BAKWATA na Mauaji Arusha

BAKWATA na Mauaji Arusha

Nimekwisha sema awali CCM wakiumbuliwa wanakimbilia kwenye udini, huo ndo mchezo wao na engineer wa karata ya udini ili kuwagawa watanzania ni JK, na historia itamhukumu kwa kudiriki ku play udini card ili kupata political support kwa waumini wa dini flani, hii itawa cost CCM and it is a very bad strategy
 
Waulizwe hao masheikh wana elimu na kipato gani? Utakuta hata waumini wao tu wanawakataa huko misikitini. Tatizo ni elimu, kipato na utashi wa kuona mbele... Sheikh wa kweli wapo na wamekaa kimya maana wanajua kinachotokea. Hutamsikia sheikh kama Issa bin Shaaban Simba akizungumza upumbavu kama huu. Senti za kupewa na kuandikiwa matamko zinawaponza masheikh njaa hao!
 
by the way mimi sijaelewa hii dhana ya udini unaohubiriwa hapa Tanzania! udini maana yake nini? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa Tanzania kama nchi haina dini lakini wananchi wake wana dini, wengine waislamu, wakrsto kwa madhehebu yake. hatuwezi kuwa na kiongozi asiye na dini. hata kama haendi kanisani au mskitini anakitu anacho kiamini ndiyo dini yake. kwa kweli dini si zaidi ya hapo. sasa leo kuna mijadala na maombi yanaondeshwa " Mola tuepushe na udini" mnataka watu wasiwe na dini au maana yake nini?
viongozi wa siasa walijificha zamani katika kichaka cha siasa wakitaka kutenganisha dini na siasa ili wafanye maovu yao na pasiwe na mtu anayewauliza, ukifika wakati wa kupiga kura wanarudi kwa hao ambao hawataki wajue wanafanya nini! siasa ni maisha yetu, kama tunachagua watu wasio na dini iko siku watasema haina haja ya kusali/ibada. wanapopitisha mikataba mibovu na kulazimika kulipa makapuni riba na gharama za hasara je hao walio na dini hawana michango yao humo? si kodi zao wao, au wao hawana uchungu na pesa zao kwa kuwa wana imani sana? vitendo vya wana siasa vina athri jamiii nzima kwa maana ya makundi yote, walemavu, wajane, wazee, watoto, waamini n.k hivyo wanasiasa wasitupeleke katika uwanja wa mambumbumbu, Tanzania ni yetu sote yeyote anapopotoka ni jukumu la jamii nzima kulaani kitendo hicho hapa hamna suala la udini
 
Mkuu Fundi Mchundo Extemist ndani waislamu sikubaliani nao kama walivyo extremist walioko katika ukristo. Anything that is extreme is harmful ndio maana katika statistics kuna kitu kinaitwa outlier kinaweza kuharibu kila kitu ndio maana watafiti wanakijaribu kukicontain au ikishindikana kukiondoa. Lakini kaa ukijua sometimes hata mwendawazimu anakuwa anasema jambo la msingi ambalo mimi na wewe tunaweza tusilione. Hebu tizama mtiririko huu:-
a. 4th January, 1998 President Mkapa anachimba mkwala kuhusu mihadhara ya dini yenye kuleta mifarakano.
b. 8th February, 1998 Padri Lwambano anaituma serikali iwashughulikie wanaoleta mihadhara ya uchochezi na mengineyo kwa ufupi waislamu.
c. 13th February, 1998 wanatandikwa waislamu pale mwembechai na kuuwawa.

Je nikuulize does it need a nuclear scientist to know what is going on here? Pia kumbuka rais aliyeko madarakani ni muumini mzuri Kanisa la St. Peters pale Msasani (karibu na ofisi za usalama). Sasa Fundi mchundo twende turudi kuna kitu kimekosekana hapa kabla hatujawaita jamaa extremists. Pia kaa ukijua kuwa Mkapa hakuwashauri waislamu kuhusu hili jambo je nikuulize alikuwa sahihi? Tatu Padri Lwambano ni padri wa kanisa gani na je lile tamko alilitoa kama nani? Kwanini asiende kutamka mimi Camillius Lwambano nasema hivi atumie title yake ya upadri? Naomba unijibu mkuu

Itakuwaje Rais Mkapa alitumwa wakati aliishaamua mwenyewe kuwa mihadhara hiyo ni hatari? Yeye alitoa tamko Januari na Padri akatoa lake Februari laini bado mnadai kuwa Padri ndiye alimtuma?

Rais Mkapa hakuwa muumini wa St.Peters. Rais Mkapa alikuwa akisali kanisa la Immakulata lililopo Upanga. Hizo ofisi za usalama wa taifa zilikuta kanisa lipo sasa uhusiano wake na kanisa ni upi? Au unataka kutuambia kuwa kwa sababu ya ukaribu wake, kanisa ndilo linalotoa maelekezo kwa TISS? Hata wakati huu ambapo boss wake ni muislamu?

Mkapa alitoa maamuzi kama Rais wa nchi na hakuwajibika kuomba ushauri kwa yeyote yule asiye sehemu ya vyombo vya usalama wa nchi. Na ndio alikuwa sahihi hasa ukikumbuka kuwa ni uongozi wa msikiti ulioomba msaada wa polisi. Sidhani kama Rais wa nchi alihusika katika uamuzi wa kitu ambacho ni operational. Au unataka kutuambia ni Kikwete ndiye aliyeamuru mapolisi wakawadhibiti CDM Arusha? Na alifanya hivyo kwa sababu ni muislamu na CDM wamejaa wakristu?

Padri Lwambano ni padri wa kanisa katoliki na tamko hilo lilikuwa ni sehemu ya mahubiri yake kama paroko wa parokia ya Mburahati. Kuwa kwake padri hakumuondolei haki yake kama raia kukemea uovu pale anapouona. Na ukweli ni kuwa kama mtumishi wa Mungu anawajibika zaidi kukemea na kutoa tahadhari pale anapoona maovu yanatokea. Ulitaka akae kimya wakati kila kukicha watu wanapiga kelele usiku kucha kwa sauti ya juu kukebehi na kudhalilisha dini yake? Hivi nyinyi kama waislamu mngevumilia mtu kuweka kanda ya kumkashifu mtume wenu 24/7 kwa sauti ya juu? Wamepoteza roho wangapi kwa kudiriki tu kuisemea ovyo dini yenu? Leo Pakistan kuna mwanamke mkristu amehukumiwa kifo kwa kupigwa mawe kwa madai ati alimtukana mtume Mohammed S.A.W ! Na Gavana muislamu ameuawa kwa kumtetea. Halafu Mkuu, unataka kumpiga madongo mtu aliyekuwa anatuasi kuwa huko tunakoelekea ni kubaya! Haoni kwa msimamo huo hauna tofauti na hao extremists unaodai kutokubaliana nao?

Amandla.....
 
JK ni mjasiriamali mkubwa wa udini Tanzania
 
Sikujua kuwa hujui kuwa polisi hawana mamlaka ya kuzuia mikutano wala maandamanoya viumbe wowote achilia mbali ya vyama vya siasa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii ambazo zimetungwa kwa matakwa ya CCM. Nchi haiendeshwi kwa amri tena amri haramu, tuambieni polisi walpata wapi mamlaka ya kuzuia maandamano au mnashbikia wauaji kwa vile walouawa si wa chama chako? Kumbuka risasi hazikuchagua dini

unachosema haki-apply katika kila situation ndiyo maana kuwa kuna sheria mbali mbali na bylaws pia nia ni kuhakikisha nchi inaenda kwa utaratibu mzuri bila vurugu. Serikali ipo kisimamia sheria na kuhakikisha kila mwananchi habughuthiwi ama sivyo kila mtu au kikundi akiruhusiwa kufanya anavyotaka bila kufuata utaratibu/ sheria zilizopo itakuwa vurugu tu, ndiyo maana wote tunapaswa kuzifuata hizo sheria kwa manufaa ya watu wote. Chadema kuzuiwa kufanya maandamano lakini waliruhusiwa kufanya mkutano ilikuwa ni jambo jema na wangetii kauri ya serikali ili kuhakikisha usalama kwa watu wote. Kama chadema wangefuata hayo leo hii tusingekuwa na watu waliokufa na kuacha familia zao zinateseka huku mbowe na slaa wakifurahia kimoyo moyo kwamba waliyotaka yamekuwa ingawa machoni pa watu wamejibebesha nyuso za huzuni za kinafiki
 
Wakiristo watanzania, msijidanganye kabisa na kujifanya kwamba eti ni nyinyi ni "European outpost in Africa". Maendeleo ya uzungu siyo maendeleo ya ukiristo, ingawa mpo wengi sana humu ambao mnajitoa akili kwa makusudi na kusherehekea mafanikio ya wazungu "in the name of jesus", na kujifanya kama vile nyinyi ni sehemu ya "white establishment". Nasikitika sana kama mifumo ya kielimu ndiyo inayowafanya muwe hivyo.

Waislamu watanzania, msijidanganye kabisa na kujifanya kwamba eti ni nyinyi ni "Arabian outpost in Africa". Maendeleo ya waarabu na makabacholi siyo maendeleo ya uislamu, ingawa mpo wachache sana humu ambao mnajitoa akili kwa makusudi na kusherehekea mafanikio ya waarabu "MOHAMMED S.A.W", na kujifanya kama vile nyinyi ni sehemu ya "Central East establishment of Saudia". Nasikitika sana kama mifumo ya madrasa ndiyo inayowafanya muwe hivyo...
 
Yote tisa lakini kumi kwa mtizamo wangu ni Jk kumteua Makamba kuwa katibu wa chama tawala ambapo wote wawili kwa pamoja wameuleta mwanzo wa mwisho wa utaifa wetu kwa kausisi cheap politics za kidini.
Nawahakikishieni kama makamba ataendelea na mamlaka aliyo nayo kwa miaka 3 zaidi vita vya kidini vitakuwa vimeiva.
Believe me or not!!
.
 
SALAAM ALAEIKUM.Ndugu zangu waislamu wakati mwingine tusishabikie maswala kama ligi ya mpira. Inabidi tuwe analytical. Hivi tumesahau pale Askofu Polikapi Pengo alipomwambia Mkapa kuwa CCM ni kichaka cha majambaz???!!! Wakati Mkapa naye ni Mkristo!!Sasa hapo kulikuwa na udini gani hapo. Hivi kupanda kwa bei ya umeme na hali mbaya tunayoipata sasa hivi inawaathiri wakristo peke yao?? Hela ambazo serikali inataka kuipa DOWANS, hujui itawafaidia akina LOWASA,ROSTAM NA CHENGE?? Sasa hao mapapa watatu na wengine wanyonyaji wanadini hao?
Kama tusiposhikamana pmoja hawa mafisadi wataendelea kutugawa kusudi watunyonye na tubaki na chuki za kidini.
Mafisadi hawana dini,

Ndugu yangu kama kweli u Muislamu naona nawe umeangukia katika mtego wao! Hivyo hiyo habari uliyoinakili imekaa sawa kwako? Rejea kuisoma na ujaribu kutafakari contents na Kichwa cha Habari. Hivyo kuna udini wowote walioufanya Waislamu? Kama kukemea vurugu ni wajibu wa kila mtu, kama kueleza kuwa machafuko yalisababisha kutotendeka kwa ibada hiyo ni natural kuwa kwa vile hao ni Maimamu basi watazungumzia kitendo wanachokiongoza (swala).
Hivyo ndugu yangu huoni kuwa hii habari inajikanyaga? Nafikiri wahusika wa CCM kina Chatanda na wengine si wafuasi wa Kiislamu, iweje waweze kuutumia uislamu? Na zaidi si tunaona ndani ya habari kukanusha kwa mashehe hao kutumiwa na CCM?
Hii habari ni uchonganishi na ndio msingi wa awali wa kuanzishwa kwa thread hii. SI KULITAKIWA KAULI YA BAKWATA KUHUSU MACHAFUKO HAYA? Jee lengo lilikuwa nini iwapo ikijulikana wazi kuwa kwa tabia zetu ni Waislamu tu ndiyo wenye dini na udini?
 
Yote tisa lakini kumi kwa mtizamo wangu ni Jk kumteua Makamba kuwa katibu wa chama tawala ambapo wote wawili kwa pamoja wameuleta mwanzo wa mwisho wa utaifa wetu kwa kausisi cheap politics za kidini.
Nawahakikishieni kama makamba ataendelea na mamlaka aliyo nayo kwa miaka 3 zaidi vita vya kidini vitakuwa vimeiva.
Believe me or not!!
.
Waislamu wana dini wengine hawana dini? Nieleze kitendo kimoja tu ambacho Kikwete amekifanya na wasio na dini ya Kiislamu hawajafanya. Nitajie Kitendo kimoja tu ambacho Makamba amekifanya lakini hakijafanywa na kiongozi mwengine hapa Tanzania, mwenye dini tofauti na ya Makamba. Nakupa Challenge hiyo na nasubiri jawabu.
 
Waislamu watanzania, msijidanganye kabisa na kujifanya kwamba eti ni nyinyi ni "Arabian outpost in Africa". Maendeleo ya waarabu na makabacholi siyo maendeleo ya uislamu, ingawa mpo wachache sana humu ambao mnajitoa akili kwa makusudi na kusherehekea mafanikio ya waarabu "MOHAMMED S.A.W", na kujifanya kama vile nyinyi ni sehemu ya "Central East establishment of Saudia". Nasikitika sana kama mifumo ya madrasa ndiyo inayowafanya muwe hivyo...

Duh1 Ukasuku??
 
Waulizwe hao masheikh wana elimu na kipato gani? Utakuta hata waumini wao tu wanawakataa huko misikitini. Tatizo ni elimu, kipato na utashi wa kuona mbele... Sheikh wa kweli wapo na wamekaa kimya maana wanajua kinachotokea. Hutamsikia sheikh kama Issa bin Shaaban Simba akizungumza upumbavu kama huu. Senti za kupewa na kuandikiwa matamko zinawaponza masheikh njaa hao!
Eti umesema kuwa hao Mashehe hawana elimu na kipato chao ni duni ndio kiwafanye wasiseme kitu? Hawa wasiosoma ndio waliokuwamstari wa mbele kuleta uhuru wa Tanzania.
Una maana kuwa kwa kukosa elimu ndio mwananchi hana uwezo wa kutowa kauli kwa jambo linalomuhusu? Na iwe hivyo basi hayo machafuko yangefanywa kiasi cha kutowagusa wao. Hivyo elimu yako inakutuma umdharau mwenye elimu ndogo na kipato kidogo? Mbona idadi kubwa ya Watanzania ni hao.
NI hao hao ndio waliotumiwa kuleta machafuko na kama utaangalia walio muhanga ni hao unaowaona hawana elimu na kipato kidogo! Wenye elimu na kipato walihifadhiwa na kuwatowa muhanga wenzao.
Bwana msomi na mwenye kipato nafikiri elimu yako ina mushkeli kwani kama ingekuwa inafanya kazi hasa ungeona makosa ya habari hii na kibwagizo chake. Unaweza kutuonyesha sehemu ambayo habari hii ilionyesha huo udini wa Mashehe waliotajwa humu? Pengine elimu yako imeshindwa kupooza hisia zako. Pole sana Bwana msomi!!!
 
nimekwisha sema awali ccm wakiumbuliwa wanakimbilia kwenye udini, huo ndo mchezo wao na engineer wa karata ya udini ili kuwagawa watanzania ni jk, na historia itamhukumu kwa kudiriki ku play udini card ili kupata political support kwa waumini wa dini flani, hii itawa cost ccm and it is a very bad strategy

wishful thinking!!
 
Geza Ulole, its rather daft to somehow compare a social group with a religion. Christianity is a social group whereby islam is a religion. Thats why laws can be changed/amended in christianity and not in islam. Christianity has one supreme leader, "the pope" if you are catholic, or Elizabeth queen of England if you are Anglican, and so....; whereby in muslims do not have a living human figure head for eveery muslim on planet. In christianity, power and authority are centralised, Vatican if you are catholic, or buckingham palace if you are Anglican. In Islam, power and authority are decentralised and every community have their own leadership. In short, the sheikh of mecca is only for mecca and he is not superior to sheikh of moldova or paraguay. I have hibernian background and studied christianity at depth, and believe me, when I decided to study other faiths, judaism, islam, budhism, etc; I was confounded by the *** which I was taught as a christian child. Learn about other faiths and you don't have to follow them. That will give you a little bit of respect of others.

Hivi religion ni nini? the way i see it Islam is a CULT.
 
what about Malaysia?

Do you think your views build a national solidarity?

Religion is a very sensitive issue. Tuwe makini.

Malaysia hakuna demokrasia ya kweli. wa-Malay ambao wengi na ni Wasilamu jifunze how they treat other ethnic and religious groups. They are brutal, insensitive and bullies.
 
Mimi huwa napenda kusoma hoja zako kwa sababu zinanisaidia kujua vichaa wana mawazo gani...Ila leo nimegundua kuwa ukichaa wako ni mkubwa kuliko nilivyodhani mwanzo au labda ni bangi umezidisha.

Kwa hiyo wewe ni stalker wa kichaa? mbona unatia huruma hivo?
 
..dah, tukiendelea hivi na serikali isipokuwa makini na huu uchochezi, tutagawana nchi kama Somalia na Sudan.
Tulikuwa tunawacheka Wakikuyu na Waluo, Wahutu na Watusi, na wengine Wapemba na waunguja...safari hii joka linakaribia mlangoni...

Tulijidanganya na "Nyoka huyo!, na apite!"
 
Jamani stop making every thing about RELIGION! Whatever happened to good and bad, right and wrong? People make mistakes and they stand to be corrected, it's a shame if we, who have been given the privilege of education at the expense of the taxes and hard work of our fellow poor country men & women, and who are considered the intellectual cream of our nation fail to discuss problems in our society in the broader light and confine ourselves to bias and religious sentiments!

Can we for once put our religiousity aside and see things for what they really are?

Can we agree that Mkapa gave this country's land, natural resources & companies to 'investors', friends & fools on a silver platter (refer to Kiwira, TTCL, radar deal, dubious mining contracts etc)without need to cry "udini"? As the current president Can we openly and critically discuss social economic direction of this country since Kikwete has taken realms of power (our education system,our living standard and the disputed election results) and the dubious scandals that have hit his administration (richmond/dowans, loliondo) without need to cry "udini"?

Lets look at our true intellectuals, ones whose intellect & determination to serve our nation have excelled beyond our borders: Prof. Shivji, Prof.Chachage, Prof. Haroub Othman(R.I.P), Dr. Salim.A.Salim, Jenerali Ulimwengu & J.K. Nyerere to name but a few, what can we learn from them?

Let's call a spade for what it really is and the truth of the matter is, if we look deep inside our hearts and use our heads we can advice our nation, criticise constructively, commend or strongly stand against what seems to take our country in a wrong direction without medling with our religions.

Let's start now before it's too late!
 
kuna vitu vinaitwa MALENGO na MKAKATI_lengo la wanaharakati wote kwasasa nikuona kunakuwa na Mabadiliko ya Kiutawala_mambo mengine yote ni Mikakati_hali kadhalika tuandikapo Posts huwa ni Mikakati kwa ajili ya mambo fulan tunayoyalenga_ni vema kufikiri sana kabla hujafanya jambo_kwa post hii nadhan umetuma wakati ukijisaidia choon_haimsaidii yeyote hata familia yako hainufaiki kwa post hii_otherwise mnatukatisha tamaa waislam tuliomo chadema kwamba inawezekana chadema ni ukiristo na sisi tunawasindikiza kwenye move zenu_kwann harakat za kisiasa zizungumzie iman wakat wanaharakat ni wenye iman tofaut na tunaunganishwa na MALENGO? Hii inanitia shaka na kunifanya niamin kuwa inawezekana mh. Zitto yupo sahih kuwa kuna udin ndan ya cdm_nimekuwa kwa muda mrefu nikikemea mambo haya na kuwaomba mods kupinga vitu_lakin posts zinazofutwa ni zile zinazokemea mambo haya ndizo hufutwa

Tunalazimika,

Usiwe na wasiwasi ndugu yangu. Joto la kidini ni kali kwa watu wengine. Na nadhani tuwaangalie tu hakuna haja ya kupoteza muda nao. Wataelewa tu baadaye kuwa Tanzania na hasa Tanganyika iko beyond mirengo ya kidini. Sidhani kama BAKWATA wana umuhimu wa kutoa tamko. Hii nchi ina umbwe la uongozi. Hatuna kiongozi - Naona kama nchi inaongozwa na Luteni Yusuf Makamba. NI HATARI SANA!
 
aFRO,

Umenena vizuri, Mungu akubariki. Makosa wanayotenda hawa jamaa ni kinyume cha misingi ya dini yoyote hata bila dini ni kinyume cha maadili, mila na destruri zetu. Sehemu kubwa ya watu wa ulaya hawana dini na wanasema waziwazi lakini wanaheshimu taratibu na sheria walizojiwekea. Sisi wakubwa wanasimamia na kutunga sheria halafu wanazivunja wenyewe. Ajabu sana. Uhuru wa mahakama umepotea na haki sasa inatolewa kufuata matakwa ya watawala na wenye nguvu ya kifedha. Nadhani haya ndiyo matatizo.

Lakini swali ni wangapi leo hasa ambao tumeachwa na mfumo nje tukipata nafasi tutafanya tofauti? Saa zingine tu wazuri wa kukosoa ukiwa pale ndani unageuka! Maalim Makamu wa kwanza wa rais wa zanzibar akiwa upinzani alikataa kuyatambua mapinduzi ya 64, lakini leo anashadidia wafuazi wake wajitokeze kwa wingi kusherehekea Mapinduzi hayo. Ni binadamu wachache sana wana principles wanazozisimamia hata ikibidi wafe. Wanamini kwazo na hawateteleki hata kama wengi watakuwa kinyume chao. Sisi wana jamii mmoja wetu akipata nafasi, je atafanya tofauti?

Kwa mazingira yanayomkabili JK tunamshauri afanyeje? Kuna watu anoamini bila wao asingekuwa raisi, hao ndio anaowatumikia. Hawezi kwenda kinyume na matakwa yao. Wana fedha, wana jeuri. Ndiyo mambo aliyoyasema Mwalimu. Ukienda ikulu kwa pesa, utazirudishaje kwa hao waliokupa? JK sasa analipa, na tujiandae miaka hii mitano ni ya kulipa na bahati mbaya itabidi tumsaidie kulipa tutake tusitake.

INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom