Bado haingii akilini mtu anawezaje kuuawa na risasi mbele ya Askari jeshi wa nchi husika ?

Bado haingii akilini mtu anawezaje kuuawa na risasi mbele ya Askari jeshi wa nchi husika ?

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
5,752
Reaction score
10,523
Toka tarehe 29 mpaka leo bado nawaza mwananchi anawezaje kulengwa shaba mbele ya askari wa jeshi la wananchi naye askari akabaki anashangaa tu kama sanamu.

Moja mwananchi anapigwa virungu mbele ya askari jeshi, jeshi bado linashangaa inafuata anauawa bado tu mwanajeshi anashangaa wala hatua zozote za maana achukui hii inawezekana vipi wakuu ?

Mimi kwangu bado hainiingii akilini wakuu mbaya zaidi wanajeshi baadhi wanageuka kuwa kama watoa huduma ya kwanza wanawapakia kwenye magari yao majeruhi wa risasi hili ni jeshi la namna gani yote haya yanafanyika mbele yao.

Binafsi sijawahi kuwa na imani kubwa sana na jeshi la wananchi kwa kipindi kirefu ila kwa yaliyo tokea Oct.29 mbele yao ndio yananishangaza sana

Pia msimamo wangu sio jeshi kuchukua nchi mpaka sasa ni huo ila yale polisi walifanya mbele yao hakuna jeshi la wananchi hapa Tanzania kuna kitu kikubwa sana hakipo sawa ndani ya katika mfumo wao mzima toka juu kwenda chini.
 
Nasikia pia kuna mkoa askari wao waliuawa na polisi wala hakuna hatua jeshi ilichukua sijui kama hii habari ya kweli
 
Hivi IGP Wambura ndio CDF ?
 
Lakini mwanajeshi kupigwa shaba ndani ya nchi yake mahali ambapo hata sio vitani hii ni hatari
Ni hatari ndio , binafsi kama bado jingekuwa nipo kwenye service, ningeopen fire kwa police, niaingevumilia kuona wana attack mwenzangu halaf nakodoa macho tu
 
Ni hatari ndio , binafsi kama bado jingekuwa nipo kwenye service, ningeopen fire kwa police, niaingevumilia kuona wana attack mwenzangu halaf nakodoa macho tu
Ngumu kuvumilia kwa yale yaliyokuwa yanafanyika
 
Tena raia walikuwa wanalengwa na wanajeshi wa nchi jirani na vikosi vya kihuni vilivyovalia kiraia huku wanajeshi wakiwa wameangalia tu kwakweli binafsi nimeona hapa tumekuwa tukidanganywa hamna jeshi au ni mifumo ya ulinzi imeshavurugika
 
Toka tarehe 29 mpaka leo bado nawaza mwananchi anawezaje kulengwa shaba mbele ya askari wa jeshi la wananchi naye askari akabaki anashangaa tu kama sanamu.

Moja mwananchi anapigwa virungu mbele ya askari jeshi, jeshi bado linashangaa inafuata anauawa bado tu mwanajeshi anashangaa wala hatua zozote za maana achukui hii inawezekana vipi wakuu ?

Mimi kwangu bado hainiingii akilini wakuu mbaya zaidi wanajeshi baadhi wanageuka kuwa kama watoa huduma ya kwanza wanawapakia kwenye magari yao majeruhi wa risasi hili ni jeshi la namna gani yote haya yanafanyika mbele yao.

Binafsi sijawahi kuwa na imani kubwa sana na jeshi la wananchi kwa kipindi kirefu ila kwa yaliyo tokea Oct.29 mbele yao ndio yananishangaza sana

Pia msimamo wangu sio jeshi kuchukua nchi mpaka sasa ni huo ila yale polisi walifanya mbele yao hakuna jeshi la wananchi hapa Tanzania kuna kitu kikubwa sana hakipo sawa ndani ya katika mfumo wao mzima toka juu kwenda chini.
Majeshi yote ni mali ya CCM
 
Lakin hata walichokifanya cha kuzurula barabaran kidogo walionesha hatua

Nazan wakat mwingine wanaweza fanya kitu,ingawaje sipend yatokee,nimeshachoka mim
 
Jamani pazeni sauti sana sana,hawa watoto wanateswa huko balaa.Kuna mmoja ameonekana na majeraha ya kuchomwa na pasi, si sawa kabisa.

Eeee Mungu tenda jambo tupone.
 
Hay mambo kuacha watu waliokuwa na nguo za kiraia kuwa silaha na kuwa wanazitumia dhidi ya raia wasiokuwa na silaha itawagharim bigtime.

Malipo sji mbinguni. Ushauri wa hovyo sana kama ni mbinu za kimedani.
 
Jeshi limesaliti katiba pakubwa sana, limesaliti raia pakubwa sana, limesaliti nchi pakubwa sana na kiujumla jeshi limepoteza maana yao mbele ya raia kwa kiasi kikubwa. Watu wanasema kama jeshi nalo linakosa uzalendo basi suala la raia kuwa wazalendo kwa nchi yao utakuwa msamiati wa chuo kikuu
 
Nchi za jirani washasoma weakness ya jeshi mda wwte wanajjingilia tu
 
Back
Top Bottom