Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Huyu nilienae baba familia yake naskia ni wapenda hela balaa, hapa nilipo nishamtia mimba ya pili mpaka siku nikienda kwao kutaka kuoa nadhani watanipa hela mimi
Ahahahahahahahahhahah..
Mkuu nenda kwasikilize acha kusikilia ya watu.
Ww nan kakwambia wanapenda hela kwao??
Ahahah.
Vijana mna kazi sana.Nawawaza sana mabinti zangu wawil hawa itakuaje hiyo 20+ years to come
 
Huyu kijana Mang'aa yeye na mshenga wake wameshindwa kuelewa mila za kichaga. Mimi mchaga pure nilioa mchaga mwenzangu nikalipa mahari laki 8.

Hayo makorokoro mengine yanayofika milioni kadhaa utaratibu unalipa mdogo mdogo mpaka uzeeni.

Mzee wangu mpaka sasa hajamaliza mahari huwa tunaamini mahari ni jambo endelevu.

Hiyo laki 8 ni vile vitu muhimu vya kununua kimila.
Same here..mzee mpaka leo hajamaliza mahari ya bi mkubwa
 
Mi nimekuonea huruma hiyo gharama ya sherehe uliyoilipia.
Lakini mkuu ulikosea Sana.
Ilitakiwa uwape 10 aafu unawaambia nyingine unaenda kutafuta utaleta.
Hiyo ingewapa picha na mahari itakuwaje.!!
 
Leo week ya pili nimeshindwa kabisa kupokea simu ya Baba mkwe na Mshenga wangu.

Iko hivi katika misoto yangu na kukulu kakala za maisha atimae nikajikuta nimedondokea kwa mtoto wa kichaga Kama ilivyo janga kwa wanaume wengi wa mjini.

Mipango ikapangwa na siku ya kufika ukweni kupeleka posa ikafika. Kidume nikajikoki na Mshenga wangu na wadada 3 wa kukodi tukazuka ukweni.

Mambo yalikua shwari hadi pale mjomba mtu akapewa fursa ya kutupangia package ya mahari ili mpango mzima ukamilike.... list ya makorokoro kibao, Mara mkaja wa mama, Bibi, mablanket ya Mama na mashangazi, mbege mapipa matatu, mbuzi 3 wa maziwa na....mwishoni akataja cash money 3 Mil.


Mimi kipindi anataja yale mazaga hata nilikua sifuatilia ,akili yote ilikua inasubiri point ya msingi Cash money.

Badae ikatolewa option ya ku convert the overall cost ika amount Kama 5 Mil. na ushee!

Jitihada za mshenga kupangua bei hazikuzaa matunda. Mbaya zaidi ile tumemaliza events shangazi anatuzuia hakuna kuondoka mpaka tumelipia gharama za maandalizi walioyotufanyia.

Kwa shingo upande nikausukuma mzigo wa M pesa tsh 280, 000 coz walidai laki 3.


Niliporudi lodge usiku mzima sikulala , series nzima ikawa inaji frash back repetitively.

Nika najiuliza kwani wananiuzia mke kisa ni afisa ustawi wa jamii?

Ana kipi Cha ziada ambacho wake wa ndg zangu wameolewa na jumla ya mahari tulizotoa na makokoro yote hata milioni haikufika?

Kwani ana kismat Cha mafanikio? Mbona tangu tuingie kwenye relationship mambo mengi tunakimbizana kwa had-hoc za kufa mtu?

Na mengine mengi ambayo si busara kuyaanika humu.

Alifajiri nikaamua kufanya maamuzi magumu ..."Katu sitorudi tena ukweni." Kwa maana kuwa sitoi tena mahari, mtoto wao nimeshamtia mimba ,wakimtaka waje wamchukue.


Ni hayo tu.....sirudi ukweni tena

Mashemeji zangu wachaga povu ruksa. Ila katu sirudi tena ukweni.
Pole mkuu kwa kwenda kuoa kwenye familia njaa kali. Alafu huo sio utaratibu kwa utamaduni wa Wachaga, mahari huwa inalipwa kidogo kidogo. Hiyo ni kukomoana tuu we tulia kama umeshatia mimba watapunguza wenyewe, huwezi amini inaweza kufika 1m tuu au chini ya hapo.
 
Kamanda, jambo LA msingi kama baadhi ya maoni ya wadau, wew wajulishe kiasi ulichokuwa nacho kwa Mara nyingine tena. Wakiendelea kukataa waambie nimeshindwa, then uone watachukua uamuzi gani. Usikimbie kimya kimya
 
USILOLIJUA NI USIKU WA GIZA. Kulipa mahari yote kwa wachaga ni dharau. Hiyo 5m waliyokutajia wanajua kabisa wewe huwezi kuilipa. Pia hata hiyo ya chakula uliyotoa ungesema hauna siku ingepita. Kwa ushauri wangu kama huyo mwanamke unampenda kubali deni lipa unapoweza utapata baraka za wazazi na uende na wazazi wako usiende kihuni. Kulipa mahali inakua kama umemnunua ila ukishindwa kulipa yote sio kosa na inawapa wakwe nguvu angalau ukileta zako utafikiria hata mahari hujamaliza.
Mwisho kama ukitaka kuo uchagani ukitajiwa mahari ni elfu 50. Usije ukalipa yote hapohapo watakuona kiburi. Kubali utailipa kidogokidogo ila usikimbie
Wao ndio wenye dharau, mahari milioni 5!???
 
Dah! Huo mpunga ni mwingi mno, kuna mikoa katika hiyo situation unakopeshwa mke utalipa mbele mbele huko
 
Sawa sawa ila mimi sitalipa gharama ya sherehe siku ya kujadili mahari
Hakuna hiyo.. Wewe unaambiwa toa laki saba tu.... Yangu nne Tatu wapike wali kg 50 nyama kg 15 watu wale story imeisha
 
Hakuna hiyo.. Wewe unaambiwa toa laki saba tu.... Yangu nne Tatu wapike wali kg 50 nyama kg 15 watu wale story imeisha
kwa hiyo bi mkubwa ataambulia zero? hutompa hata kidogo?
Akija kulianzisha timbwi timbwili la Asha ngedere itakuwaje...
 
Wachaga ni noma aisee eti rudisha garama ya kaubwabwa ulikokula,, mzee sina mengi sana ila pole kwa majanga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom