' Unakutana na mtu kwa mara ya kwanza haufahamu imani yake lakini salamu unamsalimia ya dini yako, ama unafahamu fika imani yake lakini wewe kwa kukariri ama ukorofi tu unaanza kumsalimia kwa salamu unayoitumia kwenye dini yako!! je ! yeye akikusalimia ama akakakujibu kwa dini yake utafurahiama utajibu. Tujifunze ustaarabu wa kuishi na imani nyingine bila kuwakera. Tanzania ndio nchi yenye baraka ambayo wengi tumezaliwa tukajikuta tunaishi pamoja imani tofauti kwa kushirikiana. Nadhani kuna watu wamezaliwa sehemu ambayo imani ya dini yake imekuwa ni sehemu ya mila na desturi zao kutokana na hilo salamu za kidini zimekuwa ni salamu rasmi kwa kila sehemu, lakini unapotoka nje ya eneo hilo ama unapopata mgeni usiyejua imani yake, usimkwaze kwa salamu yako jitahidi umsalimie kwa salamu ya kiswahili baada yakujua imani yake waweza kuendelea na salamu za kiimani. Kama ni siku ya ijumaa kafanya hivyo huyo mtangazaji ni sahihi na sii mbaya kwa sababu tunajua siku ya ijumaa kuna vipindi maalumu vya dini hiyo na ni siku yao na wala haina shida yoyote kama ilivyo jumapili kwa upande mwingine. Lakini kama anafanya hivyo kila siku basi atafutwe na watu wake wa karibu aelimishwe.