Waislam tunapaswa kuondokana na upofu wa dini la sivyo tutaonekana wote hatuna akili

Feld Marshal Tantawi

JF-Expert Member
Dec 24, 2014
609
1,007
Kama kuna kitu Waislamu tunapaswa kukifanya katika kuandika HISTORIA yetu na ikasomwa kila baada ya sala ni hii ya Ikulu ya Magogoni hapa Dar es salaam maana ni historia yetu na ni halali kwetu kufanya hivyo ila sio kwenye suala la Mkataba wa Bandari; huko tunahitaji kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu mikataba ya kimataifa.

Viongozi wetu hasa Ma-Imamu wetu na wengine wanaokaribishwa kutoa neno, wakumbuke kwamba suala la Bandari linahitaji udadavuzi wa SHERIA na SIO SHARIA. Hili la Bandari halihitaji MUAZINI kulisimamia, linahitaji wataalamu wa sheria kulichambua nando maana hatua yakwanza kabisa kupinga ilipelekwa mahakamani kupata ufafanuzi wa kisheria, hukumu ikatoka kwamba mkataba unazo dosari unatakiwa kurekebishwa. Kitaalamu hii ilishindikana mahakama kutengua maamuzi ya Bunge bali ilishauri Bunge lipitie sheria hizo litekebishe huo mkataba. Kwa kifupi ni kwamba MKATABA hauna faida kwa taifa.

Katika eneo ambalo Waislam tunapaswa kuliellewa ni kwamba tunapaswa kulizingatia ni hili viongozi wetu kuweka maneno ya chuki dhidi ya imani zingine, tukishindwa kuwahoji misikitini basi tutoke tuwaache waendelee na SOGA zao baada ya IBADA.

Kuna ujinga unasambazwa kwamba UJIO wa DP World utalifanya KANISA lisiingize makontena yao kwa msamaha wa kodi. Innalillah Wainalillah rajiun; kwanza tutambue masuala yote ya kikodi yanapangwa na serikali yetu, ni suala la DP World kukabidhiwa list ya misamaha ya KODI kwa taasisi husika. Na hapo hakuna atakaepinga. DP World hawaji kupanga masuala ya kodi ama tozo za bandarini; bei elekezi za bandari zitaendelea kusimamiwa na TPA na TRA. Hili Waislam tulielewe; tusipuyange.

Yaani kwa kifupi ile misamaha ambayotuliipeleka ya kuomba kuondolewa kodi ya TENDE, msamaha wa kodi ya MAJI ya ZAMZAM na mengineyo DP WORLD watayakuta mezani. Halafu pia wataikuta list ya misamaha ya kodi ya VIFAA TIBA, VIFAA VYA KUJIFUNZIA WANAFUNZI SUNDAY SCHOOLS, SECONDARY, COLLEGES nk wataikuta pale. Kwa hiyo hakuna kitu KANISA watapoteza bali wenzetu wameenda mbali zaidi kwa kuangalia uhalali wa mkataba na sio kuhusu misamaha ya kikodi au kwa sababu mwekezaji ni kampuni kutoka taifa la kiarabu. Mataifa mangapi ya kiarabu yamewekeza hapa? Ukienda pale Ngorongoro kuna kampuni ngapi za kiarabu? Ukienda Loliondo pale kuna maeneo ukifika unakaribishwa UAE 🇦🇪, umewahi kuona kanisa linaongelea hayo?

Hawa akina Arab contractors wanaojenga Bwawa la Mwalimu Nyerere si wanatoka Misri? Au wale mnawachukulia kuwa ni wajukuu wa FARAO? Na hawa wanaojenga SGR si ni waarabu wa Uturuki 🇹🇷 ? Au wale mnawachukulia ni ndugu zake Ottoman? Jikiteni katika kuzijadili hojaza TEC na sio kuwajadili waliokaa kuzichambua hizo hoja.

Anyway; ngoja niwarudisheni kwenye historia kidogo kuhusu Ikulu ya Magogoni na hili mkalikalie vikao mlijadili pengine mnaweza kulidai iwe mali yetu Waislam maana kihistoria ni mali ya Waislam na hata Magufuli aliamua kuhamisha makao makuu Dodoma ili ikulu hii iwe sehemu ya historia mkapate kuijua hii Ikulu vema.

Pale mlango wa kuingia Ofisi ya Rais (Ikulu) kuna maandishi yanasomeka hivi (ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ), maandishi haya yanatoka katika Aya ya Quran Surat Al HIJR Aya Ya 46 inayosema
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ
Wataambiwa "Wacha Mungu" Ingieni kwa salama na amani. Ikisomeka (Udkulu_Ha_Bi_Salamin_Aminina)

Jina Hili la (Dare Salaam) lilibadilishwa na Wajerumani Kutoka katika jina la Asili la (DARU SALAAM) baada ya Wajerumani kuwatoa Waislamu kimabavu katika eneo hilo na kuiweka Ikulu mwaka 1870.

Ikumbukwe kwamba Ikulu hii ilikuwa msikiti uliojengwa na Sultan Majid kutokea Zanzibar Mwaka 1865 kwa ajili ya watu kujifunzia Quran na kusoma elimu ya Dini ya kiislam (leo tungesema ulikuwa msikiti wenye chuo cha Madrasa ) ambako watu mbalimbali kutoka Congo, Malawi, walifika kusoma hapa. Jengo hili likaitwa #DAR_U_SALAAM (Dar es salaam) kama walivyo zoea wengi. Neno hilo ni neno la Kiarabu lenye maana ya NYUMBA YA AMANI. Neno hili sio geni Duniani, ukienda LEBANON utakuta Dar Salaam..

Kwa hiyo katika mambo tunayoweza kuyafundisha kama historia ni haya lakini sio huku tunakotaka kwenda.

Tujisahihishe
 
Unajua kuchambua hoja kwa mantiki, tofauti na wakina Ritz The Boss na THE BIG SHOW wenye mihemko ya kidini miaka yote, wanaoona sifa kulinda ushetani wa ndugu yao katika imani, hata kama amefanya kosa la wazi linaloonekana kwa kila mmoja.

Hilo la ikulu ya Magogoni kama kweli ni jengo lenu, kalichukueni tu, inaonekana serikali waliichukua wakati huo wakiwa na upungufu wa majengo, tofauti na sasa tayari ipo ikulu ya Dodoma, kumbe Magufuli aliona mbali sana, inawezekana alijua baada ya muda sio mrefu mtaanza kulalamika, apumzike kwa amani huko alipo.
 
Uko sahihi. Masheikh wapo kwenye majibizano ya kushindana, wakati maaskofu wanaweka mbele mustakbali wa Taiifa zima ndiyo maana huoni maaskofu wakiandika neno "sheikh", "uislamu", "waislamu" katika waraka wao.

Hao DP World wametimuliwa Djibouti nchi ya asilimia 98 waislamu tupu sembuse hapa kwetu!

Ishu hapa ni mkataba mbovu, siyo habari za uislamu wala Ukiristo

Mbona waislamu wa Uturuki wanajenga SGR maaskofu hawajatoa waraka?
Mbona Waislamu wa Misri wanajenga bwawa la Stieglers maaskofu hawajatoa waraka?

Qur'an inasema simamia haki na sema ukweli hata kama ukweli unakutandika wewe mwenyewe!

Usiposimamia haki na ukweli utaonekana kituko tu, bali yule asimamiaye ukweli atapata heshima!

Na ukweli haujalishi kausema paroko, askofu au imamu na sheikh!

Kwenye hili la bandari, maaskofu wapo katika ukweli na haki!
 
Serekali imeshajua ni rahisi kuwateka waisilamu kupitia dini yao. Wanajua waisilamu hawana muda wa kuangalia ukweli ikishachomekwa hisia ya dini yao. Kibaya zaidi viongozi wao ndio wamekuwa wepesi kupotezwa kwenye hoja, na kuachwa wakipayuka kushambuliwa kwa dini yao kwa jambo lisilo na uhusiano na dini, ili mradi msimamizi wa jambo ni muislamu, basi wao hilo jambo hulifanya ndio uislamu!
 
Hawajifunzi tu, Waislamu walimpigania Kikwete, Muislamu mwenzao kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, akaishia kuwalipa kwa kuwasweka ndani mamia ya masheikh wao kwa makosa ya ugaidi. Kuna masheikh wamekaa jela huko Arusha na nchi nzima tangu wakati wa Kikwete, wengine wametolewa na Samia majuzi tu, wengine bado wako ndani!.

Badala waangalie faida za nchi na watu wake, wao wanaangalia kutetea wanasiasa eti kwa sababu ana jina linalojishabihiana na dini yake.

Kwani kuwa Muislamu ni halali kuuza nchi ilmradi unayemuuzia ni Muislamu mwenzio, ni nini maana sasa ya kulinda dhamana uliyopewa?
 
Wale wazungu wa kahama barick wanachota dhahabu kila siku lakin sijasikia tamko lolote la TEC
 
"SHURA YA MAIMAMU TANZANIA"

WALISHATOA TAMKO LAO NA LINALINGANA KABISA KIMAUDHUI NA TAMKO LA UMOJA WA KANISA KATORIKI.

NA HAPAKUWA NA HISIA ZOZOTE ZA UDINI.

ILA AKIONGEA MKATORIKI NI UDINI

HISIA ZA UDINI ZINATOTAKANA NA KUSHINDWA HOJA HIVYO KUTAFUTA KUUNGWA MKONO NA WATU WASIOJIELEWA.

Kama mtakuwa na busara japo kidogo basi mjue kuwa mtakuwa sahihi mnapo ongealea jambo lenye mustakabari wa Taifa Letu

Yohana 8:32
tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
 
JE ANAYESEMA ATAWAZAA HAPA DUNIANI NA KUWAPOTEZA WOTE NI NANI??????

Quran 15:39.
Akasema :mola wangu mlezi! Ilivyokuwa imenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa Duniani na nitawapoteza wote.

HUYU ANAYESEMA ATATUZAENI WAISLAMU NA KUTUPOTEZA WOTE NI NANI????

Shetani hakuwafīcha kuwa anawapeleka motoni

وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا

[ MARYAM - 71 ]
Na hakuna yeyote katika nyinyi ila mwenye kuifikia jehannam Hiyo ndiyo hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe.

allah mwenyewe makazi yake ni motoni!

Sahih al-Bukhari 4848
Narrated Anas:
The Prophet (ﷺ) said, "The people will be thrown into the (Hell) Fire and it will say: "Are there any more (to come)?' (50.30) till Allah puts His Foot over it and it will say, 'Qati! Qati! (Enough Enough!)'"
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي الأَسْوَدِ، حَدَّثَنَا حَرَمِيٌّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضى الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ يُلْقَى فِي النَّارِ وَتَقُولُ هَلْ مِنْ مَزِيدٍ‏.‏ حَتَّى يَضَعَ قَدَمَهُ فَتَقُولُ قَطِ قَطِ ‏"‏‏.‏
Reference : Sahih al-Bukhari 4848
In-book reference : Book 65, Hadith 369

Kama anaebishia allah sio maskani yake motoni atuwekee ushahidi aliutoa mguu wake motoni lini.
 
Mkuu upo Mje ya Mada. Hii mada sio ya Mambo ya Dini.
Karibu Jukwaa la Dini.
 
Unajua kuchambua hoja kwa mantiki, tofauti na wakina Ritz The Boss na THE BIG SHOW wenye mihemko ya kidini miaka yote, wanaoona sifa kulinda ushetani wa ndugu yao katika imani, hata kama amefanya kosa la wazi linaloonekana kwa kila mmoja.

Hilo la ikulu ya Magogoni kama kweli ni jengo lenu, lichukueni tu, inaonekana serikali waliichukua wakati huo wakiwa na upungufu wa majengo, tofauti na sasa tayari ipo ikulu ya Dodoma, kumbe Magufuli aliona mbali sana, inawezekana alijua baada ya muda sio mrefu mtaanza kulalamika, apumzike kwa amani huko alipo.
Umemsahau Ustaadh FaizaFoxy 😂😂🔥🔥
 
Back
Top Bottom