Mahari kubwa yamkosesha mke

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
9,504
12,176
Ni kijana mwenzangu sekta ya afya, mwaka huu mwanzoni aliamua kwenda kutoa posa kwa binti ambaye alipanga aanzishe naye familia.

Binti mwajiriwa wa serikali na asili yao ni kanda ya ziwa ila wanaishi na familia katika moja mikoa wa Pwani.

Mshenga alitumwa pamoja na baadhi ya wanafamilia wa kijana.

Kijana aliaandaa milioni 2 mfukoni siku hiyo ambayo alishika mjomba wake .
Kusikilizwa laki 2 , kishika uchumba laki 3 , wakatoa cash.

Mahari ikatajwa ng'ombe 10 @400,000/- jumla mil 4 na vitu vingine milioni 1, jumla ya mahari milioni 5 itolewe yote kwa pamoja bila kuacha deni.

Mshenga akabembeleza pale ila wapi. Wakajibiwa kwa mila za kwao kupunguza mahari ni dharau , hilo Jambo haliwezekani.

Basi ule msafara wake ukarudi bila muafaka.

Kabla ya hapo Kijana alipanga na mchumba wake kuwa mahari itakuwa milioni 2.5 so yeye alijua akitoa milioni 2 akibakisha deni la laki 5, kama tunavyooambiana mtaani mahari haimaliziwi.

Kijana akamtafuta yule binti akamuuliza vp mbona mambo yameenda ndivyo sivyo, alipanga 2.5 wametajiwa 5.

Binti akamjibu kuwa yeye yupo na ndugu zake lazima mila ifuatwe.

Kijana akasema sawa ngoja nikajipange tena nitarudi nikikamilisha.

Ila septemba hii jamaa ananimbia anafikiria kughairi lile swala lake.

Mimi nikamwambia hakikisha ili lak 5 yako unarudishiwa .
 
Mwambie atulie tu. Atakuja pata committed wife kwa kilo tu. Kuna wengi wanathamini ndoa na wanaweza olewa kwa kauli tu na wakawa wake wazuri tu. Huyo msukuma sijui muhaya akae asubiri GSM atakuja kumuoa kwa milioni 5
 
Mahari ni nini?

Kwenye dini, mahari ni zawadi anayopewa binti na mumewe mtarajiwa, zawadi hii inatajwa n mwanamke mwenyewe.

Ni kama vile ahsante yake kwa kukubalia kumuoa,
Ni Umemuomba umuoe, kakubali, sasa ndio unamuomba akutajie zawadi ya kumpa kwa kukubali ombi lako, nae anakutajia(hiyo ndio mahari)
anaekupenda hakukomoi
 
Ni kijana mwenzangu sekta ya afya, mwaka huu mwanzoni aliamua kwenda kutoa posa kwa binti ambaye alipanga aanzishe naye familia.

Binti mwajiriwa wa serikali na asili yao ni kanda ya ziwa ila wanaishi na familia katika moja mikoa wa Pwani.

Mshenga alitumwa pamoja na baadhi ya wanafamilia wa kijana.

Kijana aliaandaa milioni 2 mfukoni siku hiyo ambayo alishika mjomba wake .
Kusikilizwa laki 2 , kishika uchumba laki 3 , wakatoa cash.

Mahari ikatajwa ng'ombe 10 @400,000/- jumla mil 4 na vitu vingine milioni 1, jumla ya mahari milioni 5 itolewe yote kwa pamoja bila kuacha deni.

Mshenga akabembeleza pale ila wapi. Wakajibiwa kwa mila za kwao kupunguza mahari ni dharau , hilo Jambo haliwezekani.

Basi ule msafara wake ukarudi bila muafaka.

Kabla ya hapo Kijana alipanga na mchumba wake kuwa mahari itakuwa milioni 2.5 so yeye alijua akitoa milioni 2 akibakisha deni la laki 5, kama tunavyooambiana mtaani mahari haimaliziwi.

Kijana akamtafuta yule binti akamuuliza vp mbona mambo yameenda ndivyo sivyo, alipanga 2.5 wametajiwa 5.

Binti akamjibu kuwa yeye yupo na ndugu zake lazima mila ifuatwe.

Kijana akasema sawa ngoja nikajipange tena nitarudi nikikamilisha.

Ila septemba hii jamaa ananimbia anafikiria kughairi lile swala lake.

Mimi nikamwambia hakikisha ili lak 5 yako unarudishiwa .
Jamaa apotezee.. apige zake kimya kwa ufupi aendelee na mishe mishe zake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom