Baba mkwe kumbadilisha jina mtoto wangu

Baba mkwe kumbadilisha jina mtoto wangu

Mkeo ndio anatakiwa awe upande wako kwa kila kitu,labda ni mbinu yao ya kushinikiza ulipe mahali,mueleweshe vizuri mkeo mtarajiwa hayo maisha ni yako wewe na yeye na sio wazazi,mbegu ulitupia wewe dingi anachukuaje nafasi ya kukuamlia kwenye ndoa yako?!! Kama vipi dem achague wewe au baba,na ni bora afanye mapema ili uvute kitu cha imani yako kabisa.

macson
Sawa mkuu
 
Ningekuwa mim namwambia binti,kama unataka kuolewa rudi kwangu ukaolewe kama hautaki endelea kubaki hukohuko, mahari nitatoa kwa muda niliopanga mimi kama babako hataki baasi, mahali sio lazima na kukuoa wewe sio lazima pia.Na binti anatakiwa kuelewa sio kila mzazi ana busara wengine ni wa hovyo kabsa.
 
Huyo sio baba mkwe wako, hujatimiza vigezo vya kumuita baba mkwe, malizia mahari Kisha uoe uwe na uwezo wa kuamua juu ya mke wako. Akusubirie wewe je usipomuoa binti yake? ,
 
Ndio ni neno sahihi na lipo kwenye kamusi ya kiswahili. Huyo ni kimada sio mchumba uchumba unakamilika mara baada ya taratibu zote kufuatwa kama kutolewa posa kuchumbiwana kulipiwa mahari iwe chochote kile makubaliano kutokana na mila na desturi ya sehemu husika. Huyo sio mchumba wake ni kimada wake ndio maana mzee ana hasira ya kuto..mbewa mtoto bila kufuata taratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi jamaa atulize boli. Huyo si baba mkwe wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo sio baba mkwe wako, hujatimiza vigezo vya kumuita baba mkwe, malizia mahari Kisha uoe uwe na uwezo wa kuamua juu ya mke wako. Akusubirie wewe je usipomuoa binti yake? ,
Sawa.
 
Sema ukikadiria uhalisi wa mtu kwa mwandiko wake wa jf mara nyingi lazima utaingia chaka. Mtu kama mimi, sifananii hata kidogo na mwandiko wangu humu.

Yeah,ni kweli
JF unaweza kukadiria mtu ikawa tofauti sana na uhalisia
 
Wakuu za mida hii.


Nina mchumba wangu ambaye nilimtolea kishika uchumba, tulibahatika kupata mtoto wa kiume, alijifungulia nyumbani kwetu(Kazi zangu nafanya sehemu ambayo haikumruhusu kujifungulia kwangu) mtoto nikampa jina(la baba yangu mzazi), basi baada ya mwezi mmoja alikwenda kusalimia kwao.

Alipo kaa week mbili mchumba akapiga simu kwangu akasema baba yake anasema anahitaji kumbatiza mtoto siku ya pasaka, kwa jina lake(yaani jina la baba mkwe) na hiyo siku inabidi niwepo kanisani kwao, je ninasemaje? nikamwambia hapana mtoto anatakiwa afate mahali ninakosali mimi hivyo aache tu mtoto atakuja kuwekewa wakfu atakaporudi, maana tutarudi kumchukua binti na kumtolea mahari ili arudi kuendelea na malezi nyumbani kwetu, maana utaratibu wa dini yangu sio ya kule kwao binti akasema sawa.


Jioni ya leo hii baba mkwe kapiga simu kwa mama yangu akisema kwamba anambatiza mtoto pasaka hii, nilipigiwa simu na mama kuniuliza kama hicho kitu nimeambiwa, nikamwambia hapana, nilikataa na nilimueleza kuwa asifanye hivyo.

Nikamrudia binti kumuukiza imekuwaje maagizo niliyoyatoa yamepuuziwa, akaniambia kuwa baba yake amekataa amesema kuwa hawezi kukubali kwa sababu sijamtolea chochote binti yaani mahari, kwa hiyo maamuzi hayo ndio ya mwisho na nyumbani amepiga tu kutoa taarifa.


kwa sasa bado sijafanikisha kutoa mahari, bado naitafuta na nyumbani kwao niliwaeleza kuwa ninajipanga ili nimtolee binti chochote aje kwangu, hivyo nadhani hapo ndio weakness yangu ilipo.




Wakuu hii kitu imekaaje.

Mbona kama nachanganywa,

Ushauri wenu ni wa muhimu.

Jaribu kufuatilia Mila za hilo Kabila la baba mkwe, Nachojua kuna baadhi ya makabila kama hujatoa mahari huna mamlaka yoyote. Yaani utakuta mtoto anaitwa jina la ukoo wa mama na hata akifa wao ndio wanazika.
Halafu ukiwatingishia kiberiti unakuta wala hawajali niliona kwa kijana wa dada angu alikuwa na kesi kama yako akatingisha kiberiti wakamjibu nenda zako tuko na uwezo wa kutunza mjukuu wetu hata akitaka kusoma ulaya tutampeleka afterall ukoo wetu tunataka upanuke wewe nenda tu.
Ilibidi tuwe wapole baada ya kulipa mahari tu na wala hata haikuwa kubwa walikubali kila kitu mpk leo hizi familia zinaishi kwa amani tu.
 
Kuna familia hazitaki utani. Wewe hata mahari hujatoa mamlaka ya mtoto unatoa wap.
Kwanini walimuacha alee mimba na kuacha binti yao ana jifungulia kwa mwanaume?
Walimpaje mamlaka hayo kama hajatoa mahali?
 
Back
Top Bottom