Baba yangu aliniambia hanikumbuki, niliumia sana

Baba yangu aliniambia hanikumbuki, niliumia sana

Achana naye wala usimtafute tena..kama ukiendelea kumtafuta basi atakuaibisha sana..
 
Nilivyopata akili nilitamani kumjua baba yangu mzazi hapo nikiwa darasa la 5, baada ya kuona marafiki zangu wote wapo na wazazi wao wawili.

Nikafuata mama na kumliza juu ya habari ya baba yangu, mama hakunipa jibu la kueleweka zaidi ya kunifokea, maisha yakaendelea nilivyomaliza darasa la 7. Darasa zima tulifeli nikatamani niende nikasome private school, mama akaniambia hana uwezo wa kunilipia ada hapo akili ikanijia ya kutaka kumjua baba yangu nikamfuata mama na kumliza tena safari hii mama hakuwa mkali akanieleza baba yako anaitwa Erasto Bonda ni afisa mipango wilaya ya Kwimba, kumbuka tulikuwa tukiishi nje kidogo ya wilaya ya Magu. Dah mzuka wa kutaka kumjua ukinijia nikasema kimoyoyo lazima niende nikamuone aweze nisaidia niendelee na masomo, nikajichanga nikapata nauli nikafuata mama na kusudio langu la kwenda kumuona baba, mama akanikubalia siku ikafika nikapanda gari hadi Magu mijini halafu ndiyo nipande gari za kwenda Kwimba.

Nikiwa nasubiri gari lijaze abiria nikapata mwenyeji ambaye tulikuwa safari moja akaniuliza unaenda sehemu gani nikamueleza naenda kumtafuta mtu fulani, jamaa akaniambia anamfahamu sana hadi nyumbani kwake anapajua akaendelea kusema huyo lazima atakuwa baba yako maana mnafanana sana nikamjibu ni kweli ila sijawahi kumuona, basi safari ikaanza tulivyofika tukashuka na jamaa alinipeleka hadi nyumbani Mungu ambariki sana huyu mwamba maana alipoteza muda wake kuhakikisha nimefika.

Nilivyofika nilipokelewa na mama mwenye nyumba na kuniuliza mie ni nani na nipo hapo kwa ajili gani, nilijieleza ilikuwa usiku tayari nilipewa chakula nilivyomaliza kula nilionyeshwa chamba cha kulala ukweli nilikuwa na furaha sana kuona hatimaye nimefika kwa mzee japo sijaonana naye hadi muda huo kwani niliambiwa kuna sehemu alikuwa ameenda.

Dah asubuhi sana nilikuja kugongewa na kuambiwa nijiandae kwa safari, baba hata hakukata kunisemesha chochote nilimaliza kujiandaa akanichukua na kunipeleka kituoni Mzee njiani hakuniuliza chochote ikabidi nianze kujisemelesha mzee mie nimekuja kukutafuta, jamaa akanijibu hanikumbuki niliumia sana nikimtizama mzee tunafanana kinoma, nilifikishwa stand nikasafirishwa kurudi Magu, mpaka leo sina baba wala shangazi huwa nawatamani nami ningekuwa na ndugu hao ila ndiyo mzee alishasema hanikumbuki, wacha maisha yaendelee.
Je baba yako huyo alikuwa na mawasiliano na mama yako?
 
Huwa nikiona mada kama hizi nafsi inaingia unyonge Sana kuona watu hawaelewi wanachoambiwa .moja ya matatizo ya watu kuzalisha na kukimbia ndio haya watoto wanakosa ndugu watoto wanakosa upande mmoja wa familia.mtu unaishi kinyonge kabisa

Watoto wakiume wanatakiwa kuoa na sio kutia mimba na kukimbia

Sent from my MI MAX 2 using JamiiForums mobile app
Wewe ni ke au me mkuu, mabadiliko yanaanza na wewe mzee, utamu wa dakika 5 unakuja letea watu shida ya maisha yao yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah mungu hatakutupa ipo siku huyo mzee atakutafuta japo nafsi yake inamsuta
Nilivyopata akili nilitamani kumjua baba yangu mzazi hapo nikiwa darasa la 5, baada ya kuona marafiki zangu wote wapo na wazazi wao wawili.

Nikafuata mama na kumliza juu ya habari ya baba yangu, mama hakunipa jibu la kueleweka zaidi ya kunifokea, maisha yakaendelea nilivyomaliza darasa la 7. Darasa zima tulifeli nikatamani niende nikasome private school, mama akaniambia hana uwezo wa kunilipia ada hapo akili ikanijia ya kutaka kumjua baba yangu nikamfuata mama na kumliza tena safari hii mama hakuwa mkali akanieleza baba yako anaitwa Erasto Bonda ni afisa mipango wilaya ya Kwimba, kumbuka tulikuwa tukiishi nje kidogo ya wilaya ya Magu. Dah mzuka wa kutaka kumjua ukinijia nikasema kimoyoyo lazima niende nikamuone aweze nisaidia niendelee na masomo, nikajichanga nikapata nauli nikafuata mama na kusudio langu la kwenda kumuona baba, mama akanikubalia siku ikafika nikapanda gari hadi Magu mijini halafu ndiyo nipande gari za kwenda Kwimba.

