Baba adaiwa kumuua, kumzika mtoto wake wa miaka 5 porini

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
GEITA: Mtoto Dickson Elias (5) mkazi wa Chikobe, Kata ya Butundwe, Wilaya ya Geita mwenye ulemavu wa viungo, ameuawa na baba yake mzazi kisha kuzikwa porini kwa madai ya kushindwa kuendelea kumlea baada ya mama mzazi wa mtoto huyo kurudi kwao.

Kufuatia mauaji hayo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, linamshikilia Elias Bukumie (32) ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo kwa tuhuma za mauaji.

Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo, amesema mwili wa mtoto huyo ulionekana porini na wasamaria wema.

“Wasamaria wema wakiwa porini, waliona mwili wa mtoto wa miaka mitano. Taarifa za awali zilisema amechunwa ngozi na kukatwa ulimi. Timu yetu ya upelelezi ilikwenda hadi Kijiji cha Chikobe na kuukuta mwili wa mtoto ambaye inaonekana alikuwa mlemavu wa viungo,” amesema Kamanda Jongo.

CHANZO: Mwananchi
 
Dunia haina huruma hivi wazazi wake huyo shetani wangemfanya hivyo angekuwepo fala huyo, ache akawe mke wa nyampala, kama mtu imeshindikana si kuna vituo vya watoto,
 
GEITA: Mtoto Dickson Elias (5) mkazi wa Chikobe, Kata ya Butundwe, Wilaya ya Geita mwenye ulemavu wa viungo, ameuawa na baba yake mzazi kisha kuzikwa porini kwa madai ya kushindwa kuendelea kumlea baada ya mama mzazi wa mtoto huyo kurudi kwao.

Kufuatia mauaji hayo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, linamshikilia Elias Bukumie (32) ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo kwa tuhuma za mauaji.

Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo, amesema mwili wa mtoto huyo ulionekana porini na wasamaria wema.

“Wasamaria wema wakiwa porini, waliona mwili wa mtoto wa miaka mitano. Taarifa za awali zilisema amechunwa ngozi na kukatwa ulimi. Timu yetu ya upelelezi ilikwenda hadi Kijiji cha Chikobe na kuukuta mwili wa mtoto ambaye inaonekana alikuwa mlemavu wa viungo,” amesema Kamanda Jongo.

CHANZO: Mwananchi
Mungu Baba tusamehe sisi wakosaji.

Maasi yamezidi sana loh
 
Kuna nini huko Geita lakini! Kuwa mlemavu haiwezi kumfanya mtu kukosa haki zake za msingi.

Apumzike kwa Amani mtoto Dicky.
 
GEITA: Mtoto Dickson Elias (5) mkazi wa Chikobe, Kata ya Butundwe, Wilaya ya Geita mwenye ulemavu wa viungo, ameuawa na baba yake mzazi kisha kuzikwa porini kwa madai ya kushindwa kuendelea kumlea baada ya mama mzazi wa mtoto huyo kurudi kwao.

Kufuatia mauaji hayo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, linamshikilia Elias Bukumie (32) ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo kwa tuhuma za mauaji.

Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo, amesema mwili wa mtoto huyo ulionekana porini na wasamaria wema.

“Wasamaria wema wakiwa porini, waliona mwili wa mtoto wa miaka mitano. Taarifa za awali zilisema amechunwa ngozi na kukatwa ulimi. Timu yetu ya upelelezi ilikwenda hadi Kijiji cha Chikobe na kuukuta mwili wa mtoto ambaye inaonekana alikuwa mlemavu wa viungo,” amesema Kamanda Jongo.

CHANZO: Mwananchi
Shetani katika umbile la mtu
 
Huyu mwanaume anaua tu mtoto hajui uchungu wa kubeba mimba na masaibu yake. Evil man, rest in peace poor and innocent child
 
Back
Top Bottom