sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,406
- 19,373
Huyo aliekupeleka kwake nae alikuwa hajakusaidia kikamilifu yeye kama mtu mzima.
Alijua kabisa baba yako huyo ana mke na wewe umemwambia hujawahi kuonana na baba yako, hivi hakujiongeza kufaham kwamba wewe sie mtoto wa mke anaeishi nae na kwamba wake za watu wengi hawapemdi habari za watoto wa nje ya ndoa?
Ilibidi tu akupeleke hata karibu na ofisini kwake huko amwite wakati wewe upo kasehem flan hivi (wafanyalazi wenzake wasikuone huemda wakasafirisha maneno kwa mkewe), hapo hali ingekuwa na afadhali, na wala asingekupeleka nyumbani bali angekulipia hata hoteli ukae hapo siku 2 mjuane zaidi na hata kukupeleka kwa ndugu zako ujuane nao.
Kumbuka mtoto wa nje ya ndoa ni siri kama ilivyo kwa michepuko, ni hatari kuigonganisha na wake wa ndoa.
Pole sana lakini kosa lipo kwa aliekupeleka, Ila hata mama yako pia yeye kama mtu mzima ilibidi akupe kidogo muongozo kwamba ufanye juu chini uonane na baba yako yeye kama yeye anapokuwa peke yake, sio kupitia nyumbani kwake ambako ana mke.
Ulipoenda huko ni kwamba kwa ufupi tu ulikuwa umetia mchanga kwenye kitumbua, ndoa ya huyo baba yako ilikuwa hatarini, Ilibidi tu wewe uondoke, hakukuwa na namna hapo, ila labda tu kosa kubwa ni baba yako kuto kukutafuta baada ya hapo ila hatuwezi jua huendwa alipigwa biti zito mno angefanya hivyo.
Yote kwa yote ulienda kuzua kizaa zaa tu huko, ilibidi upewe muongozo ama kusaidiwa kukutana na huyo baba yako kwa usiri na ninakuhakikishia mambo yangekua yamenyooka.