Mimi nina kisa kama hicho mtanihurumia kwa uandishi wangu, Mimi Baba yangu aliondoka nyumbani nikiwa na miaka 5 tukiwa ndugu 7 wa tumbo moja na kwa mzee, huyu mzee aliondoka tu kwa mambo yake ya kibiashara na hakurudi nyumbani, nikiwa na miaka 8 hivi kama sikosei nikaenda kwa mzee, Mimi na dada yangu na shangazi, basi mzee akutupokea vizuri tu, na nikafurahi kweli, tulikaa kwa muda afu tukaondoka tukarudi kijijini, maisha yakaendelea na ukumbuke alikuwa na mwanamke mwingine na familia nyingine kabisa na watoto wa 4 wakubwa pia,
Sijui alikuwa na yule mwanamke wakati akiwa na mama sijui maana watoto wake mkubwa tulikuwa tunazidiana Mwaka tu,
Nilivyofika darasa la 4 mimi na dada yangu tukapanga Safari tukamuone mzee maana hakuwa na mawasiliano yeyote kabisa japo tulikuwa tunasikia kuwa ni mfanyabiashara mkubwa tu anapesa, sasa tukapanga Safari mimi na dada hao tukaingia muda wa jioni hivi tukaulizia bahati nzuri tumefanana nae mno wote wa2 haikuwa kazi ngumu kumpata, mtu wa kwanza tu kumuuliza alisema mnafanana sana flani basi tukapelekwa, kufika tukamkuta Mke wake alitukaribisha vizuri tu kusema kweli, mzee hakuwepo, mida ya saa 12 jioni mzee akarudi pale home, bila salamu alivyotuona aliuliza mmefata nini? tukamweleza baba tulikumiss basi mzee akajibu hayo mapenzi ya kunimiss kwa kilugha “ yangewaua tujue mmekufa kwa kunimiss, “ duu tumechoka tuna njaa tulijisikia vibaya sana dada angu alilia sana akaapa hatokuja kurudi tena kwa mzee
Basi tukakaa kama siku 2 3 sikumbuki ila hatukukaa tukarudi kijijini kila siku tukiwa pale baba alikuwa anatufokea Maneno makali sana
Tukarudi kijijini maisha yakaendelea, dada angu akasoma akahitimu Form 4, mimi nikaingia darasa la 7, hali mbaya nikafaulu nikakumbuka mzee wangu yupo japo tulikubaliana na dada tusimfuate mzee tena hadi tukiwa watu wazima kiufupi tulijihesabia hatuna baba wa kumtegemea kwa chochote, shida haina adabu mama hana hata sh 10 natakiwa kwenda shule , nikamwambia mama mimi narudi kwa mzee angalau nipate hata dawati na nguo Za shule ada tutajua mbele kwa mbele, nakumbuka mama akanikopea nauli 50000 huyo nikapanda basi nikafika kwa mzee, nikamkuta baba alivyoniona tu alikasirika balaa, akanifokea kuliko kipindi kile nipo na dada
Mzee alinisema Maneno yote mabaya sina kosa sina namna yeyote nilikuwa najisikia kama niko jehanaam maana muda wote akiniona ananisema vibaya na matusi juu, nashukuru Yule mama alikuwa ananionea huruma sana nimechakaa nimetoka kijijini imagine, sina hata nguo Za kuvaa, Baba alikuwa na nguo nyingi sana sana, yule mama akanipangia baadhi ya nguo Za mzee ili nikirudi kijijini nipunguze niwe navaa. Maana mzee alikuwa anagawia sana watu nguo,
Baada ya siku 3 Za mateso kukaa pale hatimae Baba akaniambia kesho utaondoka, sitosahau alikuja kulala na mimi kwenye chumba nilichokua nalala alinikagua nguo zote nikabaki sina hata moja na mama Mdogo alikuwa ameniwekea kwenye begi na saa moja hivi ya mzee weeeee nilitukanwa usiku mzima, hatimae asubh saa 11 nikapelekwa stand kurudi kijijini nakumbuka Mvua ilikuwa inanyesha sana mzee alinipeleka hivyo hivyo hakujali hata niondoke kesho yake,
Safari ilikuwa Nzuri tu lakini baadae gari ilipata ajali ikaanguka watu Wakaumia sana, nakumbuka niliona mtu jicho limechomoka lote,
Nikatoka salama, nikaapa sitorudi tena kwa mzee.
Maisha yakaendelea nikasoma nikahitimu, nikapata kazi na baada ya miaka mingi sana mzee maisha yalibadilika akakimbia ile familia pia, Ndugu zake wakanishauri ikabidi mzee arudishwe nyumbani kule kijijini baada ya kukaa nje kwa miaka 16
Hadi navyoongea alirudiana na mama na namtunza kama Baba yangu japo ni mkorofi mno
Hujafa hujaumbika Poleni nimewachosha kwa kuandika mambo marefu na nimefupisha story