(Baadhi ya) Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao

Waislam wameitaka serikali iilipe Dowans bil 94 haraka kwa sababu ni haki yao (dowans) kisheria. Nimeyasikia hayo radio free africa ktk uchambuzi wa gazeti la Dar leo saa 05:00pm.


Hivi RA ana mkono hadi kwa waislam?. Mbona wanamtetea?
Nawasilisha..

Ninaamini hao sio waislamu ninao wafahamu bali ni mtu au kikundi kinacho tumiwa na mafisadi tu
Ila ninacho jiuliza kwa nini wautumie uislamu kama Bangusilo la ufisadi
KUNANI?
 
Rostam ni m2 wa kuogopwa kuliko ukoma.
Ameniambia atahakikisha tanzania haikaliki kama hatalipwa na best yake yuko pamoja nae.
 
Tatizo la waislamu wa nchi hii ya Tanzania ni kutokuwa na umoja wa chombo kimoja chenye KUSIKILIZWA NA KUTIIWA, Kila kiongozi wa dhehebu fulani anaweza kupaza sauti kama jinsi tuonavyo na itokeavyo. Jambo la msingi ni kwa waislamu kusikilizana na kuwa na chombo maalum chenye kuridhiwa na wote ili kiwe imara na ndio iwe kipaza sauti chao, badala ya iwavyo sasa.

Kwa sababu hiyo basi...mwandishi/waandishi hawakosei watumiapo neno 'waislamu' kwa mjumuisho katika kufikisha ujumbe kwani hali iliyopo ni ya mparanganyiko tu na kudharauliana, na wala tusiwalaumu waandishi kwa kutumia hilo neno 'waislamu'.

Ni mtazamo wangu binafsi tu.
 
Itafika wakati itabidi tuwekee hati miliki majina ya dini zetu. Haiwezekani wehu waje tu na kutoa maoni yao halafu zigo loote la lawama lionekane kama ni msimamo wa wafuasi wa dini fulani. Huu ni upotoshaji na udharauji mkubwa wa dini zetu. Lazima kitu kifanyike kukomesha tabia kama za hawa walafi wa hela za mafisadi aka RA!
 
Itafika wakati itabidi tuwekee hati miliki majina ya dini zetu. Haiwezekani wehu waje tu na kutoa maoni yao halafu zigo loote la lawama lionekane kama ni msimamo wa wafuasi wa dini fulani. Huu ni upotoshaji na udharauji mkubwa wa dini zetu. Lazima kitu kifanyike kukomesha tabia kama za hawa walafi wa hela za mafisadi aka RA!
 
Mimi nafikiri hilo ni tatizo la mtu huyo. Sio jumuiya ya hao waislamu. Waislamu ninaowajua mimi hawawezi kuunga mkono jambo la wizi na kipumbavu kama hilo. Basi kama ni waislamu wote wanaunga mkono. Nchi itameguka tu. hatuwezi kukubaliana na upuuzi huo.
 
Hapo waislamu wanaonewa sana. Ni tamko la mtu tu. Waislamu ninaowafahamu mimi hawawezi kuunga mkono hilo. Dini ya kiislamu hairuhusu wizi.
 
Unless Serikali ya CCM ina mpango wa kupitisha mgao misikitini, najua hawa mashehe waliojivika majukumu ya kuwasemea waislamu watapa kichapo kama alichopokea mzee ruksa kipindi kile. Patachimbika!
 
Acha kuongea upumbavu... waislam ndio nani..? Mbona mimi muislamu sijui sijasema hivyo and I know about 1.2 billion others who are not of that opinion. JF is full of imbecilic morons like you... Cite the appropriate authority sio unageneralize watu.. Fisi we! lol

Mkuu punguza hasira. Lakini you are right, watu wamekalia udini na sasa wanajaribu kuiunganisha Dowans na waislamu, huu ni upuuzi. Fisadi ni fisadi tu, hana dini. Ukianza kuangalia unaweza kuona kuna mafisadi wakristo, waislamu na mapagani, dini inayowaunganisha ni ufisadi tu.
 
Nadhani gazeti halikuwa fair; kwa nini lisiseme Sheik Halifa na badala yake wageneralize kuwa ni Waislamu? Magazeti mengine yanataka kukuza mambo na kuuza tu kwa kutumia mgongo wa Waislamu.

True
 
ndio wanaJF hata mm nimepata wasiwasi kama kweli ni tamko la ndugu zetu waislamu ninaowaaamini kwa kuwa na msimamo wa kutokubali kunyimwa haki zao.Inafurahisha na ni nia njema kuona suala la Dowans ni la Watanzania wote kulipingaa bilakujali itikadi zetu za kidini au kisiasa. Aluta Continue lazima kielewe hao wezi ni wapi na kwanini walipwe wkt Tanesco ipoi ICU.
 
Kwani wewe hujui kuwa rostam ni dini gani???? Subiri wakristo tuone kama watongea pumba kama hizi...
 
huyu khalifa hamisi mnafiki sana,mtu wa njaa sana!aliwahi kununuliwa na idd simba matokeo yake akavunjwa mguu msikiti wa mtoro kkoo!hawakilishi muislam yeyote!
 
Ulipaji fidia wa DOWANS Wednesday, 02 February 2011 09:30 *Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao
*Kafulila apingana nao

Stella Aron na Anneth Kagenda, jijini
SAKATA la ulipaji wa fidia ya Sh.bilioni 94 kwa kampuni ya DOWANS kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na kukiuka mkataba,Taasisi ya Kutetea Haki za Waislam,imeibuka na kuishauri Serikali kuharakisha malipo hayo harakaiwezekanavyo kwani ni haki yao kisheria.

Wakati taasisi hiyo ya Imam Bukhary ikiishauri hivyo Serikali, Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila ameiomba Serikali itoe maelezo ya kina kuhusiana na ulipaji wa fidia hiyo.

Mwenyekiti wa taasisi ya kiislam, Sheikh Khalifa Khamis akizungumza na Dar Leo amesema kuwa, DOWANS inatakiwa ilipwe kwakuwa ina mikataba ya kisheria hivyo kitendo cha kutokulipwa ni sawa na unyanyasaji na si uungwana.

" Mikataba ipo na inaonyesha Serikali inaitambua, hivyo kwanini wasilipwe fedha zao, kwani kuvunja mkataba kwa sheria yetu ya dini ya Kiislam ni haramu kama waliandikiana mkataba walipwe hata kama ni matapeli sisi ndiyo wenye makosa,"amesema Sheikh Khamis.

Amesema kuwa, Serikali ndiyo yenye makosa kwa kuingia mkataba na kampuni hiyo bila ya kujiridhisha hivyo inapaswa kuilipa ili ijifunze siku nyingine kuingia mikataba bila kuifanyia uchunguzi wa kina.

Ameongeza kuwa, kuna baadhi ya wabunge ndiyo walioshinikiza kuvunjwa kwa mkataba huo kutokana na chuki zao binafsi hivyo kitendo hicho ndicho kinachoigharimu Serikali hivi sasa.

SOURCE: DAR LEO 2/2/'11

Hivi Rais hataki kutoa tamko kuhusu Dowans kwa nn?
 
Yaani 'Abdalah' akitoa maoni yake juu ya swala lolote basi linakuwa tamko la Waislamu!!
 
Back
Top Bottom