Baba yangu aliniambia hanikumbuki, niliumia sana

Ila shukuru sana Mama wakambo alikupokea vizuri ilo linatosha pambana uwe diamond wa baadae akishatumbuliwa huko atakutafuta tu usijali kaza moyo
Ya Diamond na baba yake yasihusishwe na story ya huyu dogo; baba yake Diamond ana historia ya kumkataa Diamond kweli? Mbona hadi shule na hospital alikua anampeleka?
 
Rudia kusoma vizuri ndio ucomment usikurupuke
 
Nilivyopata akili nilitamani kumjua baba yangu mzazi hapo nikiwa darasa la 5, baada ya kuona marafiki zangu wote wapo na wazazi wao wawili.

Nikafuata mama na kumliza juu ya habari ya baba yangu, mama hakunipa jibu la kueleweka zaidi ya kunifokea, maisha yakaendelea nilivyomaliza darasa la 7. Darasa zima tulifeli nikatamani niende nikasome private school, mama akaniambia hana uwezo wa kunilipia ada hapo akili ikanijia ya kutaka kumjua baba yangu nikamfuata mama na kumliza tena safari hii mama hakuwa mkali akanieleza baba yako anaitwa Erasto Bonda ni afisa mipango wilaya ya Kwimba, kumbuka tulikuwa tukiishi nje kidogo ya wilaya ya Magu. Dah mzuka wa kutaka kumjua ukinijia nikasema kimoyoyo lazima niende nikamuone aweze nisaidia niendelee na masomo, nikajichanga nikapata nauli nikafuata mama na kusudio langu la kwenda kumuona baba, mama akanikubalia siku ikafika nikapanda gari hadi Magu mijini halafu ndiyo nipande gari za kwenda Kwimba.

Nikiwa nasubiri gari lijaze abiria nikapata mwenyeji ambaye tulikuwa safari moja akaniuliza unaenda sehemu gani nikamueleza naenda kumtafuta mtu fulani, jamaa akaniambia anamfahamu sana hadi nyumbani kwake anapajua akaendelea kusema huyo lazima atakuwa baba yako maana mnafanana sana nikamjibu ni kweli ila sijawahi kumuona, basi safari ikaanza tulivyofika tukashuka na jamaa alinipeleka hadi nyumbani Mungu ambariki sana huyu mwamba maana alipoteza muda wake kuhakikisha nimefika.

Nilivyofika nilipokelewa na mama mwenye nyumba na kuniuliza mie ni nani na nipo hapo kwa ajili gani, nilijieleza ilikuwa usiku tayari nilipewa chakula nilivyomaliza kula nilionyeshwa chamba cha kulala ukweli nilikuwa na furaha sana kuona hatimaye nimefika kwa mzee japo sijaonana naye hadi muda huo kwani niliambiwa kuna sehemu alikuwa ameenda.

Dah asubuhi sana nilikuja kugongewa na kuambiwa nijiandae kwa safari, baba hata hakukata kunisemesha chochote nilimaliza kujiandaa akanichukua na kunipeleka kituoni Mzee njiani hakuniuliza chochote ikabidi nianze kujisemelesha mzee mie nimekuja kukutafuta, jamaa akanijibu hanikumbuki niliumia sana nikimtizama mzee tunafanana kinoma, nilifikishwa stand nikasafirishwa kurudi Magu, mpaka leo sina baba wala shangazi huwa nawatamani nami ningekuwa na ndugu hao ila ndiyo mzee alishasema hanikumbuki, wacha maisha yaendelee.

Daaaah pole sana mkuu. So Dr Melina Erasto Bonda wa Rungwe atakuwa ndugu yako
 
Pole mkuu kikubwa uzima ndugu watakutafuta tu ikifika wakati wake kipindi hicho nawe utakuwa huwahitaji
 
Baba yako dhaifu sana anakataa mtoto kwa ajiri ya make? Kuna jamaa yangu aliletewa mtoto gafla na mchepuko mke akagoma jibu alilotoa akwamwambia huyu mtoto kwao ni hapa wewe si una kwenu hadi Leo mtoto yupo pale

[emoji851][emoji851][emoji851]wanaume wa namna hii tumebaki wachache sana
 
Pole sana inaumiza mno ila jipe moyo, hebu funguka zaidi uliporudi nyumbani ilikuwaje? ulibahatika kuendelea na masomo?
 
Walokole mnachukuliaga matatizo ya watu simple sana. Halafu unakuta wewe mwenyewe hata soksi ya 200 ilikuwa inakushinda kununua unakimbilia kwa baba au mama. Ila mkionaga mtu anapitia hali ngumu na depression mnajifanya mnaijua sana dini.

Mungu ana kanuni zake na mzazi ana majukumu yake.
Bora umemwambia ukwel mkuu,wanaboa sana hawa
 
Mkuu mi naona ulikosea...labda ilikuwa ni akili za utoto lakini hukutakiwa kwenda nyumbani...na unajua kabisa ameoa na familia..haapo ni ngumu kukubali
 
Naomba uniwie radhi kwa hili ntakalo ongea kama ntakukwaza kwa namna moja ama nyingine.

Ipo hivi mwanaume hua hana haja ya kukataa mtoto ili kuimarisha ndoa yake ,

Kwakua wakewe hujua kabisa wame hua na makando kando daima ,

Sasa hapo mzee alipo kukataa , mama yako alipaswa akupe dondoo kidogo ya kukufungua akili

Haijarishi itakuumiza vipi , Ila kwa wakati huo ulipaswa kujua tu ,

Vitu ulivyo paswa kujua ni waliishije na waliachana vipi naamin hilo lingekuweka sawa,

Kwa wanaume wengi maneno huishi miaka mingi vifuani mwetu kuliko vitendo utakavyo tufanyia ,

Kwasasa ni kama huitaji ukaribu wala uwepo wa baba yako ,ila binafsi naona ni vyema kama yupo ukamtafuta na kuonananae kwa mara nyingine

Na akufahamishe akufahamu kwasababu zipi, huenda akawa sio na analijua hilo hivyo ukakosa nafasi ya kumjuza mzazi wako harisi. NIHAYAYO TU
 
Nilivyopata akili nilitamani kumjua baba yangu mzazi hapo nikiwa darasa la 5, baada ya kuona marafiki zangu wote wapo na wazazi wao wawili.

Nikafuata mama na kumliza juu ya habari ya baba yangu, mama hakunipa jibu la kueleweka zaidi ya kunifokea, maisha yakaendelea nilivyomaliza darasa la 7. Darasa zima tulifeli nikatamani niende nikasome private school, mama akaniambia hana uwezo wa kunilipia ada hapo akili ikanijia ya kutaka kumjua baba yangu nikamfuata mama na kumliza tena safari hii mama hakuwa mkali akanieleza baba yako anaitwa Erasto Bonda ni afisa mipango wilaya ya Kwimba, kumbuka tulikuwa tukiishi nje kidogo ya wilaya ya Magu. Dah mzuka wa kutaka kumjua ukinijia nikasema kimoyoyo lazima niende nikamuone aweze nisaidia niendelee na masomo, nikajichanga nikapata nauli nikafuata mama na kusudio langu la kwenda kumuona baba, mama akanikubalia siku ikafika nikapanda gari hadi Magu mijini halafu ndiyo nipande gari za kwenda Kwimba.

Nikiwa nasubiri gari lijaze abiria nikapata mwenyeji ambaye tulikuwa safari moja akaniuliza unaenda sehemu gani nikamueleza naenda kumtafuta mtu fulani, jamaa akaniambia anamfahamu sana hadi nyumbani kwake anapajua akaendelea kusema huyo lazima atakuwa baba yako maana mnafanana sana nikamjibu ni kweli ila sijawahi kumuona, basi safari ikaanza tulivyofika tukashuka na jamaa alinipeleka hadi nyumbani Mungu ambariki sana huyu mwamba maana alipoteza muda wake kuhakikisha nimefika.

Nilivyofika nilipokelewa na mama mwenye nyumba na kuniuliza mie ni nani na nipo hapo kwa ajili gani, nilijieleza ilikuwa usiku tayari nilipewa chakula nilivyomaliza kula nilionyeshwa chamba cha kulala ukweli nilikuwa na furaha sana kuona hatimaye nimefika kwa mzee japo sijaonana naye hadi muda huo kwani niliambiwa kuna sehemu alikuwa ameenda.

Dah asubuhi sana nilikuja kugongewa na kuambiwa nijiandae kwa safari, baba hata hakukata kunisemesha chochote nilimaliza kujiandaa akanichukua na kunipeleka kituoni Mzee njiani hakuniuliza chochote ikabidi nianze kujisemelesha mzee mie nimekuja kukutafuta, jamaa akanijibu hanikumbuki niliumia sana nikimtizama mzee tunafanana kinoma, nilifikishwa stand nikasafirishwa kurudi Magu, mpaka leo sina baba wala shangazi huwa nawatamani nami ningekuwa na ndugu hao ila ndiyo mzee alishasema hanikumbuki, wacha maisha yaendelee.
pengine akili za kitoto hukutakiwa kwenda nyumbani kwake bila nshaka ulimsababishia matatizo makubwa... mtaute babu au shangazi kwanza...
 
Ya Mungu mengi........ipo siku atakutafuta....KARMA
 
Mkuu nimesoma huu uzi umeniumiza sana! Mtu unakataa damu yako?
Hata hivyo aliyepaswa kwenda kukutambulisha ni Mama yako! Labda angemwona angeona aibu!
 
[emoji851][emoji851][emoji851]wanaume wa namna hii tumebaki wachache sana
Ana bahati alikutana na mwanamke mpole,
Mwingine ndoa ingevurugika, au hata hio ndoa sahizi usikute limebaki jina tu, huwez fanya hivyo na ndoa ikabaki salama kama mwanzo
 
Nilivyopata akili nilitamani kumjua baba yangu mzazi hapo nikiwa darasa la 5, baada ya kuona marafiki zangu wote wapo na wazazi wao wawili.

Nikafuata mama na kumliza juu ya habari ya baba yangu, mama hakunipa jibu la kueleweka zaidi ya kunifokea, maisha yakaendelea nilivyomaliza darasa la 7. Darasa zima tulifeli nikatamani niende nikasome private school, mama akaniambia hana uwezo wa kunilipia ada hapo akili ikanijia ya kutaka kumjua baba yangu nikamfuata mama na kumliza tena safari hii mama hakuwa mkali akanieleza baba yako anaitwa Erasto Bonda ni afisa mipango wilaya ya Kwimba, kumbuka tulikuwa tukiishi nje kidogo ya wilaya ya Magu. Dah mzuka wa kutaka kumjua ukinijia nikasema kimoyoyo lazima niende nikamuone aweze nisaidia niendelee na masomo, nikajichanga nikapata nauli nikafuata mama na kusudio langu la kwenda kumuona baba, mama akanikubalia siku ikafika nikapanda gari hadi Magu mijini halafu ndiyo nipande gari za kwenda Kwimba.

Nikiwa nasubiri gari lijaze abiria nikapata mwenyeji ambaye tulikuwa safari moja akaniuliza unaenda sehemu gani nikamueleza naenda kumtafuta mtu fulani, jamaa akaniambia anamfahamu sana hadi nyumbani kwake anapajua akaendelea kusema huyo lazima atakuwa baba yako maana mnafanana sana nikamjibu ni kweli ila sijawahi kumuona, basi safari ikaanza tulivyofika tukashuka na jamaa alinipeleka hadi nyumbani Mungu ambariki sana huyu mwamba maana alipoteza muda wake kuhakikisha nimefika.

Nilivyofika nilipokelewa na mama mwenye nyumba na kuniuliza mie ni nani na nipo hapo kwa ajili gani, nilijieleza ilikuwa usiku tayari nilipewa chakula nilivyomaliza kula nilionyeshwa chamba cha kulala ukweli nilikuwa na furaha sana kuona hatimaye nimefika kwa mzee japo sijaonana naye hadi muda huo kwani niliambiwa kuna sehemu alikuwa ameenda.

Dah asubuhi sana nilikuja kugongewa na kuambiwa nijiandae kwa safari, baba hata hakukata kunisemesha chochote nilimaliza kujiandaa akanichukua na kunipeleka kituoni Mzee njiani hakuniuliza chochote ikabidi nianze kujisemelesha mzee mie nimekuja kukutafuta, jamaa akanijibu hanikumbuki niliumia sana nikimtizama mzee tunafanana kinoma, nilifikishwa stand nikasafirishwa kurudi Magu, mpaka leo sina baba wala shangazi huwa nawatamani nami ningekuwa na ndugu hao ila ndiyo mzee alishasema hanikumbuki, wacha maisha yaendelee.
mlaumu sana mama yako. wewe pia ni mwanaume, ukikua utawajua wanawake. mama yako hata umpende vipi jua ni mwanamke tu, kuna mengi sana juu yake amekuficha. imagine, kama alificha mimba hakumwambia mdingi wako (mfano) afu mdingi anakuja kustukia anaambiwa na mkewe kuwa alizaa nje ya ndoa, unafikiri palitosha? na si ukute aliamini mamako ndio kakutuma umstukize ili aharibu ndoa yake yeye aje. kwanini hukumwambia mamako awasiliane na mdingi kwanza kabla ya wewe kuja? nikwambie, mimi nina watoto nje ya ndoa, mama zao walishawahi firigisa ndoa yangu hadi ndugu zangu walianza kufanya mipango ya kuwateminate wale watoto ili kuniondolea usumbufu, nikaja kujua ikabidi niwaponye watoto wangu. mama yako ni mtu mbaya, mlaumu huyo. babako hana shida, ana watoto wengine hata akikupoteza wewe hapungukiwi kitu na si ukute hakujua kama umezaliwa. na mshukuru sana mkewe hakukuwekea sumu.
 
Back
Top Bottom