SONDR
JF-Expert Member
- Apr 18, 2019
- 271
- 643
Wanajamvi habari za muda huu, poleni na majukumu ya kutafuta ridhiki. Niende kwenye mada moja kwa moja.
Nimepangisha fremu kwenye NYUMBA moja mjini kwa lengo la kufungua biashara ya pombe Kali yaani liquor store.
Nikaingia mkataba na mwenye nyumba wa miezi kumi wakati huo yeye hajui nataka kufanya biashara gani. Nikanza maandalizi ya kufungua biashara yangu Jana nikaleta mzigo wa pombe Kali ambazo nimefungasha kutoka jijini Dar es salaam.
Baada ya kumaliza kushusha na kuingiza mzigo wangu kwenye fremu yangu nikaondoka nikarudi nyumbani kwangu nikisubiri mzigo mwengine ufike ili niaze kufanya biashara mnamo tarehe moja January 2024.
Cha kushangaza asubuhi ya leo Kama saa kumi na mbili na nusu napokea simu ya baba mwenye nyumba akisema amekaa na familiya na wamekubaliana hawaruhusu biashara ya pombe kwenye nyumba yao nilichoka na kukosa cha kumjibu.
Nikamhoji mbona hukuliweka Hilo kwenye mkataba na kwanini hukusema wakati na kodisha akasema Mimi sikumuambia nataka nifanye biashara gani. Nikamueleza wazo la biashara nilangu ww umekodisha fremu ili Mimi nifanye biashara halali ambayo haivunji Sheria za nchi.
Kama unaitikadi zako kuhusu biashara flani ilikupasa uweke kwenye mkataba ili mimi nikisoma naelewa kwakua siwezi kujua itikadi yako Kama hujasema au kuweka wazi.
Wakuu nachanganyikiwa sielewi nimeshatumia pesa ya kutosha alafu mwenye nyumba anakuja na hoja Kama hii naombeni ushauri wenu wakuu.