Babie Kabae na Udini Clouds Tv

Babie Kabae na Udini Clouds Tv

"Asalaam aleykum" (Amani iwe juu yako) ni zaidi ya salamu mkuu (ni dua pia).

"Habari za asubuh" umeamkaje"... salamu za kishashi hizi hazina hata maana
Anasahau kuwa hata Yesu ndio ilikuwa salamu yake, anadis kisa kasikia kiarabu
 
Huyu dada ni mtangazaji mzuri sana ila anakera sana kila siku anakomaa kutuhubiria habari za uislamu, kutufafanulia mafundisho mbalimbali ktk vipindi vya 360, nilidhani ananikera mimi tu ila nimewahi kukaa vijiwe zaidi ya viwili tukawa tunaangalia 360 nikasikia watu wengine wakikerwa pia.

Baby Kabaya we fanya kazi iliyokupeleka, habari za kutufundisha uislamu peleka Iman Tv huko au nunua kipindi maalumu. Kila mtu hapo clouds akianza kufafanua mafundisho ya dini yake hapatatosha. Acha hayo mambo.
Hakika anakera sana aache misifa za kijinga kama anataka kuzungumza dini aombe kipindi kama akina shekhe yahaya
 
Hivi leo ni lini? Naona mlianzia usabatoni sasa mnaelekea Clouds kwa Kabaye na uislam. Sijui mkitoka huko mtaenda kwa nani? Labda Yericko Nyerere aje atusaidie.
Sema aje akusaidie, unadhani kila mtu anahitaji fikra za yericko ili aweze kupambanua mambo
 
Hivi vipindi watu walio serious na kazi hawavifahamu huyu baby kabaye hata simfaham, unaangalia tv saa 12 asubuhi una akili wewe?

Naamka saa 11, fanya mzoezi 30 mins, oga na kuvaa 15, baada ya dk 15 nipo azania front church nnapata upako, mpaka saa 1.45 ninakuwa nimeshafika ofisini, kazi, kazi,kula, kazi tena mpaka saa 11 jioni, narudi home saa 2 natoka home ninaenda kwa mchepuko/baa au movie mpaka saa 6 - 7, narudi kulala. Muda na TV na baby kabaye sina
 
Babie kabae ni mtu ambae anajitahid sana kuwa neutral linapokuja suala la imani jafika kipind chake,kwann hujawah kumshangaa na kumdiss anapozipromote pasaka na christmass kwny clouds 360???mm ni Christian lakin huyu dada umemuonea,labda kama unamwonea wivu maana wanawake kw wanawake hampendani
Nani mwanamke? Kile si kipindi cha dini aombe kipindi cha dini au aende TV Iman
 
Hebu jisumbue kidogo kutafuta maana ya hyo salamu unayoilalamikia kwa kiswahili halafu urudi hapa, wakristo mna matatizo sana.
Waarabu wamewaharibu sana nyie, ndomaana huko Mombasa na pemba wamewaharibu kila kitu
 
Ni kutawaliwa kifikra tu mkuu, wala tusiwalaumu wanaotumia hiyo salaam coz waafrika tumetawaliwa kuanzia akili hadi makalio.

Mtu anaona uzito kusema "habari ya asubuhi", ambacho ni kiswahili kizuri ila kwake kutumia kiarabu kusalimia ni fahari sana.

Ni sawa na mwingine kusema "good morning", zote ni matokeo ya kutawaliwa kuanzia ubongo hadi makalio.
Hapo umenena kiongozi
 
Hivi hapa tatizo ni Baby Kabaye kuongelea dini? Au tatizo ni dini ya kiislamu? Maana mwisho wa siku kazungumziwa Mungu au sio? Sasa ni lini imeanza kuwa dhambi au kinyume na sheria kumzungumzia Mungu?

Aisee Mungu ni mmoja na hakwepeki katika uhai wala kifo wala hatupungukiwi na chochote tukisikia anazungumziwa, sana sana tunaongeza kitu katika uelewa wetu! Tujifunze kukubali kwamba kuna binadamu wako tofauti na sisi, hata iweje hakuna siku wote tutakua sawa hapa duniani (sijui wakati/baada ya kifo)!!
Tatizo ni kuingiza maudhui ya dini ktk vipindi ambavyo si vya dini
 
We na we uwe unaelewa mtu kaandika nini.....

Mwenzako anacholalamikia ni kuwa huyu dada ni kama anakuwa anafanya campaign ya dini au kiimani katika kipindi ambacho maudhui yake si ya kiimani.

Hivyo vipindi unavyovisema hata vya imani ya kiislam vipo, na huwa vinakuwapo msimu wa Ramadan na hata siku ya ijumaa ambapo waislaam huwa na ibada.....

Hiyo jumapili ni siku ya ibada kwa Christians na ndio maana gospel huwa zinapigwa karibuni kila channel ya television isipokuwa siku za katikati ya wiki.....

Sasa wewe ni nini hiki unasema.....elewa complain ya mtu na usiichukulie kirahisi au kwa mitazamo ya kukopi na kupest bila kutafakari.
Shukwani mkuu, pokea like yangu
 
Waarabu wamewaharibu sana nyie, ndomaana huko Mombasa na pemba wamewaharibu kila kitu
Hata mapadre na makasisi huwaharibu watoto wasio na hatia au hujui hilo?
 
Hivi vipindi watu walio serious na kazi hawavifahamu huyu baby kabaye hata simfaham, unaangalia tv saa 12 asubuhi una akili wewe?

Naamka saa 11, fanya mzoezi 30 mins, oga na kuvaa 15, baada ya dk 15 nipo azania front church nnapata upako, mpaka saa 1.45 ninakuwa nimeshafika ofisini, kazi, kazi,kula, kazi tena mpaka saa 11 jioni, narudi home saa 2 natoka home ninaenda kwa mchepuko/baa au movie mpaka saa 6 - 7, narudi kulala. Muda na TV na baby kabaye sina
Azania front then mchepuko. Sas si unafuta upako?
 
Azania front then mchepuko. Sas si unafuta upako?

Mkuu, kila mtu ana mapungufu yake mimi ni binadamu sio malaika, nina mwili na roho nitabadilika tuu ila hiyo ndio ratiba yangu
 
Uzi ushachafuka na watu wameanza kuonesha rangi zao halisi.
 
Mpelekeeni taarifa na kama yuko huku umesikia maoni ya wasikilizaji, sio ukishika mic unabwabwaja chochote sehemu tofauti. Kama ni kipindi cha dini sawa mwaga nondo zote za kidini lakini vipindi kama ni vya mabo mengine kumbuka kuwa wasikilizaji ni wa imani tofauti
 
Vinalipiwa mkuu na ni vipindi maalumu kama vile vipindi vya dini ya kiislamu TBC, ITV na Channel 10 siku za ijumaa, hivyo havina shida kabisa maana ni maalumu kwaajili hiyo, 360 sio kipindi cha dini
mfumo kiristu unakusumbua ndg pole xn
 
Back
Top Bottom