Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Mdoa mada na Mimi yalishanikuta kama yako ila Mimi sio kwa mchaga,nilitajiwa kwa USD 3000,sawa na milioni 6 na laki 6,nimewapa tu zawadi ya mjukuu na nikajiongezea mihula miwili ya kwenye kiti cha ubaharia!
Sheria yangu niliyojiwekea mahari hata niambiwe Trilioni moja sitatoa zaidi ya laki 5 na itolewe na VAT kabisa hapo sitaki kukwepa kodi,na risiti nipewe ili ikitokea dharura mahakama wajue pa kuanzia
 
Leo week ya pili nimeshindwa kabisa kupokea simu ya Baba mkwe na Mshenga wangu.

Iko hivi katika misoto yangu na kukulu kakala za maisha atimae nikajikuta nimedondokea kwa mtoto wa kichaga Kama ilivyo janga kwa wanaume wengi wa mjini.

Mipango ikapangwa na siku ya kufika ukweni kupeleka posa ikafika. Kidume nikajikoki na Mshenga wangu na wadada 3 wa kukodi tukazuka ukweni.

Mambo yalikua shwari hadi pale mjomba mtu akapewa fursa ya kutupangia package ya mahari ili mpango mzima ukamilike.... list ya makorokoro kibao, Mara mkaja wa mama, Bibi, mablanket ya Mama na mashangazi, mbege mapipa matatu, mbuzi 3 wa maziwa na....mwishoni akataja cash money 3 Mil.


Mimi kipindi anataja yale mazaga hata nilikua sifuatilia ,akili yote ilikua inasubiri point ya msingi Cash money.

Badae ikatolewa option ya ku convert the overall cost ika amount Kama 5 Mil. na ushee!

Jitihada za mshenga kupangua bei hazikuzaa matunda. Mbaya zaidi ile tumemaliza events shangazi anatuzuia hakuna kuondoka mpaka tumelipia gharama za maandalizi walioyotufanyia.

Kwa shingo upande nikausukuma mzigo wa M pesa tsh 280, 000 coz walidai laki 3.


Niliporudi lodge usiku mzima sikulala , series nzima ikawa inaji frash back repetitively.

Nika najiuliza kwani wananiuzia mke kisa ni afisa ustawi wa jamii?

Ana kipi Cha ziada ambacho wake wa ndg zangu wameolewa na jumla ya mahari tulizotoa na makokoro yote hata milioni haikufika?

Kwani ana kismat Cha mafanikio? Mbona tangu tuingie kwenye relationship mambo mengi tunakimbizana kwa had-hoc za kufa mtu?

Na mengine mengi ambayo si busara kuyaanika humu.

Alifajiri nikaamua kufanya maamuzi magumu ..."Katu sitorudi tena ukweni." Kwa maana kuwa sitoi tena mahari, mtoto wao nimeshamtia mimba ,wakimtaka waje wamchukue.


Ni hayo tu.....sirudi ukweni tena

Mashemeji zangu wachaga povu ruksa. Ila katu sirudi tena ukweni.
Pole sana Mkuu
Nakumbuka nilipotaka kujua mahari ni kiasi gani
Mahari ni zawadi ya Bi harusi hivyo nilitakiwa kumuuliza mhusika mwenyewe.
Akanitajia Mahari haifiki hata 100k
Nikamuuliza Mara ya pili hii ndio mahari yako?
Akajibu vipi una pesa nyingi nikutajie mzigo mkubwa
Aaah hapana Mamiloo. Basi nikabeba Toto biiiichiii kwa elfu 90+

Hii utaikuta tu katika familia yenye kushikamana na dini
 
USILOLIJUA NI USIKU WA GIZA. Kulipa mahari yote kwa wachaga ni dharau. Hiyo 5m waliyokutajia wanajua kabisa wewe huwezi kuilipa. Pia hata hiyo ya chakula uliyotoa ungesema hauna siku ingepita. Kwa ushauri wangu kama huyo mwanamke unampenda kubali deni lipa unapoweza utapata baraka za wazazi na uende na wazazi wako usiende kihuni. Kulipa mahali inakua kama umemnunua ila ukishindwa kulipa yote sio kosa na inawapa wakwe nguvu angalau ukileta zako utafikiria hata mahari hujamaliza.
Mwisho kama ukitaka kuo uchagani ukitajiwa mahari ni elfu 50. Usije ukalipa yote hapohapo watakuona kiburi. Kubali utailipa kidogokidogo ila usikimbie
 
Biashara ya utumwa bado ipo kimtindo. Haijalishi utalipa kidogo kidogo mpaka uzeeni bado amount ni ile ile, 5ml, unanunua kitega uchumi? Na hiyo kurudisha garama 280k duh hapo noma.
 
Huyu kijana Mang'aa yeye na mshenga wake wameshindwa kuelewa mila za kichaga. Mimi mchaga pure nilioa mchaga mwenzangu nikalipa mahari laki 8.

Hayo makorokoro mengine yanayofika milioni kadhaa utaratibu unalipa mdogo mdogo mpaka uzeeni.

Mzee wangu mpaka sasa hajamaliza mahari huwa tunaamini mahari ni jambo endelevu.

Hiyo laki 8 ni vile vitu muhimu vya kununua kimila.
Ya nini kujisumbua na madeni wakati iko mikoa unapata mke hata kwa aya moja tu kwenye quran
 
Dah poa braza tunaheshimu maamuzi yako, usirudi tu ukweni, sio sababu ya mahari kubwa ila kuombwa kurudisha gharama ya tafrija ile sio sawa kabisa maana we hukuwaambia waandae tafrija ila ni wao kama wao
Sure hapa hawajamtendea haki mwana.Wamezingua kwa kifupi.Mm nisingerudisha maana akil yangu naijua mwenyewe jinsi ilivyo faster kufanya michanganuo na kuchukua maamuzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom