Mkurugenzi TPA: Bunge lina haki kuukubali au kuukataa mkataba wa DP World

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema Bunge la Tanzania lina haki ya kuridhia au kutoridhia mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari(IGA).

Mkataba huo ulisainiwa Oktoba 25, mwaka jana kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Hata hivyo hofu imeibuka kuhusu masilahi ya Taifa kwenye mkataba huo ambapo wanasiasa, wanaharakati na wasomi wanahoji vifungu 31 vya mkataba huo pamoja na nafasi ya Bunge katika kufikia uamuzi wa mwisho.

Kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (e) ya Katiba ya 1977 kama ilivyorekebishwa, Bunge limepewa mamlaka ya kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

“Kushauri ni moja kati ya kazi za Bunge na zipo nyingine nyingi kwa mujibu wa Katiba, katika hili hapa (mkataba wa IGA) Katiba inasema Bunge ndilo linaridhia kwa hiyo Bunge linaangalia ambacho Serikali imesaini na upande mwingine, basi linaridhia au haliridhii,” amesema Mbossa.

Mbossa ametoa kauli hiyo leo Juni 8, 2023 wakati wa mahojiano yaliyofanyika katika Kituo cha televisheni cha Clouds 360, asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa hoja na elimu kuhusu makubaliano ya mkataba huo kwa Taifa.

“Kama Bunge halitaridhia mkataba huu hautakuwepo kwa sababu una sharti lazima uridhiwe. Bila kuridhia utatekeleza kwa nguvu ipi?”amehoji Mbossa na kufafanua kuwa maelekezo yoyote ya kurekebisha vifungu vya mkataba huo kutoka bungeni, yatatafsiriwa ni kutoridhiwa kwa mkataba huo.

Chanzo: Clouds 360, Mwananchi
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Attachments

  • 279672BF-5802-407C-ABA6-92E15BDA5880.jpeg
    279672BF-5802-407C-ABA6-92E15BDA5880.jpeg
    35.9 KB · Views: 9
Ulishasainiwa unajadiliwa nini sasa?

Kwa jinsi inavyoelezwa ni kwamba mkataba unasainiwa kwanza, baada ya hapo kuna maridhiano ya kwamba kilichosainiwa kipitishwe au kikwamishwe...

Sasa kwa muundo wa serikali ya Tanzania, chombo kinachosaini mikataba ni serikali na kinachojadili na kuamua kuridhia au lah, ni bunge...

Shida ipo mahali pamoja tu hapa, je sisi kama wananchi tuna ubakika gani kama wabunge ambao ni wawakilishi wetu hawapo compromised!!!
 
Wananchi ambao ndiyo wenye nchi huo mkataba wamekua wana wasiwasi nao na hawaukubali ni busara kuuondoa, bandari shida hapo ni ubadhirifu tu na kufanya kazi kwa mazoea pakifanyiwa mabadiliko na uwekezaji mkubwa na serikali bado kama nchi tunaweza kuendesha bandari yetu.

Hao waarabu watafanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwa kasi kubwa sana tuache upuuzi watanzania tuilinde nchi yetu kama tumeshindwa kuiendesha tuvunje hata hiyo TPA.
 
Kwa jinsi inavyoelezwa ni kwamba mkataba unasainiwa kwanza, baada ya hapo kuna maridhiano ya kwamba kilichosainiwa kipitishwe au kikwamishwe...

Sasa kwa muundo wa serikali ya Tanzania, chombo kinachosaini mikataba ni serikali na kinachojadili na kuamua kuridhia au lah, ni bunge...

Shida ipo mahali pamoja tu hapa, je sisi kama wananchi tuna ubakika gani kama wabunge ambao ni wawakilishi wetu hawapo compromised!!!
Bunge ni rubber stamp, kwaiyo mhimili yote kuanzia bunge, mahakama na executive siyo sehemu salama
 
Hapo mwarabu anacholenga ni kusafirisha magendo ya rasilimali wakiwemo wanyamapori, kuna scandal ya namna dhahabu ya zimbabwe ilivyokuwa inatoroshwa na wajanja, malango ya nchi siyo sehemu za kumilikisha wageni hata siku moja.
 
Kwa jinsi inavyoelezwa ni kwamba mkataba unasainiwa kwanza, baada ya hapo kuna maridhiano ya kwamba kilichosainiwa kipitishwe au kikwamishwe...

Sasa kwa muundo wa serikali ya Tanzania, chombo kinachosaini mikataba ni serikali na kinachojadili na kuamua kuridhia au lah, ni bunge...

Shida ipo mahali pamoja tu hapa, je sisi kama wananchi tuna ubakika gani kama wabunge ambao ni wawakilishi wetu hawapo compromised!!!
Kwahili hawawezi kuwa compromised, ila watatafuta namna njema ya ku quit huku waki control political damage, which will be just okay politically...Kuliko kuuza nchi bora iwe hivyo
 
Mimi niwapongeze mashujaa wa nchi hii kwakupigana kiume mpaka kufikisha hili jambo hapo...God bless you guys, kazi yenu ni njema sana

Hongera hizi ni kwa watanzania wote, safari tuliungana kama taifa bila kujali vyama vyetu...Let us stand still kwa maslahi ya taifa letu...I can now eat my food!
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema Bunge la Tanzania lina haki ya kuridhia au kutoridhia mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari(IGA).

Mkataba huo ulisainiwa Oktoba 25, mwaka jana kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Hata hivyo hofu imeibuka kuhusu masilahi ya Taifa kwenye mkataba huo ambapo wanasiasa, wanaharakati na wasomi wanahoji vifungu 31 vya mkataba huo pamoja na nafasi ya Bunge katika kufikia uamuzi wa mwisho.

Kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (e) ya Katiba ya 1977 kama ilivyorekebishwa, Bunge limepewa mamlaka ya kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

“Kushauri ni moja kati ya kazi za Bunge na zipo nyingine nyingi kwa mujibu wa Katiba, katika hili hapa (mkataba wa IGA) Katiba inasema Bunge ndilo linaridhia kwa hiyo Bunge linaangalia ambacho Serikali imesaini na upande mwingine, basi linaridhia au haliridhii,” amesema Mbossa.

Mbossa ametoa kauli hiyo leo Juni 8, 2023 wakati wa mahojiano yaliyofanyika katika Kituo cha televisheni cha Clouds 360, asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa hoja na elimu kuhusu makubaliano ya mkataba huo kwa Taifa.

“Kama Bunge halitaridhia mkataba huu hautakuwepo kwa sababu una sharti lazima uridhiwe. Bila kuridhia utatekeleza kwa nguvu ipi?”amehoji Mbossa na kufafanua kuwa maelekezo yoyote ya kurekebisha vifungu vya mkataba huo kutoka bungeni, yatatafsiriwa ni kutoridhiwa kwa mkataba huo.

Chanzo: Clouds 360, Mwananchi
kama bunge lote asilimia kubwa ni CCM imeisha hiyo.
 
Hii kampuni kama ina mlolongo wa kesi zote hizi inayo maadui wengi wa kibiashara zabandari. Je itapata wapi muda wa kufanya kwa tija na ufanisi kazi za bandari za Tanzania???. Nchi inaingia ubia na kampuni yenye migogoro na magovi na wabia wengine kiasi hicho na bado wako watu wenye akili timamu wanaoimbia mapambio ya sifa za hii kampuni!!!!!!! Kwa mtazamo mwengine kuingia ubia na hawa ndio tumejiungamanisha na hayo makesi yote indirectily. "Rafiki wa adui yako ni adui yako"
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema Bunge la Tanzania lina haki ya kuridhia au kutoridhia mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari(IGA).

Mkataba huo ulisainiwa Oktoba 25, mwaka jana kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Hata hivyo hofu imeibuka kuhusu masilahi ya Taifa kwenye mkataba huo ambapo wanasiasa, wanaharakati na wasomi wanahoji vifungu 31 vya mkataba huo pamoja na nafasi ya Bunge katika kufikia uamuzi wa mwisho.

Kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (e) ya Katiba ya 1977 kama ilivyorekebishwa, Bunge limepewa mamlaka ya kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

“Kushauri ni moja kati ya kazi za Bunge na zipo nyingine nyingi kwa mujibu wa Katiba, katika hili hapa (mkataba wa IGA) Katiba inasema Bunge ndilo linaridhia kwa hiyo Bunge linaangalia ambacho Serikali imesaini na upande mwingine, basi linaridhia au haliridhii,” amesema Mbossa.

Mbossa ametoa kauli hiyo leo Juni 8, 2023 wakati wa mahojiano yaliyofanyika katika Kituo cha televisheni cha Clouds 360, asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa hoja na elimu kuhusu makubaliano ya mkataba huo kwa Taifa.

“Kama Bunge halitaridhia mkataba huu hautakuwepo kwa sababu una sharti lazima uridhiwe. Bila kuridhia utatekeleza kwa nguvu ipi?”amehoji Mbossa na kufafanua kuwa maelekezo yoyote ya kurekebisha vifungu vya mkataba huo kutoka bungeni, yatatafsiriwa ni kutoridhiwa kwa mkataba huo.

Chanzo: Clouds 360, Mwananchi
Sa100 must go!!!!
 
Kwa jinsi inavyoelezwa ni kwamba mkataba unasainiwa kwanza, baada ya hapo kuna maridhiano ya kwamba kilichosainiwa kipitishwe au kikwamishwe...

Sasa kwa muundo wa serikali ya Tanzania, chombo kinachosaini mikataba ni serikali na kinachojadili na kuamua kuridhia au lah, ni bunge...

Shida ipo mahali pamoja tu hapa, je sisi kama wananchi tuna ubakika gani kama wabunge ambao ni wawakilishi wetu hawapo compromised!!!
Hamnaga kitu kama hicho mkataba ukisha sainiwa ndio final.majadiljano Bungeni yanatakiwa kufanyika kabla ya mkataba kusainiwa.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema Bunge la Tanzania lina haki ya kuridhia au kutoridhia mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari(IGA).

Mkataba huo ulisainiwa Oktoba 25, mwaka jana kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Hata hivyo hofu imeibuka kuhusu masilahi ya Taifa kwenye mkataba huo ambapo wanasiasa, wanaharakati na wasomi wanahoji vifungu 31 vya mkataba huo pamoja na nafasi ya Bunge katika kufikia uamuzi wa mwisho.

Kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (e) ya Katiba ya 1977 kama ilivyorekebishwa, Bunge limepewa mamlaka ya kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

“Kushauri ni moja kati ya kazi za Bunge na zipo nyingine nyingi kwa mujibu wa Katiba, katika hili hapa (mkataba wa IGA) Katiba inasema Bunge ndilo linaridhia kwa hiyo Bunge linaangalia ambacho Serikali imesaini na upande mwingine, basi linaridhia au haliridhii,” amesema Mbossa.

Mbossa ametoa kauli hiyo leo Juni 8, 2023 wakati wa mahojiano yaliyofanyika katika Kituo cha televisheni cha Clouds 360, asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa hoja na elimu kuhusu makubaliano ya mkataba huo kwa Taifa.

“Kama Bunge halitaridhia mkataba huu hautakuwepo kwa sababu una sharti lazima uridhiwe. Bila kuridhia utatekeleza kwa nguvu ipi?”amehoji Mbossa na kufafanua kuwa maelekezo yoyote ya kurekebisha vifungu vya mkataba huo kutoka bungeni, yatatafsiriwa ni kutoridhiwa kwa mkataba huo.

Chanzo: Clouds 360, Mwananchi
waukatae tu. hatuhitaji jibu lingine. au la wakiukubali, basi kisiwepo kipengele cha kwamba tusiendeleze bandari zingine. wanaogopa nini? wachukue bandari ila tuwe na uhuru kujenga bandari ingine kama ya bagamoyo, tanga na mtwara, ili wachina wakija bagamoyo wawape ushindani wa kueleweka. shida waarabu wanaogopa bandari ya bagamoyo ikijengwa basi dubai inapugnuza mzigo sana.
 
Back
Top Bottom