Ninajua kinachokusumbua ni elimu yako ndogo katika mahusiano na watu walio na imani tofauti na wewe.
1. Nani asiyejua salamu hiyo ulioitaja inatumiwa na ninyi
2. Nani asiyejua kuwa hayo ni maneno ya kiarabu yenye maana ya amani iwe nawe?
3. Sasa umeeleza salamu ya wakristo lakini nikuhakikishie hakuna mkristo anayemsalimia mtu ambaye sii wa imani yake kwa salamu hiyo
4. Hata maneno yake yawe mazuri vipi , kwa kitendo cha kuwa ndio salamu rasmi ya dini fulani ni makosa makubwa sana kulazimisha kumsalimia mtu wa imani tofauti kwa salamu ile
5. Salamu maana yake unamtakia heri na yule anayesalimiwa anatakiwa afurahi kwa maneno uliomtamkia, kinyume na hapo ukinisalimia kwa salamu inayotumika kwenye dini yako naona zaidi u nanikebehi zaidi ya kunisalimia na umeshaniaribia siku hapo, maaana ninaanza kukuchambua sababu ya wewe kunisalimia salamu hiyo huku ukijua fika ni wa imani nyingine.
6. Kwa taarifa yako hata wakatoliki uliowataja wana salamu ya kilantini yenye maana kama hiyo "Pax vobiscum" lakini hawaitumii kwa watu wa imani nyingine kwa sababu kilatini ni lugha rasmi ya kanisa katoliki , kama ilivyo kiarabu lugha rasmi ya dini yenu. Ukishslijua hilo ili kuendelea kuishi kwa mahusiano mazori ya kuonyesha kuto kudharau imani za watu wengine ni vyema kama kuna salamu ya lugha ya kigeni mnayotumia miongoni mwa waamini wa imani fulani muendelee kuitumia ninyi kwa ninyi, na mnapokutana na mtu wa i mani nyingine, tumia salamu ya kawaida ya lugha ya taifa hata kama haina tafsiri nzuri kama unavyotaka, hata kama imetoholewa kwenye lugha nyingine sii kitu. Ni vyema kutokunisalimia kabisa kuliko kunisalimia kwa salamu ambayo itanikera. Haya kama mkatoliki akikomaa sasa naye awe anakusalimia "Pax vobiscum" wewe utajibu nini ama utafurahi? Hata kama anajua namna ya kujibu ama unajua maana yake si utaamini anataka kuiona salamu ya dini yake ni suprime over oll other?