Mtangazaji wa Cloudstv 360 Sam Sasali asema mnaoichukia Clouds tv hamieni Kwingine hamjalazimishwa Kuwaangalia Wao tu

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Akizungumza Asubuhi ya leo pamoja na Mbilikimo mwenzie Hassan Ngoma katika kile ninachokiita kuwa ni Majibu yao dhidi ya Uzi wangu wa Jana hapa hatimaye na leo tena Mtangazaji wa Cloudstv 360 Samuel Nathaniel Sasali a.k.a Emollo Jolly Bebe ametoa Kauli ambayo hajui kuwa inaweza hata Kuathiri Mapato ya Kibiashara katika Kampuni yangu Kimatangazo na hatimaye akaishia Kukosa Mshahara wake kwakuwa ni kupitia hayo Matangazo ndiyo Yeye na Familia yake nzima njia yao ya kwenda Uani ( Chooni / Msalani ) haioti Nyasi.

Baada ya Kombora Kali lililorushwa nami Jana Kwake Mtangazaji Hassan Ngoma na hatimaye Kufika mahala pake hatimaye leo hii Mtangazaji Mwenza Sam Sasali bila hata kuifikiria kwa marefu na mapana Kauli yake amesema kuwa kama kuna Mtu yoyote anadhani Kipindi cha Cloudstv 360 na hata Vipindi vingine vya Clouds tv vinawakwaza basi waache mara moja Kuangalia na wao hawajali Kitu na wanasonga mbele.


Mimi nawashangaa sana Watu ( hapa akinilenga Mimi Cleverbright wa JF ) kama unakichukia hiki Kipindi na Clouds tv si ubadilishe tu Channel na utizame Channels nyingine? Kwani Sisi tumekulazimisha ututizame? Sisi ndiyo Timu ya Taifa na tutaendelea Kusifu juhudi za CCM, Rais JPM na Serikali yake huku ikiwezekana tukiwaponda kila mara Wapinzani hadi mkome na wala hatujali kwakuwa Sisi ni Timu ya Taifa. Msituchoshe tafadhali TV Stations zipo nyingi na wala hatujawaiteni au kuwalazimisha mtuangalie “ alisema Mbilikimo Emolo Jolly Bebe (Sam Sasali).

Labda nimsaidie tu Mtangazaji Sam Sasali pamoja na kwamba Siku hizi anapendeza mno na Kuvalia Suti zake za Tandale Uzuri kwamba anaweza kudhania kuwa Kauli yake hii haina madhara Kwao ila kwa tuliopo katika hizi Tasnia za Kimawasiliano, Habari na Matangazo kwa muda mrefu hii Kauli yake inaweza kuwa na madhara hasa Kibiashara na akajikuta anawaponza hata Wafanyakazi wenzie kwa kukosa Mishahara yao na wakaishia tu kupigiana Miayo pale Mjengoni Kwao huku wakiishia tu Kushiba harufu za Samaki za pale Escape One ambako ni Jirani sana nao.

Ni nani aliyemthibitishia Sam Sasali kwamba 100% ya Watazamaji na Wadhamini ( Sponsors ) wa Kipindi chao cha Cloudstv360 na Vipindi vyao vingine katika Tv Station yao ni wana CCM pekee? Hivi hao Watu ambao huwa wanawapelekea Matangazo huwa Kwanza wanawaambia kuwa Wao ni wana CCM? Hivi Sam Sasali anajua ni Vigezo gani huwa vinatumika hadi kuweza Kumvutia Sponsor kuja Kudhamini Product au Service yake katika Chombo cha Habari? Hivi Sam Sasali kabla ya Kukurupuka na Kuhemka Kuitoa hiyo Kauli alishaipima Kwanza na kuona kama haitokuwa na Madhara Kibiashara au alijua akiitoa tu vile atakuwa ananikomesha Mimi cleverbright wakati ukweli ni kwamba wala hajanikomoa na hawajanikomoa san asana leo ndiyo wamedhihirisha kuwa Utangazaji wao ni wa hovyo hovyo na pengine ndiyo maana Siku hizi kila Kukicha wanaishia Kudharaulika tu japo Wao wanaweza wakawa hawajui.

Pia nitumie nafasi hii kutoa Pole zangu hasa kwa Mtangazaji Hassan Ngoma kwa jinsi Uzi wangu dhidi yake wa Jana ulivyoweza Kumtibua kiasi kwamba leo katika Kipindi chake mara zote anaonekana Kuujibu Uzi wangu na hii inaonyesha kwamba Lengo langu limetimia na kwa upande mwingine najiona Mshindi kwani kama Uzi wangu ule usingemuuma kamwe asingelala Usiku Kucha anauwazia na leo kila mara anaukumbushia huku akiujibu Ki Kike Kike na Mapovu yakimtoka hadi mengine yanaangukia Meza yao na Simu yake pale Studioni walipo.

Nasikitika sana tu pia kwamba Mtangazaji wa Kike ambaye Kwangu Mimi ndiyo namuona ni Mwerevu Upstairs kuliko wote Bi. Babie Kabae ( aliye Ziarani Marekani kwa sasa ) nae akiwa amebadilishwa Kitabia na hawa Watangazaji wawili Hassan Ngoma na Sam Sasali wakati huko nyuma alipokuwa na DED wa Mbulu sasa Mwanatasnia Hudson Kamoga walitengeneza Chemistry nzuri mno kiasi kwamba Kipindi chao hicho cha Cloudstv 360 kiliweza Kubamba ( Kupendeza ) na Kupendwa na wengi kwakuwa walikuwa hawana Unafiki katika Utangazaji wao na wala walikuwa hawaonyeshi Kujipendekeza kama ilivyo sasa.

Ukiondoa tu Kichwa ( Genius ) aliyeondoka duniani Marehemu Ruge Mutahaba hapo katika Kampuni yao nzima ya CMG ukiachia mbali Mmiliki Joseph Kusaga Kwangu Mimi nadhani kuna Watangazi wawili tu ambao sina Mashaka nao hasa Kiakili na ni Werevu ( Geniuses ) hasa na ambao kwa Maoni yangu wangepaswa kuwa ndiyo wanatengeza Chemistry nzuri na Bibie Babie Kabae ambao ni Masoud Kipanya na Ciza lakini siyo hizi Takataka mbili ambazo badala ya Kuongeza Viewers kwa kuwa na Maudhui yenye Mashiko wao ndiyo Kwanza wanawakwaza Viewers na hatimaye wanakimbiwa.

Na labda niuambie tu Uongozi mzima wa CMG hadi DG Kusaga kuwa kama hamtoliangalia hili kwa Kina na hasa huu Utangazaji wa Kipashkuna ( Kishangingi ) alionao Mtangazaji Hassan Ngoma na ambao ameshamuambukiza sasa na Mwenzake Sam Sasali ( Emolo Jolly Bebe ) kuna hatari sasa Watu wengi wakahamia katika Kipindi cha BARAGUMU Live cha Channel Ten kilicho na Watu kama akina Mwalimu Albert Kilala, Dada Mrembo Vida Roy, Moses Muntente na wengineo ambao kwakweli kwa sasa wanaanza Kuonekana kuwa ni Substitute nzuri kwa Kipindi cha Cloudstv 360. Na kama Utangazaji wa BARAGUMU Live utaendelea hivi huku wakiongeza Ubunifu mwingine kidogo basi Watanzania wengi wenye Akili na tusiopenda Unafiki wala Upumbavu tutahamia huko.

Yangu ni haya tu kwa leo na najua na Kesho tena mkiwa katika Kipindi chenu hicho cha Cloudstv 360 kama kawaida yenu mtakukuruka na Kuwashwawashwa katika Kunijibu hivyo name nichukue nafasi hii kuwatakieni Kheri katika hilo japo ninawalaumu sana kwamba mliponijibu leo hamkunitaja Jina langu cleverbright wala huu Mtandao mzuri wa Watu Makini na Werevu kuliko nyie Wawili hivyo nawaombeni basi Kesho mkiwa mnanijadili msisahau Kunitaja cleverbright na pia Kuutaja huu Mtandao tafadhalini.

Natamani mno Siku moja niione hii Chemistry ya Babie Kabae, Masoud Kipanya, Ciza na Paul James ndani ya Cloudstv360 kwani hawa ukiachilia mbali Umahiri wao katika Utangazaji na Ubunifu pia wana Zawadi moja Kubwa sana waliyozawadiwa na Mwenyezi Mungu ambayo ni ya Akili ( Uwerevu ) hivyo watakuwa wanakitendea vyema kabisa hicho Kipindi na hawa Wapuuzi ( Watu wa hovyo hovyo ) Wawili wanaweza wakatafutiwa Kipindi chao na Wakakibatiza hata Jina zuri tu la Wapuuzi Hovyo Hovyo Show.
 
Kwahiyo wao wanakuja kufuata jibu lao JF na wewe hua unaenda kuangalia TV kusubiri ujibiwe.

Ukijibiwa, unakuja tena kujibia JF na wao wanachukua jibu lako wanalifanyia mchakato na kukuandalia jibu ambalo wewe utalifuata tena kwenye kipindi chao.

Huu ugomvi ni wa kindugu mno
 
Uzi mrefu Sana huu, unachosha kusoma kwa maana pia hauna vitu vya kujifunza wala kuvutia.

Point ni Kama kweli huyo Mtangazaji kasema hayo maneno basi anatakiwa,achukuliwe hatua za kinidhamu na ofc yake ikiwezekana afukuzwe kazi maana anaonekana hana ufahamu na Elimu bora hata kuhusu masuala na maadili ya utangazaji.

Ila kwa upande wako pia inaonekana unamatatizo makubwa kichwani,unatumia muda wako mwingi kufatilia Mambo ya watu bila faida yeyote, kwa lugha ya Kiswahili sanifu wewe unafaa kuitwa Mnaa, Mbeya, Mtu wa Majungu nk. Msipende kutumia JF kuripoti vitu vya kijinga Kama hivi, peleka maoni kwa bosi wake au andika Facebook huko. Huu ni upumbavu!
 
Ni ngumu kukutofautisha wewe na huyo Sam Sasali (ambaye umemuita emolo na majina mengine)
Ulishindwa kujenga hoja bila kudhalilisha umbile lake la ufupi?
Inaonekana hizi ni personal attacks baina yenu.
Wote, wewe na Sam mna namna sawa katika kujenga hoja; hamtafakari bali mnaropoka tu.
 
Ni ngumu kukutofautisha wewe na huyo Sam Sasali (ambaye umemuita emolo na majina mengine)
Ulishindwa kujenga hoja bila kudhalilisha umbile lake la ufupi?
Inaonekana hizi ni personal attacks baina yenu.
Wote, wewe na Sam mna namna sawa katika kujenga hoja; hamtafakari bali mnaropoka tu.

Kama una Undugu nae / nao mwambie / waambie wapunguze Upumbavu wao tafadhali.
 
Back
Top Bottom