Nikiwa nasubiri gari lijaze abiria nikapata mwenyeji ambaye tulikuwa safari moja akaniuliza unaenda sehemu gani nikamueleza naenda kumtafuta mtu fulani, jamaa akaniambia anamfahamu sana hadi nyumbani kwake anapajua akaendelea kusema huyo lazima atakuwa baba yako maana mnafanana sana nikamjibu ni kweli ila sijawahi kumuona, basi safari ikaanza tulivyofika tukashuka na jamaa alinipeleka hadi nyumbani Mungu ambariki sana huyu mwamba maana alipoteza muda wake kuhakikisha nimefika.

Nilivyofika nilipokelewa na mama mwenye nyumba na kuniuliza mie ni nani na nipo hapo kwa ajili gani, nilijieleza ilikuwa usiku tayari nilipewa chakula nilivyomaliza kula nilionyeshwa chamba cha kulala ukweli nilikuwa na furaha sana kuona hatimaye nimefika kwa mzee japo sijaonana naye hadi muda huo kwani niliambiwa kuna sehemu alikuwa ameenda.

Dah asubuhi sana nilikuja kugongewa na kuambiwa nijiandae kwa safari, baba hata hakukata kunisemesha chochote nilimaliza kujiandaa akanichukua na kunipeleka kituoni Mzee njiani hakuniuliza chochote ikabidi nianze kujisemelesha mzee mie nimekuja kukutafuta, jamaa akanijibu hanikumbuki niliumia sana nikimtizama mzee tunafanana kinoma, nilifikishwa stand nikasafirishwa kurudi Magu, mpaka leo sina baba wala shangazi huwa nawatamani nami ningekuwa na ndugu hao ila ndiyo mzee alishasema hanikumbuki, wacha maisha yaendelee.
 
Si kwa nia mbaya, lkn nadhani wewe ni kijana bado, mambo ya mizozano ya ndoa huyajui vizuri, sio kumwogopa mke bali kutotaka kuifanya Home kuwa Hell.
Kuna wanawake vichaa huku duniani ikifika kwenye issue ya mtoto wa nje! Tena awe mdogo kuliko wanae ,Yaani nyumbani panakuwa hell na shetani anapiga sarakasi kila ukirudi, nyumba inaharibika, hata upige vipi bado balaa liko palepale, watoto wanateseka, anampigia bosi wako simu anamtukana, anataka kuchoma moto gari ya kazini, nk nk mambo ni mengi
Kuna mfanya kazi mwenzangu mkurya,mke alikiwasha, jamaa akawa anaongea mwenyewe barabarani, analala baa, na kazi alipoteza. Simlaumu mzee kwa kufunika kombe aliepusha mengi. Lakini mtoa mada ana nafasi bado kama anataka kumwona mzee! Na vizuri akawa naye vizuri kabla mzee hajafariki. Wayaweke sawa. Malaana haya ya kukataliwa yanaishi vizazi na vizazi.
Ndugu yangu Ikombabhuki mimi nina miaka mingi ya ndoa rasmi ni mwaka wa 9 huu na nimeowa kwa kuchelewa . Mimi kwangu ndoa sio mkataba wa mpaka kufa. Pia mimi naoa sio kuolewa nasema hivyo nina uzoefu na mgogoro hiyo ila hata siku moja mke wangu hawezi kuwa juu yangu. Napenda democrasia ila ukiiendekeza sana inakuwa upuuzi. Sipendi kuwa na watoto wanje ila ilitokea mmoja kulingana na majukumu ya kazi na ukiwa mwanaume lijali makosa yapo nikapata mtoto nje ya ndoa. Akaleta za kuleta nikamwambia either atambae yeye au akubali full stop na yeye anajua msimamo yangu tokea uchumba kuwa sirudi nyuma kama treni ikitokea kurudi nyuma jua hiyo ni ajari mbaya. Mbona saivi yeye mwenye kutoka kwenye mshahara wake analipia ada za wote ikitokea nimechelewa kulipa. Nina kauli moja tu kuwa siwezi kumpenda mtu zaidi ninavyo jipenda mimi ko sinaoni shida zaidi hata nikimpoteza, nahisi principle imekuja baada kupitia mengi tena ya kuuzunisha. Watu ambao watanisumbua ni wazazi, ndugu wa kuzaliwa pamoja na watoto wangu hao nitatumia kuwapoteza hata ikitokea kuna ulazima na siwengine tunao kutana ukubwani.
 
Walokole mnachukuliaga matatizo ya watu simple sana. Halafu unakuta wewe mwenyewe hata soksi ya 200 ilikuwa inakushinda kununua unakimbilia kwa baba au mama. Ila mkionaga mtu anapitia hali ngumu na depression mnajifanya mnaijua sana dini.

Mungu ana kanuni zake na mzazi ana majukumu yake.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]jf bwana
 
Huyo aliekupeleka kwake nae alikuwa hajakusaidia kikamilifu yeye kama mtu mzima.

Alijua kabisa baba yako huyo ana mke na wewe umemwambia hujawahi kuonana na baba yako, hivi hakujiongeza kufaham kwamba wewe sie mtoto wa mke anaeishi nae na kwamba wake za watu wengi hawapemdi habari za watoto wa nje ya ndoa?

Ilibidi tu akupeleke hata karibu na ofisini kwake huko amwite wakati wewe upo kasehem flan hivi (wafanyalazi wenzake wasikuone huemda wakasafirisha maneno kwa mkewe), hapo hali ingekuwa na afadhali, na wala asingekupeleka nyumbani bali angekulipia hata hoteli ukae hapo siku 2 mjuane zaidi na hata kukupeleka kwa ndugu zako ujuane nao.

Kumbuka mtoto wa nje ya ndoa ni siri kama ilivyo kwa michepuko, ni hatari kuigonganisha na wake wa ndoa.

Pole sana lakini kosa lipo kwa aliekupeleka, Ila hata mama yako pia yeye kama mtu mzima ilibidi akupe kidogo muongozo kwamba ufanye juu chini uonane na baba yako yeye kama yeye anapokuwa peke yake, sio kupitia nyumbani kwake ambako ana mke.

Ulipoenda huko ni kwamba kwa ufupi tu ulikuwa umetia mchanga kwenye kitumbua, ndoa ya huyo baba yako ilikuwa hatarini, Ilibidi tu wewe uondoke, hakukuwa na namna hapo, ila labda tu kosa kubwa ni baba yako kuto kukutafuta baada ya hapo ila hatuwezi jua huendwa alipigwa biti zito mno angefanya hivyo.

Yote kwa yote ulienda kuzua kizaa zaa tu huko, ilibidi upewe muongozo ama kusaidiwa kukutana na huyo baba yako kwa usiri na ninakuhakikishia mambo yangekua yamenyooka.
Umesema yote kabisa Mama yake' anapaswa kulaumiwa katika Hilo kitendo cha kumuacha mtoto aende kumtafuta baba yake' ambaye hajawahi kuonana nae hata siku 1 na akamuacha mtoto ndio aendee mwenyewe kujieleza ilikuwa ni mistake Sana

Alipaswa kupanga siku ambayo angesafiri yeye pamoja na mtoto wake Kisha wangetafuta njia Bora ya kumtafuta Huyo Mzee sehemu nyingine tofauti na kazini kwake Jambo la kwanza wangetafuta marafiki wa karibu wa Huyo Mzee wangewaomba wawasaidie kuwa kutanisha na Huyo Mzee Kisha ndio wakutane nae lakini hiyo njia aliyoitumia Huyo kijana haikuwa njia rafiki Tena anabahati Sana wamama wengine jinsi walivyokuwa na roho mbaya angeweza hata kuzurika
 
Hakuna mwenye nafuu hata mmoja binadamu wote ni wakatili maana mi mwenyewe niliachwa hospitali.

Sijawahi kumjua baba wala Mama.

Nikisikia mtu anasema mama anauchungu na mwana natamani nimtukane tusi la nguoni.
Aisee [emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]

Hivi huwa wanazaa Watoto kwa sababu gani Kama hawapo tayari kuwalea !?
 
Labda maza alishamwambia babako we siyo mtoto wake maana wamama wengi pia huwa wanazingua sana ila kwakua mwanaume siku zote ni mbebeshwa lawama mwishoni bila kujulikana chanzo lazma jamii yote imuone mbaya tu.
Yeah alipaswa kufahamu habari kamili in details wajua katika maisha ya mahusiano Kuna watu wengine huwa wanapitishwa katika nyakati ngumu sana
 
Hakuna mwenye nafuu hata mmoja binadamu wote ni wakatili maana mi mwenyewe niliachwa hospitali.

Sijawahi kumjua baba wala Mama.

Nikisikia mtu anasema mama anauchungu na mwana natamani nimtukane tusi la nguoni.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23] kubaaabbaake

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nina kisa kama hicho mtanihurumia kwa uandishi wangu, Mimi Baba yangu aliondoka nyumbani nikiwa na miaka 5 tukiwa ndugu 7 wa tumbo moja na kwa mzee, huyu mzee aliondoka tu kwa mambo yake ya kibiashara na hakurudi nyumbani, nikiwa na miaka 8 hivi kama sikosei nikaenda kwa mzee, Mimi na dada yangu na shangazi, basi mzee akutupokea vizuri tu, na nikafurahi kweli, tulikaa kwa muda afu tukaondoka tukarudi kijijini, maisha yakaendelea na ukumbuke alikuwa na mwanamke mwingine na familia nyingine kabisa na watoto wa 4 wakubwa pia,

Sijui alikuwa na yule mwanamke wakati akiwa na mama sijui maana watoto wake mkubwa tulikuwa tunazidiana Mwaka tu,

Nilivyofika darasa la 4 mimi na dada yangu tukapanga Safari tukamuone mzee maana hakuwa na mawasiliano yeyote kabisa japo tulikuwa tunasikia kuwa ni mfanyabiashara mkubwa tu anapesa, sasa tukapanga Safari mimi na dada hao tukaingia muda wa jioni hivi tukaulizia bahati nzuri tumefanana nae mno wote wa2 haikuwa kazi ngumu kumpata, mtu wa kwanza tu kumuuliza alisema mnafanana sana flani basi tukapelekwa, kufika tukamkuta Mke wake alitukaribisha vizuri tu kusema kweli, mzee hakuwepo, mida ya saa 12 jioni mzee akarudi pale home, bila salamu alivyotuona aliuliza mmefata nini? tukamweleza baba tulikumiss basi mzee akajibu hayo mapenzi ya kunimiss kwa kilugha “ yangewaua tujue mmekufa kwa kunimiss, “ duu tumechoka tuna njaa tulijisikia vibaya sana dada angu alilia sana akaapa hatokuja kurudi tena kwa mzee

Basi tukakaa kama siku 2 3 sikumbuki ila hatukukaa tukarudi kijijini kila siku tukiwa pale baba alikuwa anatufokea Maneno makali sana

Tukarudi kijijini maisha yakaendelea, dada angu akasoma akahitimu Form 4, mimi nikaingia darasa la 7, hali mbaya nikafaulu nikakumbuka mzee wangu yupo japo tulikubaliana na dada tusimfuate mzee tena hadi tukiwa watu wazima kiufupi tulijihesabia hatuna baba wa kumtegemea kwa chochote, shida haina adabu mama hana hata sh 10 natakiwa kwenda shule , nikamwambia mama mimi narudi kwa mzee angalau nipate hata dawati na nguo Za shule ada tutajua mbele kwa mbele, nakumbuka mama akanikopea nauli 50000 huyo nikapanda basi nikafika kwa mzee, nikamkuta baba alivyoniona tu alikasirika balaa, akanifokea kuliko kipindi kile nipo na dada

Mzee alinisema Maneno yote mabaya sina kosa sina namna yeyote nilikuwa najisikia kama niko jehanaam maana muda wote akiniona ananisema vibaya na matusi juu, nashukuru Yule mama alikuwa ananionea huruma sana nimechakaa nimetoka kijijini imagine, sina hata nguo Za kuvaa, Baba alikuwa na nguo nyingi sana sana, yule mama akanipangia baadhi ya nguo Za mzee ili nikirudi kijijini nipunguze niwe navaa. Maana mzee alikuwa anagawia sana watu nguo,

Baada ya siku 3 Za mateso kukaa pale hatimae Baba akaniambia kesho utaondoka, sitosahau alikuja kulala na mimi kwenye chumba nilichokua nalala alinikagua nguo zote nikabaki sina hata moja na mama Mdogo alikuwa ameniwekea kwenye begi na saa moja hivi ya mzee weeeee nilitukanwa usiku mzima, hatimae asubh saa 11 nikapelekwa stand kurudi kijijini nakumbuka Mvua ilikuwa inanyesha sana mzee alinipeleka hivyo hivyo hakujali hata niondoke kesho yake,

Safari ilikuwa Nzuri tu lakini baadae gari ilipata ajali ikaanguka watu Wakaumia sana, nakumbuka niliona mtu jicho limechomoka lote,
Nikatoka salama, nikaapa sitorudi tena kwa mzee.
Maisha yakaendelea nikasoma nikahitimu, nikapata kazi na baada ya miaka mingi sana mzee maisha yalibadilika akakimbia ile familia pia, Ndugu zake wakanishauri ikabidi mzee arudishwe nyumbani kule kijijini baada ya kukaa nje kwa miaka 16
Hadi navyoongea alirudiana na mama na namtunza kama Baba yangu japo ni mkorofi mno
Hujafa hujaumbika Poleni nimewachosha kwa kuandika mambo marefu na nimefupisha story
Ulilisamehe la nini sasa[emoji57][emoji57]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom