(Baadhi ya) Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

(Baadhi ya) Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lokissa, Feb 2, 2011.

 1. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ulipaji fidia wa DOWANS

  *Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao
  *Kafulila apingana nao


  Stella Aron na Anneth Kagenda, jijini
  Wednesday, 02 February 2011


  SAKATA la ulipaji wa fidia ya Sh.bilioni 94 kwa kampuni ya DOWANS kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na kukiuka mkataba,Taasisi ya Kutetea Haki za Waislam,imeibuka na kuishauri Serikali kuharakisha malipo hayo harakaiwezekanavyo kwani ni haki yao kisheria.

  Wakati taasisi hiyo ya Imam Bukhary ikiishauri hivyo Serikali, Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila ameiomba Serikali itoe maelezo ya kina kuhusiana na ulipaji wa fidia hiyo.


  Mwenyekiti wa taasisi ya kiislam, Sheikh Khalifa Khamis akizungumza na Dar Leo amesema kuwa, DOWANS inatakiwa ilipwe kwakuwa ina mikataba ya kisheria hivyo kitendo cha kutokulipwa ni sawa na unyanyasaji na si uungwana.


  " Mikataba ipo na inaonyesha Serikali inaitambua, hivyo kwanini wasilipwe fedha zao, kwani kuvunja mkataba kwa sheria yetu ya dini ya Kiislam ni haramu kama waliandikiana mkataba walipwe hata kama ni matapeli sisi ndiyo wenye makosa,"amesema Sheikh Khamis.


  Amesema kuwa, Serikali ndiyo yenye makosa kwa kuingia mkataba na kampuni hiyo bila ya kujiridhisha hivyo inapaswa kuilipa ili ijifunze siku nyingine kuingia mikataba bila kuifanyia uchunguzi wa kina.


  Ameongeza kuwa, kuna baadhi ya wabunge ndiyo walioshinikiza kuvunjwa kwa mkataba huo kutokana na chuki zao binafsi hivyo kitendo hicho ndicho kinachoigharimu Serikali hivi sasa.


  SOURCE: DAR LEO 2/2/'11
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  DarLeo wametafuta habari ya kuuzia gazeti.

  Hiyo taasisi hata haijulikani halafu ndo wanaitumia kuwawakilisha waislamu. Huyo sheikh mwenyewe hana sababu zozote za msingi kushadidia hoja yake.

  Ama la nao wanaendeleza wimbo wa udini, kesho tutasikia wameenda kumhoji mchungaji wa kanisa gani sijui.
   
 3. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Sasa Waisilamu ndio watanzania wote? Hizi habari za udini zinakolezwa na chama tawala. Absolutely stupid.
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  stupid at its best
   
 5. m

  mzee wa pwani New Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu Sheikh ni ndugu yake Rost Utamu
   
 6. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Duu! CCM kiboko, sasa wameona waipeleke hoja hii kwenye dini ili ianze kuleta mtafaruku kwa wananchi! Unajua dini siyo nzuri kuzijadili huku coz zinabeba imani za watu, na watu wako tayari kufia dini zao. Cha msingi tunapojadili hili swala tusiseme Waislam, mtajeni huyo mheshimiwa anayeitwa Khamis ili kutoleta mambo ya kiimani. Waweza kuta Khamis ni mwanachama mzuri wa CCM sasa wanataka kumtumia kuwaongelea waislam wote, Magazeti yaache kuandika uzushi na kuwataja waislam au wakristo!
   
 7. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Huyu Mhes Immam Bukhary hajui kwamba fedha inayolipwa ni mali ya Watanzania, at the end of the day yeye na Mtanzania yeyote yule ndiye atakaye lipa. Maana yake kodi zitapandishwa tena, yaani vitu vitapanda bei, hiyo itasabaisha inflation fedha zetu zitakosa thamani.

  Hata kama mikataba ni ya kanjanja tujinasue sasa, wasomi situnao wacha wafanye kazi zao!!!!!!!!!
  Masikini Tanzania tutakuwa watumwa wa madeni, tutakosa jinsi ya kujikwamua shauri ya ujanja wa watu wachache wanao onga fedha za ufisadi huko makanisani pamoja na misikitini na sisi mbumbumbu tunawaona waungwana kwa fedha za laana.

  Hebu tugutuke tujue kuwa hizo fedha ni nguvu za Watanzania pamoja na vizazi vyetu. Zingefanya miradi ya maendeleo kama zipo. Hao ni wezi wa mchana kweupe, ngoja katiba mpya itue tuone ujanja wao, maana wanabebwa na katiba dhaifu hii tuliyonayo. Maalimu wafunguke macho wasishabikie uozo maana tutateseka wote. Bei za vitu zikipanda tutaumia wote.

  Muogope Mungu yeye hakubaliani na wezi, tuwakatae hao mafisadi tuwapige vita tusiwakumbatie!

  DOWANS HAKUNA KULIPA!!!!!!!
   
 8. k

  kaka mtu Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waislam wameitaka serikali iilipe Dowans bil 94 haraka kwa sababu ni haki yao (dowans) kisheria. Nimeyasikia hayo radio free africa ktk uchambuzi wa gazeti la Dar leo saa 05:00pm.


  Hivi RA ana mkono hadi kwa waislam?. Mbona wanamtetea?
  Nawasilisha..
   
 9. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Kichwa cha habari cha gazeti na cha mada hii si sahihi. Wanaotajwa sidhani kama ni wawakilishi wa Waislam bali wa hiyo taasisi iliyotoa kauli yake. Hatuwezi kusikiliza kauli ya kila mtu na kuibandika kwenye jamii pana.

  Msitake kuwafanya Waislamu waonekane watu wa ajabu nchini. Halafu, kama walivyosema wengine hapa, hii ni kuendeleza ujinga ulioanzishwa na baadhi ya wanasiasa waliofilisika kwa manufaa yao.
   
 10. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Siyo waislam bali baadhi ya waislam. Hao ni wale ambao hawaishi kwenda kwake kuombaomba na sasa wanajikomba kwake.
  Hivi ni muislam gani hataumia iwapo dowans italipwa?; hivi hao polisi waliokosa posho zao hakuna waislam humo? Hivi bei ya umeme ilipopandishwa waislam wana mita zao tofauti au wana bei yao tofauti?.

  Jamani tusijidanganye, suala la dowans si la kidini!

  Tusitoke kwenye mada.
   
 11. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmmmmmhhhhh, habari nyingine ukisikia mpaka mwili unasisimka!!!!!!:twitch:
   
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nadhani gazeti halikuwa fair; kwa nini lisiseme Sheik Halifa na badala yake wageneralize kuwa ni Waislamu? Magazeti mengine yanataka kukuza mambo na kuuza tu kwa kutumia mgongo wa Waislamu.
   
 13. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Umenena vema, nakuunga kwa hoja yako nzuri.
   
 14. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  ameshapewa hela ya chai then akatumwa aonekane anawasemea waislam.
   
 15. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Acha kuongea upumbavu... waislam ndio nani..? Mbona mimi muislamu sijui sijasema hivyo and I know about 1.2 billion others who are not of that opinion. JF is full of imbecilic morons like you... Cite the appropriate authority sio unageneralize watu.. Fisi we! lol
   
 16. Daudi Paul

  Daudi Paul Member

  #16
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  Haiwezekani kama wao wanaona ni fair basi wawachangie lakini cio kutoka kwenye kodi zetu:sick:
   
 17. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #17
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Bado sitaki kuamini kama ni Waislam wamesema hayo....labda kama ni kikundi cha watu wenye majina ya Waislam wamesema hivyo kwa maslahi yao
   
 18. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kinyambiss,
  Hiyo haikuwa ni kauli ya 'kaka mtu-mwenye thread hii' bali ametoa habari kupitia chanzo alichokisikia jioni hii na kutujuza wengine tulio bado maofisini na ambao hatujasikia taarifa hiyo redioni, hivyo si kumtendea haki kwa kumshutumu kwa hali yake ya kutujuza. Yeye sie aliyesema mkuu.
  Let's be realistic and firm on issues.
   
 19. k

  kabindi JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jinsi Nchi inavyozidi kupata matatizo tunazidi kuona watu wenye akili na wapumbavu! Kama Sheikh Halifa Amezungumza hayo kwa niaba ya waislamu, basi nadhani atakuwa amewaaibisha na ni lazima awaombe msamaha! maana tunajua ni waislamu wengi wenye akili timamu kama wakristo.

  Lakini kama ni mawazo yake, basi ni miongoni mwa wale wapumbavu wenye mtindio wa ubongo! si yeye peke yake bali wapo pia wakristo ndani ya CCM wenye mawazo kama hayo! Nenda kawaulize baadhi ya Mawaziri(si wote) wa Kikwete ambao ni Wakristo! utasikia wanachokisema! ni kwa kuwa wanjikomba kwa Kikwete! UPUMBAVU MTUPU wa mawazo ya akina Sheikh Halifa/Halima.
   
 20. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Someni wenyewe hiyo habari hapa Ulipaji fidia wa DOWANS

  Ulipaji fidia wa DOWANS
  Wednesday, 02 February 2011 09:30

  *Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao
  *Kafulila apingana nao


  Stella Aron na Anneth Kagenda, jijini

  SAKATA la ulipaji wa fidia ya Sh.bilioni 94 kwa kampuni ya DOWANS kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na kukiuka mkataba,Taasisi ya Kutetea Haki za Waislam,imeibuka na kuishauri Serikali kuharakisha malipo hayo harakaiwezekanavyo kwani ni haki yao kisheria.

  Wakati taasisi hiyo ya Imam Bukhary ikiishauri hivyo Serikali, Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila ameiomba Serikali itoe maelezo ya kina kuhusiana na ulipaji wa fidia hiyo.


  Mwenyekiti wa taasisi ya kiislam, Sheikh Khalifa Khamis akizungumza na Dar Leo amesema kuwa, DOWANS inatakiwa ilipwe kwakuwa ina mikataba ya kisheria hivyo kitendo cha kutokulipwa ni sawa na unyanyasaji na si uungwana.


  " Mikataba ipo na inaonyesha Serikali inaitambua, hivyo kwanini wasilipwe fedha zao, kwani kuvunja mkataba kwa sheria yetu ya dini ya Kiislam ni haramu kama waliandikiana mkataba walipwe hata kama ni matapeli sisi ndiyo wenye makosa,"amesema Sheikh Khamis.

  Amesema kuwa, Serikali ndiyo yenye makosa kwa kuingia mkataba na kampuni hiyo bila ya kujiridhisha hivyo inapaswa kuilipa ili ijifunze siku nyingine kuingia mikataba bila kuifanyia uchunguzi wa kina.


  Ameongeza kuwa, kuna baadhi ya wabunge ndiyo walioshinikiza kuvunjwa kwa mkataba huo kutokana na chuki zao binafsi hivyo kitendo hicho ndicho kinachoigharimu Serikali hivi sasa.
   
Loading...