Baba mkwe kumbadilisha jina mtoto wangu

Baba mkwe kumbadilisha jina mtoto wangu

Wengine mnakumbwa na hayo kwa kujitakia. Kuoa hujaoa Hugo binti , mtoto unaweza kukuta humuhudumii unaponda maisha tuu na hata mawasiliano umekata, hapo kinachofuata ni hicho! Hiyo ni RED ALERT unatakiwa uichukulie kwa makini.
Vijana wengi wanachukulia kuwa matunzo wa mtoto ni jambo kama LA hiari vile au lisilo na umuhimu kumbe ni LA umuhimu mkubwa hasa akiwa katika umri huo mdogo.
Peleka matunzo kwa kadiri ya kipato chako na utaona utakavyo heshimiwa na mambo kama hayo ya majina huwezi yaona

Sent using Jamii Forums mobile app
Kasome mada kwanza siyo kukurupuka kuandika kwa vile unaweza kuandika. Kuna alipisema hahudumii aunt hamhudumii mtoto?
ID yako na maandishi yako hayafanani kanisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu za mida hii.

Nina mchumba wangu ambaye nilimtolea kishika uchumba, tulibahatika kupata mtoto wa kiume, alijifungulia nyumbani kwetu(Kazi zangu nafanya sehemu ambayo haikumruhusu kujifungulia kwangu) mtoto nikampa jina(la baba yangu mzazi), basi baada ya mwezi mmoja alikwenda kusalimia kwao.

Alipo kaa week mbili mchumba akapiga simu kwangu akasema baba yake anasema anahitaji kumbatiza mtoto siku ya pasaka, kwa jina lake(yaani jina la baba mkwe) na hiyo siku inabidi niwepo kanisani kwao, je ninasemaje? nikamwambia hapana mtoto anatakiwa afate mahali ninakosali mimi hivyo aache tu mtoto atakuja kuwekewa wakfu atakaporudi, maana tutarudi kumchukua binti na kumtolea mahari ili arudi kuendelea na malezi nyumbani kwetu, maana utaratibu wa dini yangu sio ya kule kwao binti akasema sawa.

Jioni ya leo hii baba mkwe kapiga simu kwa mama yangu akisema kwamba anambatiza mtoto pasaka hii, nilipigiwa simu na mama kuniuliza kama hicho kitu nimeambiwa, nikamwambia hapana, nilikataa na nilimueleza kuwa asifanye hivyo.

Nikamrudia binti kumuukiza imekuwaje maagizo niliyoyatoa yamepuuziwa, akaniambia kuwa baba yake amekataa amesema kuwa hawezi kukubali kwa sababu sijamtolea chochote binti yaani mahari, kwa hiyo maamuzi hayo ndio ya mwisho na nyumbani amepiga tu kutoa taarifa.

kwa sasa bado sijafanikisha kutoa mahari, bado naitafuta na nyumbani kwao niliwaeleza kuwa ninajipanga ili nimtolee binti chochote aje kwangu, hivyo nadhani hapo ndio weakness yangu ilipo.

Wakuu hii kitu imekaaje.

Mbona kama nachanganywa,

Ushauri wenu ni wa muhimu.
Kwa hiyo jamii ya jf ikupe msaada gani chief ?
 
Umetoa kishika uchumba,wamekuruhusu kuishi na binti yao kwa mwaka mmoja mpaka akajifungua..
Huenda mzazi wa binti anaamini huna mpango wa kutoa mahari,Kama ungekuwa na nia mwaka mzima ungepeleka chochote,maana kuna watu ambao hukaa na wanawake miaka 15 afu wanabariki ndoa,huenda mzazi wa binti hilo halitaki,nachokuomba au kukushauri ndugu yangu,hapo naona wewe umewakosea wazazi wa msichana wamekuamini kwa mwaka mzima ila umewaangusha katika hilo,ukigundua hilo kosa unaweza jipanga vzur ili huyo baba asimpe mtoto jina lingine,tafuta wazee ambao wanaushawishi mkubwa waende kwa mazazi wamuahidi kuwa mtoto wao ataletewa mahari na wanaomba huo utaratibu alokuwa nao mzazi wa binti usitishwe kwanza kwa kipindi hiko mlichoahidi mtapeleka mahari,after all mahari sio lazima uimalize yote,toa kiasi kidogo uoe kabisa uchukue mke wako. Kama baba wa binti hatataka hilo,jua kabisa hapo kuna shida,hiyo ndoa yako itakuwa inaendeshwa na wazazi/mzazi wa mkeo,hiyo itakuwa hasara kubwa kwako,bora usioe kuliko kufanya hilo kosa.
Hao wazee utakao watuma waende kwa kujua kuwa upande wao wamekosea na wamuhakikishie mzee kuwa hilo Jambo litakaa sawa. Mzee akijua kuwa mmetambua kosa na mpo tayari kurekebisha atalainika na mambo yatakwenda sawa

Nakutakia kila la kheri,mungu akuongoze kwenye hili

Shukran sana
 
Wazinzi bwana mnashangaza sana, mkuu huyo ni mkeo siyo mchumba wako, nenda kachukue mkeo peleka kwenu hiyo ya mahali wazazi wenu ndo watayajenga.
 
Mama mkwe alitaka kuleta upuuuzi wa kunifanyia maamuzi kwenye familia yangu. Nilichokifanya hana hamu na mimi, ukishindwa huo mtihani basi ujue umeolewa rasmi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye kumpa mtoto jina sio sahihi hata. Mtoto wako apewe jina na baba mkwe tangu lini wewe ndio baba wa huyo Mtoto au yeye?Hapa inaonekana itakuja kupata sana shida huko mbeleni ndio ile mkiamua kitu baba kasema baba kasema pole sana una mtihani mkubwa.Na kama wanakufahamu ulishafika huko na ulishatoa kishika uchumba na umewaambia utatoa sioni kama ilikuwa na haja ya kufanya vile
 
Wengine mnakumbwa na hayo kwa kujitakia. Kuoa hujaoa Hugo binti , mtoto unaweza kukuta humuhudumii unaponda maisha tuu na hata mawasiliano umekata, hapo kinachofuata ni hicho! Hiyo ni RED ALERT unatakiwa uichukulie kwa makini.
Vijana wengi wanachukulia kuwa matunzo wa mtoto ni jambo kama LA hiari vile au lisilo na umuhimu kumbe ni LA umuhimu mkubwa hasa akiwa katika umri huo mdogo.
Peleka matunzo kwa kadiri ya kipato chako na utaona utakavyo heshimiwa na mambo kama hayo ya majina huwezi yaona

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, usimu attack kijana, amesema motto ndio kwanza ana mwezi tu, sasa unasemaje hapeleki matumizi ?, nakubaliana na wewe kwamba yawezekana Baba mkwe ameona kijana yuko weak kwenye eneo Fulani, but hiyo haiwezi kuwa sababu ya kujaribu kumpora haki huyo kijana ya kutoa jina kwa mwanae.
 
Sky Elcat na Kantwe naomba mje mtoe ushauri wenu hapa, naamini nafasi ya wanawake waliokomaa kifikra
 
Ninaamimi huyo Baba mkwe ameshakusoma na akajua kuwa wewe ni Fala anaweza kukupelekesha atakavyo..

Wakwe watake wasitake ni lazima waheshimu mipangilio yako wewe muoaji. Wasipotaka waachie Binti yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piga chini huyo mzazi mwenzako, maana inavyo onekana anamsikiliza sana baba take kuliko wewe mume wake mtarajiwa.
Na huyo baba mkwe wako ni msumbufu sana, inaelekea atakuja kukupangia jinsi ya kuishi na mwanae na kukusumbua sana huko mbeleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mke atawaacha wazazi wake nae mume ataacha wazazi wake na kuambatana pamoja, nao watakua mwili mmoja.

Ukiona nyoko nyoko zinakua nyingi achague moja, wew ndio umeowa aua babamkwe?

ALAFU NA KISA CHA MTOTO KUPEWA JINA LA BABU NI NINI?

ushauri wangu yote yapigwe chini hayo majina.
Mtoto apewe Jina lake lisifanane na lako wala la babu.
Acha upotofu, sijui nukuu hiyo umeitolea wapi? Biblia inasema mume atawaacha wazazi wake na kuambatana na mkewe.
Jamaa inabidi atekeleze wajibu wa kuoa na kujipanga, ili kila linalowahusu walifanyie nyumbani kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu za mida hii.

Nina mchumba wangu ambaye nilimtolea kishika uchumba, tulibahatika kupata mtoto wa kiume, alijifungulia nyumbani kwetu(Kazi zangu nafanya sehemu ambayo haikumruhusu kujifungulia kwangu) mtoto nikampa jina(la baba yangu mzazi), basi baada ya mwezi mmoja alikwenda kusalimia kwao.

Alipo kaa week mbili mchumba akapiga simu kwangu akasema baba yake anasema anahitaji kumbatiza mtoto siku ya pasaka, kwa jina lake(yaani jina la baba mkwe) na hiyo siku inabidi niwepo kanisani kwao, je ninasemaje? nikamwambia hapana mtoto anatakiwa afate mahali ninakosali mimi hivyo aache tu mtoto atakuja kuwekewa wakfu atakaporudi, maana tutarudi kumchukua binti na kumtolea mahari ili arudi kuendelea na malezi nyumbani kwetu, maana utaratibu wa dini yangu sio ya kule kwao binti akasema sawa.

Jioni ya leo hii baba mkwe kapiga simu kwa mama yangu akisema kwamba anambatiza mtoto pasaka hii, nilipigiwa simu na mama kuniuliza kama hicho kitu nimeambiwa, nikamwambia hapana, nilikataa na nilimueleza kuwa asifanye hivyo.

Nikamrudia binti kumuukiza imekuwaje maagizo niliyoyatoa yamepuuziwa, akaniambia kuwa baba yake amekataa amesema kuwa hawezi kukubali kwa sababu sijamtolea chochote binti yaani mahari, kwa hiyo maamuzi hayo ndio ya mwisho na nyumbani amepiga tu kutoa taarifa.

kwa sasa bado sijafanikisha kutoa mahari, bado naitafuta na nyumbani kwao niliwaeleza kuwa ninajipanga ili nimtolee binti chochote aje kwangu, hivyo nadhani hapo ndio weakness yangu ilipo.

Wakuu hii kitu imekaaje.

Mbona kama nachanganywa,

Ushauri wenu ni wa muhimu.

Tafuta hela kwa vyovyote ukamilishe unachotakiwa kufanya.
 
Back
Top Bottom