Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Mahali inategemeana na kichwa cha mwanamke husika!! Tuseme mwanamke ameenda shule na akaelewa alichofundishwa! Mwanamke yupo au anaweza kuwa very productive akiwezeshwa! Kama hana ajira kisha ukampa 5M ajiajiri, basi baada ya mwaka hiyo itakuwa 5M x5! Mwanamke mwenye sifa hizo thamani ya mahari yake ni halali hata ikizidi hiyo 5M kwa sababu itakuwa compensated kupitia shughuli zenu za kimaendeleo!

Lakini kama mwanamke mwenyewe ni wale wanaoshinda kujiremba na kupiga umbeya, ukimpa mtaji anauua kwa kuhonga na kujinunulia vitu vizuri, na hakuna cha maana anachoringia zaidi ya uzuri wake, na wale mapoyoyo wakiwa wanaringia makalio yao, basi mwanamke kama huyo hata laki 3 kama mahari ni nyingi mnooooooooooooo!!!

Je, huyo mchumba wako anasimama kwenye mfano wa 1 au wa 2 ?!
 
Kuoa si lazima bob!
Na siku zote mahali huwa haiishi mpk uzeeni
 
Huyu kijana Mang'aa yeye na mshenga wake wameshindwa kuelewa mila za kichaga. Mimi mchaga pure nilioa mchaga mwenzangu nikalipa mahari laki 8.

Hayo makorokoro mengine yanayofika milioni kadhaa utaratibu unalipa mdogo mdogo mpaka uzeeni.

Mzee wangu mpaka sasa hajamaliza mahari huwa tunaamini mahari ni jambo endelevu.

Hiyo laki 8 ni vile vitu muhimu vya kununua kimila.
Vitu kma hv inabd muwaambie wageni utaratibu unakuaje

Mi naona hta familia nayo imetka kutembelea upepo kma jamaa angetoa yote
 
Ongea na mkeo kuwa hiyo mahari huiwezi atafikisha ujumbe na mjumbe hauwawi. Kama wakikomaa chukua mke kaa nae, hamna familia inayokubali kulea binti yao na mtoto wake wakati baba yake upo watakupa hata bure
 
Hiyo usd 3000 ni kwa watu gani mahari hulipwa kwa usd??
 
Mi nilitajiwa mahari + makorokoro m6 nilishaachana nae maana nilimwambia sina pesa hizo, halafu wachaga bana wanawake wenyewe ufundi 0% tuoe zile flat zao au nini?
 
mtu akapewa fursa ya kutupangia package ya mahari ili mpango mzima ukamilike.... list ya makorokoro kibao, Mara mkaja wa mama, Bibi, mablanket ya Mama na mashangazi, mbege mapipa matatu, mbuzi 3 wa maziwa na....mwishoni akataja cash money 3 Mil
nimecheka kweli
 
Niliporudi lodge usiku mzima sikulala , series nzima ikawa inaji frash back repetitively
 
Bado kidogo nikushauri uongee na huyo mama watoto kuhusu hio mil 5 ili awashawishi wazazi wakupunguzie..
ila kila nikiikumbuka laki mbili na themanini ya chakula uliyolipishwa naskia uchungu Chief..

tupa kule hio familia takataka.
Duuuuuhhhhhh,mwanangu mshenga wako alikuwa domo zege?
 
Ukiachana na Mahari kuwa 5M plus haijadiliki

Kitendo cha wewe kulipia Gharama za wao kuandaa sherehe hii mpya...

Sitaki kuwahukumu wachaga wote ila kama ndio utaratibu wenu ndugu zangu thats too much!!

5M hiyo unatoa kwa familia ya Mkeo mtarajiwa kama mahari hizi ni gharama ambazo lazma utazilipa kama Bwana Harusi
--- Gauni la Harusi plus Saloon Nafikri
--- Pete za ndoa
--- Suti ya Bwana Harusi
--- Gharama ya Ukumbi
--- Gharama za Kikao cha kwanza
--- Gharama za Usafiri kwenda kulipa 5M
Plus mambo mengne madogo madogo
Mkuu bora umesepa Kibingwa ila mwambie Afisa Ustawi wa Jamii kwamba gharama zimekua kubwa u cant afford ili ajue ukwel.
Vjana wengi hivi leo hawaoi kwa sababu ya kukutana na kujazana ujinga kwenye vjiwe!
 
Tumia njia mbadala. Wakwe mashangazi hadi huyo mjomba wa mahari watakupigia magoti kukubembeleza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom