
hapo kwenye nyekundu umenivunja moyo sana Great thinker Zomba,
Hivi wakristo wa humu JF unawajuaje au unaposoma comments za mtu anapompinga JK basi wewe moja kwa moja una mjudge kama ni Mkristo?

Chuwa hazijifichi kwenye mchele.
 
Hivi misikiti inapata wapi pesa za kuendesha shughuli zake ?
 
Udini ni kichaka cha kuficha udhaifu wote. Jk analaumiwa kutokana na kushindwa kuongoza nchi. Hachukiwi kwa sababu ya uislam wake.

Hapo ndipo patamu, nionyeshe moja tu aliloshindwa Kikwete, tulijadili halafu turukie lingine, nnakuhakikishia huna.
 
Wewe ndio mpuuzi kwa sababu hakuna asiyekemea mauaji, na issue sio kukemea mauaji kama utavyotaka kuipindisha.
Walichofanya Maaskofu sio kukemea mauji tu, wameingia katika siasa na hilo halipingiki
. Sasa kama wewe ni kipofu kwa sababu ya imani yako siwezi kukusaidia, lakini mwenye kuona ataona hilo nililosema hapo juu..

labda mie sielewi haya
1. Kwanini viongozi wa dini wakikosoa selikari ndipo hoja za kufanya mambo yasiyo wahusu huja? wakiipongeza hakuna maneno kabisa.
2.Kiongozi huwa na mipaka? yaani viongozi wa dini hawaruhusiwi kukosoa mfumo wa selikari yao? angalau viongozi hao wangekuwa wazungu na wanakosoa selikari ya tanzania hapo shida ingekuwepo, lakini nao ni watanzania na wanapiga na wanaweza kupigiwa kura.
3.Kwanini waislamu walaani kauli ya viongozi wenzao na sio tatizo? tatizo ni uchaguzi wa meya wa Arusha na sio kingine je waislaamu wanatuambia nini kwa mchakato wa kumpata meya ?Au kwakuwa ni wa CCM basi hapo hakuna shida?
4. Viongozi wa dini hawapaswi kuielimisha jamii?
 
While the reality is any religion in a way promote good in a society, however if not careful it can promote division
 
Back
Top Bottom