Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Dah poa braza tunaheshimu maamuzi yako, usirudi tu ukweni, sio sababu ya mahari kubwa ila kuombwa kurudisha gharama ya tafrija ile sio sawa kabisa maana we hukuwaambia waandae tafrija ila ni wao kama wao
Ni wachaga ila event waliifanya kiswahili sana
 
Mahari ni kikwazo kikubwa sana siku kwa sisi vijana.

Utajiuliza kuwa baada ya mahari hakutakuwa na harusi au maisha ya ndoa?

Je hujaisaidia hiyo familia kumchukua Binti yao na kuishi naye?

Je undugu hatakuwepo kati ya kwao Binti na kwenu katika kusaidiana kimaisha?

Wazazi wanapaswa wajifunze na kujisahihisha la sivyo wataendelea kuongeza idadi za ma-single mothers kila siku.

Mleta mada uko sahihi kabisa 100%.
True
 
Mahari ni kikwazo kikubwa sana siku kwa sisi vijana.

Utajiuliza kuwa baada ya mahari hakutakuwa na harusi au maisha ya ndoa?

Je hujaisaidia hiyo familia kumchukua Binti yao na kuishi naye?

Je undugu hatakuwepo kati ya kwao Binti na kwenu katika kusaidiana kimaisha?

Wazazi wanapaswa wajifunze na kujisahihisha la sivyo wataendelea kuongeza idadi za ma-single mothers kila siku.

Mleta mada uko sahihi kabisa 100%.
Kulikua na kila dalili kuwa nilikua nafanyiwa udalali na Mzee alikua amepiga ukimyaa tu
 
Utalipa tu iyo ela
Umenikumbusha mjomba wangu juzi tu hapa kaenda kumalizia mahari alipooa na hapo ana watoto wakubwa wameoa na wajukuu kibao kapata.....lazima uje ulipe tu
Leo week ya pili nimeshindwa kabisa kupokea simu ya Baba mkwe na Mshenga wangu.

Iko hivi katika misoto yangu na kukulu kakala za maisha atimae nikajikuta nimedondokea kwa mtoto wa kichaga Kama ilivyo janga kwa wanaume wengi wa mjini.

Mipango ikapangwa na siku ya kufika ukweni kupeleka posa ikafika. Kidume nikajikoki na Mshenga wangu na wadada 3 wa kukodi tukazuka ukweni.

Mambo yalikua shwari hadi pale mjomba mtu akapewa fursa ya kutupangia package ya mahari ili mpango mzima ukamilike.... list ya makorokoro kibao, Mara mkaja wa mama, Bibi, mablanket ya Mama na mashangazi, mbege mapipa matatu, mbuzi 3 wa maziwa na....mwishoni akataja cash money 3 Mil.


Mimi kipindi anataja yale mazaga hata nilikua sifuatilia ,akili yote ilikua inasubiri point ya msingi Cash money.

Badae ikatolewa option ya ku convert the overall cost ika amount Kama 5 Mil. na ushee!

Jitihada za mshenga kupangua bei hazikuzaa matunda. Mbaya zaidi ile tumemaliza events shangazi anatuzuia hakuna kuondoka mpaka tumelipia gharama za maandalizi walioyotufanyia.

Kwa shingo upande nikausukuma mzigo wa M pesa tsh 280, 000 coz walidai laki 3.


Niliporudi lodge usiku mzima sikulala , series nzima ikawa inaji frash back repetitively.

Nika najiuliza kwani wananiuzia mke kisa ni afisa ustawi wa jamii?

Ana kipi Cha ziada ambacho wake wa ndg zangu wameolewa na jumla ya mahari tulizotoa na makokoro yote hata milioni haikufika?

Kwani ana kismat Cha mafanikio? Mbona tangu tuingie kwenye relationship mambo mengi tunakimbizana kwa had-hoc za kufa mtu?

Na mengine mengi ambayo si busara kuyaanika humu.

Alifajiri nikaamua kufanya maamuzi magumu ..."Katu sitorudi tena ukweni." Kwa maana kuwa sitoi tena mahari, mtoto wao nimeshamtia mimba ,wakimtaka waje wamchukue.


Ni hayo tu.....sirudi ukweni tena

Mashemeji zangu wachaga povu ruksa. Ila katu sirudi tena ukweni.
 
Solution hii hapa mkuu

FB_IMG_1569948112007.jpeg
 
Mahari ya milioni 5? Uchagani sehemu gani? Kwanza sisi wachaga tunaamini mahari haishii utalipa mpaka uzeeni.

Labda mshenga wako hakuelewa utaratibu kuna vitu vya muhimu vya kulipa katika mahari ya awali havizidi laki 8.

Vinavyobaki kama mifugo utalipa unavyojisikia mpaka uzeeni.
Kuna jamii za kiafrika zina practise Human traficking
 
Ukiachana na Mahari kuwa 5M plus haijadiliki

Kitendo cha wewe kulipia Gharama za wao kuandaa sherehe hii mpya...

Sitaki kuwahukumu wachaga wote ila kama ndio utaratibu wenu ndugu zangu thats too much!!

5M hiyo unatoa kwa familia ya Mkeo mtarajiwa kama mahari hizi ni gharama ambazo lazma utazilipa kama Bwana Harusi
--- Gauni la Harusi plus Saloon Nafikri
--- Pete za ndoa
--- Suti ya Bwana Harusi
--- Gharama ya Ukumbi
--- Gharama za Kikao cha kwanza
--- Gharama za Usafiri kwenda kulipa 5M
Plus mambo mengne madogo madogo
Mkuu bora umesepa Kibingwa ila mwambie Afisa Ustawi wa Jamii kwamba gharama zimekua kubwa u cant afford ili ajue ukwel.
 
Ndugu nikupe pongezi kwanza kwa kuilipia hiyo Karamu uliyoandaliwa, ningekuwa mimi huyo baba mkwe, mama mkwe, mashangazi wakwe na mtoto wao wasingekuwa na hamu na mimi tena.

Binafsi nilishaweka kikomo kwenye mahari, isizidi milioni hapo ni kila kitu. Mambo ya mkaja wa nani sijui mkaja wa nani mimi yananihusu vipi!?
 
Lengo la huu uzi ni kuwachafua wachaga kuonyesha hawaoleki.
Kaoe kwenu kwa mahari ya kuku hao std 2 hata lasaba hawamalizi. Butu ile mbaya.

Huwezi chukua kichwa huku unalalamika.

Eti umemtia mimba.
Hakika wewe ni .
Mimba inatolewa. Damu ya kijinga kama yako inachafua ukoo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom