G
guest-1787677467
Guest
Ushauri mzuri sana huu.Jipe moyo, baba yako ni MUNGU kama ulikataliwa na huyo wa duniani. Usikute mama yako anajua tatizo.
Ushauri mzuri sana huu.Jipe moyo, baba yako ni MUNGU kama ulikataliwa na huyo wa duniani. Usikute mama yako anajua tatizo.
Huyo baba mtu alichemka, mtoto kalala kwako wife Kesha muona hiyo kesi haishi, baba angemaliza na mkewe na maisha yange endelea.Huyo aliekupeleka kwake nae alikuwa hajakusaidia kikamilifu yeye kama mtu mzima.
Alijua kabisa baba yako huyo ana mke na wewe umemwambia hujawahi kuonana na baba yako, hivi hakujiongeza kufaham kwamba wewe sie mtoto wa mke anaeishi nae na kwamba wake za watu wengi hawapemdi habari za watoto wa nje ya ndoa?
Ilibidi tu akupeleke hata karibu na ofisini kwake huko amwite wakati wewe upo kasehem flan hivi (wafanyalazi wenzake wasikuone huemda wakasafirisha maneno kwa mkewe), hapo hali ingekuwa na afadhali, na wala asingekupeleka nyumbani bali angekulipia hata hoteli ukae hapo siku 2 mjuane zaidi na hata kukupeleka kwa ndugu zako ujuane nao.
Kumbuka mtoto wa nje ya ndoa ni siri kama ilivyo kwa michepuko, ni hatari kuigonganisha na wake wa ndoa.
Pole sana lakini kosa lipo kwa aliekupeleka, Ila hata mama yako pia yeye kama mtu mzima ilibidi akupe kidogo muongozo kwamba ufanye juu chini uonane na baba yako yeye kama yeye anapokuwa peke yake, sio kupitia nyumbani kwake ambako ana mke.
Ulipoenda huko ni kwamba kwa ufupi tu ulikuwa umetia mchanga kwenye kitumbua, ndoa ya huyo baba yako ilikuwa hatarini, Ilibidi tu wewe uondoke, hakukuwa na namna hapo, ila labda tu kosa kubwa ni baba yako kuto kukutafuta baada ya hapo ila hatuwezi jua huendwa alipigwa biti zito mno angefanya hivyo.
Yote kwa yote ulienda kuzua kizaa zaa tu huko, ilibidi upewe muongozo ama kusaidiwa kukutana na huyo baba yako kwa usiri na ninakuhakikishia mambo yangekua yamenyooka.
Mimi na kubali watoto ni utajir hasa hasa Kwa wasukuma...Mkuu mlaumu mama yako, mama yako ndiye mwenye makosa siku ukiwajua wanawake hutakaa umuone baba yako ni mbaya.
baba ni mwanaume na wewe ni mwanaume. Wanawake hawafai mwache baba ale maisha na umpende haijalishi kakufanyia nini . Kama unabisha mpende mama yako alafu mchukie baba yako siku ukija kuoa utakuja kulia machozi na hakuna wa kukusaidia
Swali kwako: katika pitapita zako za ujanani alafu ghafla ukaja kuoa, akija kijana aliemaliza darasa la saba takribani miaka 14 hata kama mmefanana hivi nakudai ni mwanao utakubali?
Mama yako ndio kiini kikuu cha hayo matatizo yako, hakuwa responsible na wewe kuhusiana na suala la baba yako tangu hatua za awali kabisa za malezi na makuzi yako.Nilivyopata akili nilitamani kumjua baba yangu mzazi hapo nikiwa darasa la 5, baada ya kuona marafiki zangu wote wapo na wazazi wao wawili.
Nikafuata mama na kumliza juu ya habari ya baba yangu, mama hakunipa jibu la kueleweka zaidi ya kunifokea, maisha yakaendelea nilivyomaliza darasa la 7. Darasa zima tulifeli nikatamani niende nikasome private school, mama akaniambia hana uwezo wa kunilipia ada hapo akili ikanijia ya kutaka kumjua baba yangu nikamfuata mama na kumliza tena safari hii mama hakuwa mkali akanieleza baba yako anaitwa Erasto Bonda ni afisa mipango wilaya ya Kwimba, kumbuka tulikuwa tukiishi nje kidogo ya wilaya ya Magu. Dah mzuka wa kutaka kumjua ukinijia nikasema kimoyoyo lazima niende nikamuone aweze nisaidia niendelee na masomo, nikajichanga nikapata nauli nikafuata mama na kusudio langu la kwenda kumuona baba, mama akanikubalia siku ikafika nikapanda gari hadi Magu mijini halafu ndiyo nipande gari za kwenda Kwimba.
Nikiwa nasubiri gari lijaze abiria nikapata mwenyeji ambaye tulikuwa safari moja akaniuliza unaenda sehemu gani nikamueleza naenda kumtafuta mtu fulani, jamaa akaniambia anamfahamu sana hadi nyumbani kwake anapajua akaendelea kusema huyo lazima atakuwa baba yako maana mnafanana sana nikamjibu ni kweli ila sijawahi kumuona, basi safari ikaanza tulivyofika tukashuka na jamaa alinipeleka hadi nyumbani Mungu ambariki sana huyu mwamba maana alipoteza muda wake kuhakikisha nimefika.
Nilivyofika nilipokelewa na mama mwenye nyumba na kuniuliza mie ni nani na nipo hapo kwa ajili gani, nilijieleza ilikuwa usiku tayari nilipewa chakula nilivyomaliza kula nilionyeshwa chamba cha kulala ukweli nilikuwa na furaha sana kuona hatimaye nimefika kwa mzee japo sijaonana naye hadi muda huo kwani niliambiwa kuna sehemu alikuwa ameenda.
Dah asubuhi sana nilikuja kugongewa na kuambiwa nijiandae kwa safari, baba hata hakukata kunisemesha chochote nilimaliza kujiandaa akanichukua na kunipeleka kituoni Mzee njiani hakuniuliza chochote ikabidi nianze kujisemelesha mzee mie nimekuja kukutafuta, jamaa akanijibu hanikumbuki niliumia sana nikimtizama mzee tunafanana kinoma, nilifikishwa stand nikasafirishwa kurudi Magu, mpaka leo sina baba wala shangazi huwa nawatamani nami ningekuwa na ndugu hao ila ndiyo mzee alishasema hanikumbuki, wacha maisha yaendelee.
Kiini cha tatizo hili ni huyo mwanamke mwenzako, wala siyo huyo baba yake mtoa hoja.Pole mkuu, ila wanaume mngekua na nyinyi mnabeba mimba na kuusikia uchungu mimi nahisi haya maswala yangekua yanapungua.