Genekai
R I P
- Feb 9, 2010
- 12,514
- 5,003
Kuna kila dalili kwamba Chama cha mapinduzi CCM kimeamua kutumia BAKWATA mkoani Arusha kupingana na kauli ya maaskofu ya kutomtambua meya wa Arusha. Bakwata wametangaza kumtambua meya na kua tayari kushirikiana nae. Hata hivyo katika kile kinachoashiria Bakwata kutumiwa na CCM, viongozi hao walitoa kauli za kujichanganya huku kiongozi mmojawapo akiunga mkono kauli ya mary chatanda kwamba kumtambua au kotomtambua meya sio kazi ya viongozi wa dini bali ni suala la kisiasa. Lakini wakati sheikh huyo akitamka maneno hayo kiongozi mwingine wa kiislamu aliyekuwpo kwenye kikao hicho alisema wao wanamtambua meya wa Arusha aliyetangazwa na mkurugenzi na kwamba wako tayari kushirikiana naye. Ni wazi tamko hilo limetolewa kwa makusudi ya kuwapinga maaskofu ambao juzi walitoa tamko la kutomtambua meya wa Arusha na kutokua tayari kushirikiana nao. Inakuaje wanasema kumtambua au kotomtambua meya sio kazi ya viongozi wa dini halafu baadae nao wanasema wanamtambua meya wa Arusha na wako tayari kushirikiana nao????? Na je walikua wapi siku zote kutoa tamko la kumtambua meya wa Arusha hadi maaskofu watoe kauli ya kutomtambua meya huyo???
Hapo kwenye RED ndo pamenigusa! Shule mkuu ndo tatizo lao!