(Baadhi ya) Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao

Kwani hiyo taasisi ina uhusiano au inatambulika na BAKWATA??
 
natamani tarehe 24 iwe kesho ilituanze kazi rasmi tumalize utata wa dowans
 
Hivi Rais hataki kutoa tamko kuhusu Dowans kwa nn?

Waziri Stephen Wasira juzi alipobanwa kuhusu Dowans alitamka hivyo kuwa '...raisi hawezi kulizungumzia hilo suala..'. Swali linabaki palepale Kwanini asilizungumzie? Vilio vyote hivi,malalamiko yote haya hayasikii na ameamua kuweka pamba masikioni? Akumbuke uvumilivu unamwisho wake. Aangalie upepo wa Tunisia na Misri utabadili mwelekeo siku si nyingi kuelekea kusini na Dowans ndo ufunguo. Ajiandae kulikabili hilo.
 
kwani wakuu hamjamjua rostam azizi ...kama ambavyo misri zipo pande mbili wapo wendawazimu wanaomtetea hosni mubarak hao ni maswaiba wa rostam azizi nasio wa mtume muhammad{s.a.w} kwanza uislamu hamjui rostam azizi na uislamu haujaja duniani kuja kuleta umeme wa dowans mbona rostam alishatoa msaada hata church ili wamtetee...kufa kwa nyani ..huyu ataondoka tu arudi kwake irani.
 
Naona hii thread imekaa kichochezi ila mimi ni moja wa waislamu nakutuma ukamjibu huyo sheikh wako Uislamu hauruhusu kudhulumu, na mtume muhammad SAW anasema jitahidi kuzuia muislamu mwenzio asidhulumu wala asidhulumiwe. Sasa mpelekee taarifa hiyo.
 
Rostam sijamsikia akichanga kwa Waisilamu kama vile kujenga misikiti n.k. Ila iliripotiwa aliwahi kulisaidia kanisa la Mtikila na wanakwaya wa KKT Kinondoni.

Hivyo hii habari ya huyu sheikh kutaka alipwe haraka inanishangaza -- something is not right at all!
 
Am sick and tired of hearing about dowans..i mean hili suala c liko court afu najua tatizo ni kufunjwa mkataba ,breach of contract au cjui unlawfull termination huyu mwakyembe na kamati yake wametuingiza mkenge WASHUGHULIKIWE .Afu ndo turudi kuchunguza hawa dowans wameiba kiasi gani na WAPI? Je kipindi mashine zao zinafanya kazi wametuuzia umeme kweli ama zilikua zinaungurumishwa tu bila kutoa megawat na wakalipwe kwa umeme hewa.
Kama hawakutuzia hewa MAN AM AFRAID THEY ARE GOING TO BE PAID.
Whinning,complaining,crying etc cant help.
Tujifunze tu sasa mbunge hatakiwi kumiliki kampuni kama dowans kisha achukue kandarasi humu TZ..Tunataka WAZUNGU
 
Devil is busy working.....mayb chi chi em imeanza tena kutumia viongozi wa dini walafi kama mtaji na kwenye swala la do wansi bt hatudanganyiki.....sumu hajaribiwi kwa kuilamba
 
Ulipaji fidia wa DOWANS

*Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao
*Kafulila apingana nao


Stella Aron na Anneth Kagenda, jijini
Wednesday, 02 February 2011


SAKATA la ulipaji wa fidia ya Sh.bilioni 94 kwa kampuni ya DOWANS kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na kukiuka mkataba,Taasisi ya Kutetea Haki za Waislam,imeibuka na kuishauri Serikali kuharakisha malipo hayo harakaiwezekanavyo kwani ni haki yao kisheria.

Wakati taasisi hiyo ya Imam Bukhary ikiishauri hivyo Serikali, Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila ameiomba Serikali itoe maelezo ya kina kuhusiana na ulipaji wa fidia hiyo.


Mwenyekiti wa taasisi ya kiislam, Sheikh Khalifa Khamis akizungumza na Dar Leo amesema kuwa, DOWANS inatakiwa ilipwe kwakuwa ina mikataba ya kisheria hivyo kitendo cha kutokulipwa ni sawa na unyanyasaji na si uungwana.


" Mikataba ipo na inaonyesha Serikali inaitambua, hivyo kwanini wasilipwe fedha zao, kwani kuvunja mkataba kwa sheria yetu ya dini ya Kiislam ni haramu kama waliandikiana mkataba walipwe hata kama ni matapeli sisi ndiyo wenye makosa,"amesema Sheikh Khamis.


Amesema kuwa, Serikali ndiyo yenye makosa kwa kuingia mkataba na kampuni hiyo bila ya kujiridhisha hivyo inapaswa kuilipa ili ijifunze siku nyingine kuingia mikataba bila kuifanyia uchunguzi wa kina.


Ameongeza kuwa, kuna baadhi ya wabunge ndiyo walioshinikiza kuvunjwa kwa mkataba huo kutokana na chuki zao binafsi hivyo kitendo hicho ndicho kinachoigharimu Serikali hivi sasa.


SOURCE: DAR LEO 2/2/'11

Wakati mwingine nafikiri huwa tunakosea tunapojumlisha kila mtu katika kundi fulani (kiutaalamu inaitwa fallacy of overgeneralization). Haiwezekani kabisa waislamu wote wasiopungua 30% ya watanzania wakataka DOWANS ilipwe hata kama anayesema ni mwajiriwa wa TISS sheikh Simba. Humu mitaani tunamoishi kuna waislamu wengi mno wasiotaka DOWANS ilipwe sasa hili gaze la CCM linamaanisha nini kugeneralise? Naanza kuhisi kuwa CCM inalitumia Habari Leo kama vile ilivyokuwa ikiitumia taasisi mfu ya REDET. Naamini kabisa kama DR% Salmin Ahmed Salim asingetukanwa na Dr Dr Dr na kuitwa terrorist wa Hizbu mwaka 2005 kwenye kura za maoni, hii nchi ingekuwa mbali mno. Ni afadhali kuwa na kiongozi muislamu wa kweli kuliko kuwa na mtu anayejiita muislamu (hata msikitini haendi) huku akitumia udini kubaki madarakani. KWa ndugu zangu member na Senior Member mnaosema siweza kutengeneza hoja, ni majuzi tu hap[a CAmbridge University alikuja Sheikh (namuifadhi jina) kutoa hoja ya uislamu na maendeleo. Alinikuna aliposema ipo tofauti kati ya MOSLEMS na ISLAMISTS. Muheshimiwa Dr Dr Dr na huyu Imam Bukhary moslems, na Dr Salim ni Islamist. Tofauti ni nini, jaribu kutumia ubongo utapata jibu lake ila kama mimi nisie muislamu najua hilo, inabidi wengine wajue zaidi.
 
Najiuliza ni kwanini mwandishi hakufuata taluma yake ipasavyo? kabisa hii taarifa haiwakilishi Waislamu wote...wataka tu hao kuuza magazeti
 
Hoja yao ni ya msingi, huwezi vunja mkataba hivi hivi , lakini pia imetawaliwa na udini wa kulinda serekali iliyo na waislamu wengi!
 
Nadhani gazeti halikuwa fair; kwa nini lisiseme Sheik Halifa na badala yake wageneralize kuwa ni Waislamu? Magazeti mengine yanataka kukuza mambo na kuuza tu kwa kutumia mgongo wa Waislamu.

Tujiulize lengo la gazeti, lengo la hao waliotoa kauli. lengo ni kupotosha umma. hii habari ya udini kwa ujumla wake ni ajenda ya wanasiasa uchwara ambao wanatumia vyombo mbalimbali vya habari kueneza upuuzi huu, ili kupata leverage katika hali ya kisiasa ilivyo sasa nchini na mwelekeo wake. wanajua kwamba watu wengi hawatafakari kwa nini kitu hiki kinazungumzwa, bali wanaangalia tu kile kinacholetwa mbele yao na kikifakamia.

Niliwahi kubishana na mmarekani mmoja wakati ule US imevamia Iraq. alikuwa conviced na maelezo ya akina Bush & Rumsfeld kuhusu WMD. mimi nikamwambia hapa kuna ulterior motives. wakati huo kule marekani mtu akionekana kueleza wazo tofauti anaonekana kama msaliti. ukweli ulikuja julikana baadae, lakini imewagharimu sana marekani.

Uislamu au Ukristu, yaani udini, sio hoja kabisa kwa watanzania wa kawaida. ni vitu vinavyopandikizwa tu. lesser minds wanakuwa excited pale dini "pinzani" inapoonekana kufanya jambo la aibu au upuuzi, na wanashabikia. wenye dini yao wanatafuta namna ya kujitetea, na kutafuta tope katika dini pinzani ili walipe kisasi! greater minds wanajiuliza why all this talk and where does it lead us? of course it misleads us, from the real topics and real issues, to nonsense.
 
Duu! CCM kiboko, sasa wameona waipeleke hoja hii kwenye dini ili ianze kuleta mtafaruku kwa wananchi! Unajua dini siyo nzuri kuzijadili huku coz zinabeba imani za watu, na watu wako tayari kufia dini zao. Cha msingi tunapojadili hili swala tusiseme Waislam, mtajeni huyo mheshimiwa anayeitwa Khamis ili kutoleta mambo ya kiimani. Waweza kuta Khamis ni mwanachama mzuri wa CCM sasa wanataka kumtumia kuwaongelea waislam wote, Magazeti yaache kuandika uzushi na kuwataja waislam au wakristo!


sio uzushi hata mimi nilimsikia huyo sheikh kwenye taarifa ya habari ya times fm jana usiku,..ni wazi kuwa baadhi ya waislam wataitetea serikali hata kwa maovu ili mradi tu wamemtetea muislam mwenzao(JK).,hapo ndipo shule inapoanza kuonyesha umuhimu wake....of course kikwete anawatuma
 
Waislam wameitaka serikali iilipe Dowans bil 94 haraka kwa sababu ni haki yao (dowans) kisheria. Nimeyasikia hayo radio free africa ktk uchambuzi wa gazeti la Dar leo saa 05:00pm.


Hivi RA ana mkono hadi kwa waislam?. Mbona wanamtetea?
Nawasilisha..
Waislamu hawamtetei mtu ni lazima ufikiri vizuri kwamba Khamisi ndio msemaji wa waislamu wa bongo?magazeti yetu yanapenda sana kujenerolaizi sana,Lipumba,Hamadi Rashid,Maalim seif,wanaandaa maandamano kupitia Cuf kuipinga DOWANS kulipwa,kwa mtazamo wa chanzo chako hao niliokutajia sio waislamu?:msela:
 
Mkuu punguza hasira. Lakini you are right, watu wamekalia udini na sasa wanajaribu kuiunganisha Dowans na waislamu, huu ni upuuzi. Fisadi ni fisadi tu, hana dini. Ukianza kuangalia unaweza kuona kuna mafisadi wakristo, waislamu na mapagani, dini inayowaunganisha ni ufisadi tu.

Wakristu wengi wangependa DOWANS walipwe, pia Waislamu na dini nyingine, lakini hili gazeti!!!!!! mhhh!!!! silielewi kabisa hivi ni si linamilikiwa na Business Times au??? inakuwaje jamani?
 
:first:Hao sio waislam, ni wahuni tu wametumiwa na wanasiasa! Hakuna muislam anayeweza kushabikia uchafu huu! Kwanini mhariri hakwenda kwa Mufti au BAKWATA angalau kujua msimamo wa waislamu? Hao waliotumiwa ni wahuni, ni waislamu jina na usikute hata KITIMOTO wanakula tena sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:first:
 
Ulipaji fidia wa DOWANS

*Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao
*Kafulila apingana nao

Stella Aron na Anneth Kagenda, jijini
Wednesday, 02 February 2011

SAKATA la ulipaji wa fidia ya Sh.bilioni 94 kwa kampuni ya DOWANS kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na kukiuka mkataba,Taasisi ya Kutetea Haki za Waislam,imeibuka na kuishauri Serikali kuharakisha malipo hayo harakaiwezekanavyo kwani ni haki yao kisheria.

Wakati taasisi hiyo ya Imam Bukhary ikiishauri hivyo Serikali, Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila ameiomba Serikali itoe maelezo ya kina kuhusiana na ulipaji wa fidia hiyo.

Mwenyekiti wa taasisi ya kiislam, Sheikh Khalifa Khamis akizungumza na Dar Leo amesema kuwa, DOWANS inatakiwa ilipwe kwakuwa ina mikataba ya kisheria hivyo kitendo cha kutokulipwa ni sawa na unyanyasaji na si uungwana.

" Mikataba ipo na inaonyesha Serikali inaitambua, hivyo kwanini wasilipwe fedha zao, kwani kuvunja mkataba kwa sheria yetu ya dini ya Kiislam ni haramu kama waliandikiana mkataba walipwe hata kama ni matapeli sisi ndiyo wenye makosa,"amesema Sheikh Khamis.

Amesema kuwa, Serikali ndiyo yenye makosa kwa kuingia mkataba na kampuni hiyo bila ya kujiridhisha hivyo inapaswa kuilipa ili ijifunze siku nyingine kuingia mikataba bila kuifanyia uchunguzi wa kina.

Ameongeza kuwa, kuna baadhi ya wabunge ndiyo walioshinikiza kuvunjwa kwa mkataba huo kutokana na chuki zao binafsi hivyo kitendo hicho ndicho kinachoigharimu Serikali hivi sasa.

SOURCE: DAR LEO 2/2/'11

Na watatumwa sana mwaka huu.
 
Back
Top Bottom