Baba mkwe kumbadilisha jina mtoto wangu

Gustavo Gaviria

JF-Expert Member
Nov 19, 2018
630
1,109
Wakuu za mida hii.

Nina mchumba wangu ambaye nilimtolea kishika uchumba, tulibahatika kupata mtoto wa kiume, alijifungulia nyumbani kwetu(Kazi zangu nafanya sehemu ambayo haikumruhusu kujifungulia kwangu) mtoto nikampa jina(la baba yangu mzazi), basi baada ya mwezi mmoja alikwenda kusalimia kwao.

Alipo kaa week mbili mchumba akapiga simu kwangu akasema baba yake anasema anahitaji kumbatiza mtoto siku ya pasaka, kwa jina lake(yaani jina la baba mkwe) na hiyo siku inabidi niwepo kanisani kwao, je ninasemaje? nikamwambia hapana mtoto anatakiwa afate mahali ninakosali mimi hivyo aache tu mtoto atakuja kuwekewa wakfu atakaporudi, maana tutarudi kumchukua binti na kumtolea mahari ili arudi kuendelea na malezi nyumbani kwetu, maana utaratibu wa dini yangu sio ya kule kwao binti akasema sawa.

Jioni ya leo hii baba mkwe kapiga simu kwa mama yangu akisema kwamba anambatiza mtoto pasaka hii, nilipigiwa simu na mama kuniuliza kama hicho kitu nimeambiwa, nikamwambia hapana, nilikataa na nilimueleza kuwa asifanye hivyo.

Nikamrudia binti kumuukiza imekuwaje maagizo niliyoyatoa yamepuuziwa, akaniambia kuwa baba yake amekataa amesema kuwa hawezi kukubali kwa sababu sijamtolea chochote binti yaani mahari, kwa hiyo maamuzi hayo ndio ya mwisho na nyumbani amepiga tu kutoa taarifa.

kwa sasa bado sijafanikisha kutoa mahari, bado naitafuta na nyumbani kwao niliwaeleza kuwa ninajipanga ili nimtolee binti chochote aje kwangu, hivyo nadhani hapo ndio weakness yangu ilipo.

Wakuu hii kitu imekaaje.

Mbona kama nachanganywa,

Ushauri wenu ni wa muhimu.
 
Mke atawaacha wazazi wake nae mume ataacha wazazi wake na kuambatana pamoja, nao watakua mwili mmoja.

Ukiona nyoko nyoko zinakua nyingi achague moja, wew ndio umeowa aua babamkwe?

ALAFU NA KISA CHA MTOTO KUPEWA JINA LA BABU NI NINI?

ushauri wangu yote yapigwe chini hayo majina.
Mtoto apewe Jina lake lisifanane na lako wala la babu.
 
Mkuu haya mambo kidogo yanachanganya nilimpa jina mtoto wangu kumuenzi baba yangu.
 
Waambie kwasababu haujagoma kulipa mahari basi wasitishe ilo zoezi la ubatizaji na wakupe mda ufanye kile wanachotaka {kulipa mahari) kama wakigoma basi nawewe ukaoa uyo binti basi kazi utakua nayo mbeleni, mpigie binti simu mwambie awaambie wazazi wake upo tayari kulipa mahari so wasifanye icho wanachotaka kufanya na kama wakikataa wakalazimisha basi hauoni haja na kuendelea nae(apa unatingisha kiberiti uone watareact vipi)
 
Sawa mkuu

Kazi ninayo
 
Hapo mzeee amekosea sana. Analeta ukoloni, ingekuwa umekataa kuchukua majukumu kama baba wa kid sawa.

Huyo ni mtoto wako, sio wa kwake. Mtoto wake ni huyo binti ndio ana uhuru naye kwa % nyingi sana.

Kufanya lolote kwa mtoto wako ni lazima akuhusishe, ukikataa basi, sio kulazimisha kujifanya yeye ndio baba wa binti.

Eti anathamin mahari kisa haujalipa, kwani kitendo cha kuoa ni lazima, au ukiamua kutoa kuaoa, utakosa Custody ya mtoto na kuwa baba wa kid.

Hao ndio wazee wanaokuw na njaa na ukolon wa kudai na kuthamini sana mahari kuliko utu na heshima, hii inasababisha baadhi ya wanaume kuwa kataza hata wake zao kwenda makwao. Utashangaa unalipia mahari harafu kesho unasikia shida ukweni, man wengi wanaaumua ku mute kwa vitendo kama hivi.

Ningelikuwa mimi, sipendi dharau. Ningesema clear kabisa, mzee hiyo ni damu yangu. Mimi ndio baba wa mtoto, kwani nikilipa mahari ndio ntakuwa nmeununua ubaba halisi wa mwanangu?? Nawasihi mnisikize mimi lakini kinyume na hapo, SITO HUSIKA NA MATOKEO YA HAYO MNAYOFANYA.
 
Back
Top Bottom