Ze_big_chill
Member
- Dec 15, 2016
- 16
- 161
Nilivyopata akili nilitamani kumjua baba yangu mzazi hapo nikiwa darasa la 5, baada ya kuona marafiki zangu wote wapo na wazazi wao wawili.
Nikafuata mama na kumliza juu ya habari ya baba yangu, mama hakunipa jibu la kueleweka zaidi ya kunifokea, maisha yakaendelea nilivyomaliza darasa la 7. Darasa zima tulifeli nikatamani niende nikasome private school, mama akaniambia hana uwezo wa kunilipia ada hapo akili ikanijia ya kutaka kumjua baba yangu nikamfuata mama na kumliza tena safari hii mama hakuwa mkali akanieleza baba yako anaitwa Erasto Bonda ni afisa mipango wilaya ya Kwimba, kumbuka tulikuwa tukiishi nje kidogo ya wilaya ya Magu. Dah mzuka wa kutaka kumjua ukinijia nikasema kimoyoyo lazima niende nikamuone aweze nisaidia niendelee na masomo, nikajichanga nikapata nauli nikafuata mama na kusudio langu la kwenda kumuona baba, mama akanikubalia siku ikafika nikapanda gari hadi Magu mijini halafu ndiyo nipande gari za kwenda Kwimba.
Nikiwa nasubiri gari lijaze abiria nikapata mwenyeji ambaye tulikuwa safari moja akaniuliza unaenda sehemu gani nikamueleza naenda kumtafuta mtu fulani, jamaa akaniambia anamfahamu sana hadi nyumbani kwake anapajua akaendelea kusema huyo lazima atakuwa baba yako maana mnafanana sana nikamjibu ni kweli ila sijawahi kumuona, basi safari ikaanza tulivyofika tukashuka na jamaa alinipeleka hadi nyumbani Mungu ambariki sana huyu mwamba maana alipoteza muda wake kuhakikisha nimefika.
Nilivyofika nilipokelewa na mama mwenye nyumba na kuniuliza mie ni nani na nipo hapo kwa ajili gani, nilijieleza ilikuwa usiku tayari nilipewa chakula nilivyomaliza kula nilionyeshwa chamba cha kulala ukweli nilikuwa na furaha sana kuona hatimaye nimefika kwa mzee japo sijaonana naye hadi muda huo kwani niliambiwa kuna sehemu alikuwa ameenda.
Dah asubuhi sana nilikuja kugongewa na kuambiwa nijiandae kwa safari, baba hata hakukata kunisemesha chochote nilimaliza kujiandaa akanichukua na kunipeleka kituoni Mzee njiani hakuniuliza chochote ikabidi nianze kujisemelesha mzee mie nimekuja kukutafuta, jamaa akanijibu hanikumbuki niliumia sana nikimtizama mzee tunafanana kinoma, nilifikishwa stand nikasafirishwa kurudi Magu, mpaka leo sina baba wala shangazi huwa nawatamani nami ningekuwa na ndugu hao ila ndiyo mzee alishasema hanikumbuki, wacha maisha yaendelee.