Baba yangu aliniambia hanikumbuki, niliumia sana

Baba yangu aliniambia hanikumbuki, niliumia sana

Ni kweli Mungu ndiyo baba yangu, hata sijui mama alimkosea nini nakumbuka hata rafiki wa mzee alikuwa akipita home na kutusalimia.
Huyo baba alikuwa anatambua uwepo wako? Alikuwa na mawasiliano na mama yako? Alijua mama yako amebeba mimba yake? Alijua wakati alipozaa? Alikuhudumia ulipokuwa mdogo? Kwa kifupi naona wewe ulikosea namna ya kujitambulisha. Hata kama awe baba yako huwezi kumzukia namna hiyo ghafla. Kuna process ulitakiwa uchukuwe kabla ya kuonana. Ungeweza kuwasiliana naye kwanza na baadae mkapanga muonane namna gani. Vinginevyo uniambie alikuwa anatambua tangu ulipozaliwa na alikuwa anafanya mawasialiano na mama yako.
 
Huyo baba alikuwa anatambua uwepo wako? Alikuwa na mawasiliano na mama yako? Alijua mama yako amebeba mimba yake? Alijua wakati alipozaa? Alikuhudumia ulipokuwa mdogo? Kwa kifupi naona wewe ulikosea namna ya kujitambulisha. Hata kama awe baba yako huwezi kumzukia namna hiyo ghafla. Kuna process ulitakiwa uchukuwe kabla ya kuonana. Ungeweza kuwasiliana naye kwanza na baadae mkapanga muonane namna gani. Vinginevyo uniambie alikuwa anatambua tangu ulipozaliwa na alikuwa anafanya mawasialiano na mama yako.
Mkuu rudia tena kusoma bandiko langu,kuna maswali hutaniuliza
 
Mkuu rudia tena kusoma bandiko langu,kuna maswali hutaniuliza
Nimerudia lakini sijaona jibu hata moja kwani hujaelezea. Labda wewe urudie kusoma maswali yangu ili ujibu. Maswali niliyouliza ni ya msingi sana kuweza kukisia ni kwa nini huyo baba alikurudisha.
 
mimi huwa sioni haja ya kuficha mtoto wa nje sijui wengine wanafeli wapi
Nina babamkubwa nunda, hakuwa anajali kama alipitia mwanamke huko akija kusema huyu mtoto ni wa babamkubwa, mtoto akiacha ziwa umri wa shule, wanapelekwa wanaelewa nyumbani kwake!
Alikuwa na mashamba na mifugo, hakukuwa na njaa nyumbani kwake. Na alikuwa muajiriwa serikalini.
Cha ajabu waliowin life ni watoto wa mke wa ndoa, wengine walichezea ile position, walikuwa wanatiwa ujinga na mama zao, wapambane na mke wa babamkubwa. R.I.P

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Huwa nikiona mada kama hizi nafsi inaingia unyonge Sana kuona watu hawaelewi wanachoambiwa .moja ya matatizo ya watu kuzalisha na kukimbia ndio haya watoto wanakosa ndugu watoto wanakosa upande mmoja wa familia.mtu unaishi kinyonge kabisa

Watoto wakiume wanatakiwa kuoa na sio kutia mimba na kukimbia

Sent from my MI MAX 2 using JamiiForums mobile app
 
Alikuruka kulinda ndoa yake, ungekuwa umemfuata kazini mchana, angekupokea ila asingekupeleka kwa mkewe, mngemalizana kiume na nduguzo ungewajua, lakini bado una nafasi. Mfuate tena ila pitia kwa rafiki yake wa karibu, usiende direct.
Huyo mzee alikua mpumbavu,kamzaa kwa uzinzi wake jukumu la kumlea ni lake...unamkataa mtoto kisa ndoa
 
Hayo ni makosa yake , angekuwa anamjali alivyotoka naye angejua namna ya kumsaidia.. hakuna haja ya kumtetea kuhalalisha dhambi zake .
 
Daaa Ila kuna watu wanapia maisha ya Hatare sana


Umenikumbuka story ya kijana mmoja tukiwa boarding school pio kibaigwa siku moja tukiwa kama kikundi watu kadhaa na simu za magendo dogo mmoja akasema ampigie baba yake simu aombe hela


Kapiga simu ikaita


"Haloo baba shikamoo mi flan baba akajibu flani ndo nan jamaa mwanao baba baba akavuta pozi kwa sekunde za ukimya baday aaaaaaah OK hujambo? Sema


Dogo alikata simu kwa akili za utoro wakucheka wakacheka Ila mshkaji alikuwa mpole wiki nzima
 
Walokole mnachukuliaga matatizo ya watu simple sana. Halafu unakuta wewe mwenyewe hata soksi ya 200 ilikuwa inakushinda kununua unakimbilia kwa baba au mama. Ila mkionaga mtu anapitia hali ngumu na depression mnajifanya mnaijua sana dini.

Mungu ana kanuni zake na mzazi ana majukumu yake.
Walokole tena!?
 
Haya maisha noma,

Kuna dogo mmoja alikuwa anaishi Mwanza- Mwananchi( Buzuruga kwa juu), dogo alikuwa anatubana "kete" sasa dogo alikuwa anaishi na mama ake mzazi na baba ake wa kambo, ilikuwa familia fulani hivi unorganised, sababu dingi ake na maza ake walikuwa walevi sana ila walikuwa na upendo sana kwa masela tuliokuwa tunaenda kula "puya" pale, dogo aliniambia maza ake ni mtu wa Kigoma ila dingi ake ni Msukuma wa pale pale town....

Baada ya miaka kadhaa kupita nikaja kuonana na dogo stendi ya Hiace hapo town (Kemondo) kabeba furushi la makopo (plastic scraps), nikamuuliza dogo kulikoni??? Akaanza kunipa stori,

Dogo anasema mama ake alianza kuugua akamuuguza mpaka akafa, baada ya kifo cha mama ake mtiti ndo ukaanza, maana watoto wa yule (mzee) baba ake wa kambo walimkataa, wakamwambia hawamtambui, hivyo msiba ukiisha atafute pa kwenda, na mbaya zaidi dogo akasema hamfahamu ndugu ya mama ake hata mmoja, na hata huko Kigoma kwa bibi ake hakuwahi kwenda hata siku moja, kiufupi hakuwa na connection yoyote na ndugu yeyote maana hata mama kwa bahati mbaya hakuzaa na yule baba ake wa kambo, na mama ake dogo hakuwahi kumwambia baba ake mzazi yuko wapi na anaitwa nani..., dogo akaniambia alivyofurushwa kule Buzuruga hakupata hata chochote ndo akaingia mtaani kupambana, na ishu nyingine dogo hukumaliza hata darasa la saba kielimu,

Nilijisikia uchungu sana dogo alivonipa ule mkasa, pamoja na kwamba hata mimi nilikuwa na kamsoto fulani, lakini nilijiona nina nafuu kubwa sana kuliko yule dogo

Jamani kuna watu wana maisha magumu..
 

Jamani tusilaumiane bila sababu
 
Hawakua na upendo tu hao ni washenzi,tunasaidia watu baki mitaani leo mtu ambaye anaishi nyumbani?huyo mzee nae ni mshenzi tu maana kama aliishi na mama wa huyo dogo angemkingia kifua au hata angemuanzishia kabiashara kokote akamkodia hata na chumba cha bei ndogo hapo mabatini au Igogo poa tu akashindwe mwenyewe

Hao walikua ni washenzi tu
 
Usijali mkuu hata Jack Ma alikuwa hakumbukwi wewe saka pesa ukizipata utakumbukwa tuu
 
Nilivyopata akili nilitamani kumjua baba yangu mzazi hapo nikiwa darasa la 5, baada ya kuona marafiki zangu wote wapo na wazazi wao wawili.

Nikafuata mama na kumliza juu ya habari ya baba yangu, mama hakunipa jibu la kueleweka zaidi ya kunifokea, maisha yakaendelea nilivyomaliza darasa la 7. Darasa zima tulifeli nikatamani niende nikasome private school, mama akaniambia hana uwezo wa kunilipia ada hapo akili ikanijia ya kutaka kumjua baba yangu nikamfuata mama na kumliza tena safari hii mama hakuwa mkali akanieleza baba yako anaitwa Erasto Bonda ni afisa mipango wilaya ya Kwimba, kumbuka tulikuwa tukiishi nje kidogo ya wilaya ya Magu. Dah mzuka wa kutaka kumjua ukinijia nikasema kimoyoyo lazima niende nikamuone aweze nisaidia niendelee na masomo, nikajichanga nikapata nauli nikafuata mama na kusudio langu la kwenda kumuona baba, mama akanikubalia siku ikafika nikapanda gari hadi Magu mijini halafu ndiyo nipande gari za kwenda Kwimba.

Nikiwa nasubiri gari lijaze abiria nikapata mwenyeji ambaye tulikuwa safari moja akaniuliza unaenda sehemu gani nikamueleza naenda kumtafuta mtu fulani, jamaa akaniambia anamfahamu sana hadi nyumbani kwake anapajua akaendelea kusema huyo lazima atakuwa baba yako maana mnafanana sana nikamjibu ni kweli ila sijawahi kumuona, basi safari ikaanza tulivyofika tukashuka na jamaa alinipeleka hadi nyumbani Mungu ambariki sana huyu mwamba maana alipoteza muda wake kuhakikisha nimefika.

Nilivyofika nilipokelewa na mama mwenye nyumba na kuniuliza mie ni nani na nipo hapo kwa ajili gani, nilijieleza ilikuwa usiku tayari nilipewa chakula nilivyomaliza kula nilionyeshwa chamba cha kulala ukweli nilikuwa na furaha sana kuona hatimaye nimefika kwa mzee japo sijaonana naye hadi muda huo kwani niliambiwa kuna sehemu alikuwa ameenda.

Dah asubuhi sana nilikuja kugongewa na kuambiwa nijiandae kwa safari, baba hata hakukata kunisemesha chochote nilimaliza kujiandaa akanichukua na kunipeleka kituoni Mzee njiani hakuniuliza chochote ikabidi nianze kujisemelesha mzee mie nimekuja kukutafuta, jamaa akanijibu hanikumbuki niliumia sana nikimtizama mzee tunafanana kinoma, nilifikishwa stand nikasafirishwa kurudi Magu, mpaka leo sina baba wala shangazi huwa nawatamani nami ningekuwa na ndugu hao ila ndiyo mzee alishasema hanikumbuki, wacha maisha yaendelee.
Huyo aliyekupeleka nyumbani ndo hana akili,serious unaweza mkuta mtoto njiani akwambie mwanangu nawe unakuja tumkabidhi mke wangu??

Sent from my CPH1909 using JamiiForums mobile app
 
Kufupisha tena bila kuficha baba ni mpumbavu sasa yaani anamtosa mtoto wake kisa kuogopa mke. Sisi wanaume wa Afrika huwa tunaoa sio kuolewa.

Huenda kuna sababu nyingine iliyo mfanya huyo mzee amkatae mtoto ambayo ni kubwa kuliko ya kumuogopa mke wa sasa.

Ninampa pole tu kijana kwa yalio mtokea tena wakati wa kipindi anahitaji msaada.
Si kwa nia mbaya, lkn nadhani wewe ni kijana bado, mambo ya mizozano ya ndoa huyajui vizuri, sio kumwogopa mke bali kutotaka kuifanya Home kuwa Hell.
Kuna wanawake vichaa huku duniani ikifika kwenye issue ya mtoto wa nje! Tena awe mdogo kuliko wanae ,Yaani nyumbani panakuwa hell na shetani anapiga sarakasi kila ukirudi, nyumba inaharibika, hata upige vipi bado balaa liko palepale, watoto wanateseka, anampigia bosi wako simu anamtukana, anataka kuchoma moto gari ya kazini, nk nk mambo ni mengi
Kuna mfanya kazi mwenzangu mkurya,mke alikiwasha, jamaa akawa anaongea mwenyewe barabarani, analala baa, na kazi alipoteza. Simlaumu mzee kwa kufunika kombe aliepusha mengi. Lakini mtoa mada ana nafasi bado kama anataka kumwona mzee! Na vizuri akawa naye vizuri kabla mzee hajafariki. Wayaweke sawa. Malaana haya ya kukataliwa yanaishi vizazi na vizazi.
 
Back
Top Bottom