Shehe Ponda: Ikiwa Serikali inashindwa kutimiza Baadhi ya majukumu yake kwa Ufasaha ndivyo Itaweza Kufundisha Watoto Wetu Dini ya Kiislamu?

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,308
24,200
10 August 2023
WAISLAM WAIKAANGA SERIKALI MTAALA ELIMU YA DINI "KUHUSU BANDARI WAMETUITA KWANINI SIO HILI".



Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania viongozi wake Sheikh Ponda, Sheikh Kundecha, Sheila Suleiman Daudi, Sheikh Abdallah Mrisho na Sheikh Hassan Abbas wametoa taarifa kwa umma juu ya mstuko wao mpango wa serikali kujichukulia jukumu la kuisimamia dini na kuifundisha dini baada ya kutoa mtaala wake kuanzia angazi ya kindergarten hadi vyuo vya ualimu.

Habari kwa kina:

Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar

Taasisi na jumuiya za kiislamu Tanzania, haikubaliani na hatua ya Serikali kusimamia dini ya kiislamu na kuifundisha

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 10, 2023, Amiri Jumuiya na Taasisi za Kislamu Tanzania Alhajj Sheikh Musa Kundecha, amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa kwamba,Serikali sasa imekwishaandaa silabasi za masomo ya dini na kuondoa mambo yote ya imani ya dini inayohusiana na dini hizo.

Amesema kwamba katika kikao chao cha Julai 23/7/2023 kilichofanyika Masjid EFA viongozi wa jumuiya na taasisi za kislaam walipokea kwa mstuko mkubwa taarifa kwamba Serikali sasa inasimamia dini na kufundisha.


“Mstuko huu unakuja katika ukweli kwamba kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu, serikali haina dini na kuwa mambo ya dini yapo nje ya utendaji wa Serikali na kila dini itasimamia mafunzo ya dini yake na kwa kuzingatia kwamba dini na masomo yake yalipangwa kwa pamoja baina ya taasisi za dini na Serikali kupitia vitengo vyake vya elimu na kuandaa silabasi na vitabu vya kufundishia” amesema Sheikh Kundecha.

Sheikh Kundecha amesema kwa mujibu wa historia ya masomo ya dini na kufundishwa kwake,ilikwishatokea Serikali kuingilia masomo ya dini na wasilamu kupinga kuingiliwa huko hatimaye kukubalika masomo ya dini yataandaliwa kwa pamoja baina ya wananchi na Serikali na kupatikana silabasi na vitabu kuanzia ngaizi ya wali hadi vyuo vya ualimu.

”Sasa jambo hili linatulazimisha kuamini kuwa serikali inakuja na mfumo wa dini mpya, ikizingatiwa kwamba dini yetu ya kiislamu na serikali ipo tofauti kubwa za misingi”amesema Shekhe Kundecha.

Ametoa mfano kwenye Serikali kuna pombe zote ni halali, wakati katika uislamu pombe zote ni haramu.

Shekhe Kundecha amesema kutokana na uzito wa jambo hilo,walilazimika kumuandikia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, kumuomba kukutana ili kulingalia jambo hilo kwa mustakabali wa taifa letu barua ambayo ilifika ofisini kwake Julai 25,2023 lakini mpaka sasa hawajaitwa wala kujibu barua hiyo.

“Serikali yenyewe haina dini na sasa imeandaa, mafundisho ya dini ya kiislamu na kuondoa mambo yote ya kiimani dini ya uislamu bila imani hakuna dini sasa sisi tunaomba waziri akutane nasi ili kujenga mustakabali mwema wa nchi yetu,” amesema
 
Serikali ilibugi kurasimisha tahasusi za dini bila kujua walimu watatoka wapi?
Kwa vigezo vya ajira serikalini, hakuna sheikh atakidhi hivyo vigezo bali mapadri waliosemea uislam ndo wataajiriwa kufundisha uislam mashuleni.
 
Serikali ilibugi kurasimisha tahasusi za dini bila kujua walimu watatoka wapi?
Kwa vigezo vya ajira serikalini, hakuna sheikh atakidhi hivyo vigezo bali mapadri waliosemea uislam ndo wataajiriwa kufundisha uislam mashuleni.
Uisilamu ubafundishwa shuleni hili iweje?uzushi mtupu
 
Serikali inaposema haina dini, huwa inamaanisha nini, ni tahasusi za dini ya kiislamu tu ndio zitakazofundishwa au dini zote, kwani madhehebu yameshindwa kufundisha Imani zao?
 
😂😂🔥🔥 Prof Mkenda kachemka!
Ni mfumo wetu. Mfumo wetu unaruhusu watawala kulala na vimada wao, na vimada wakawapa ushauri wabadilishe nini kwenye mifumo na sheria zetu. Kwa hili suala waislam wana hoja ya msingi kabisa. Kufundisha dini siyo kazi ya serikali hata kidogo.
 

KIKWETE AMPA KONGOLE RAIS SAMIA MABADILIKO SERA MITAALA YA ELIMU​

Published on Tuesday 27 June, 2023 15:09:18

Image
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Ushirika wa Wafadhili wa Elimu Duniani (GPE) amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mitaala ili kukidhi mahitaji ya soko Kitaifa na Kimataifa.

Mhe. Kikwete ametoa pongezi hizo Juni 27, 2023 jijini Dodoma katika kikao na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kumpitisha kwenye kwenye Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mabadiliko ya mitaala.

Akizungumza katika kikao hicho pia ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kutekeleza agizo hilo na kuwataka kuhakikisha mabadiliko ya mitaala yanaakisi Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia kwa kutoa elimu bora kwa wote pamoja na kuhakikisha ubora wa wahitimu katika ngazi zote.

"Mageuzi haya ni ya msingi, ninaomba tuzingatie sana suala la ubora. Na katika utekelezaji hakikisheni umma wa watanzania unaelimishwa, mueleze kuhusu manufaa yake sasa na hata baadae" alisema Mhe. Kikwete.

Mhe. Kikwete ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali za kutekeleza mageuzi hayo kwa kushirikisha wadau mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amemshukuru Mhe. Kikwete kwa kukubaki kushiriki katika kikao hicho na kutoa maoni kuhusu muelekeo huo mpya wa Sera ya elimu na Mitaala.

" tinakushukuru sana kwa maoni na nia yetu ni kuhakikisha tunapoanza utekelezaji hasa upande wa Amali tunaanza kwa ubora wa hali ya juu, ndio maana tunahitaji sana ushiriki wa wadau" , amesema Prof.Mkenda.

Aidha Prof. Mkenda amemhakikishia kuwa Wizara imejipanga kikamilifu katika kutekeleza kwa awamu malengo yote ya Sera baada ya kupitishwa Rasimu hiyo kulingana na ratiba inavyopendekeza.

Source : tovuti ya wizara ya elimu
 
Shehe Ponda amesema kamwe Waislamu hawatakubali Watoto Wao wafundishwe Somo la Dini ya Kiislamu kwa mtaala wa Serikali na walimu wa Serikali

Shehe Ponda ameitaka Serikali kuwaheshimu Waislamu na wakumbuke Serikali haina Dini

Ponda amesema iwapo Serikali hadi sasa imeshindwa kutimiza Baadhi ya majukumu yake kwa ufanisi ndivyo Itaweza Kufundisha Watoto Wao Dini ya Kiislamu?

Mlale Unono 😃
 
Shehe Ponda amesema kamwe Waislamu hawatakubali Watoto Wao wafundishwe Somo la Dini ya Kiislamu kwa mtaala wa Serikali na walimu wa Serikal...
Mambo ya kufundisha dini serikali iachie dini zenyewe kufanya hiyo kazi, madrasa and sundaya school zinaweza hiyo kazi.
 
Yuko sawa,masomo ya dini yatolewe kwenye mitaala ya elimu watu wa dini wafundishane huko kwenye majumba ya imani zao.
 
Mitaala

Mapendekezo ya mitaala kwa darasa la kwanza na la pili, masomo ni Kusoma, Kuandika, Kuonesha umahiri msingi katika Lugha ya Kiingereza, Hisabati, Kuthamini Utamaduni, Sanaa na Michezo na Kutunza Afya na Mazingira.

Masomo kwa darasa la tatu hadi la sita ni Kiswahili, English, Kifaransa, Kichina, Kiarabu, Hisabati, Historia ya Tanzania na Maadili, Elimu ya Dini, Sanaa na Michezo, Sayansi na Jiografia na Mazingira.

Kwa elimu ya sekondari hatua ya chini, masomo ni Historia ya Tanzania na Maadili, Historia, Jiografia, English, Literature in English, Kiswahili, Kiarabu, Kichina, Kifaransa, Michezo, Biolojia, Kemia, Fizikia, Kilimo, Hisabati, Sayansi ya Kompyuta na Utunzaji wa Taarifa za Fedha.

Source : tovuti ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TEI)
 
Serikali ilibugi kurasimisha tahasusi za dini bila kujua walimu watatoka wapi?
Kwa vigezo vya ajira serikalini, hakuna sheikh atakidhi hivyo vigezo bali mapadri waliosemea uislam ndo wataajiriwa kufundisha uislam mashuleni.
Kwanini unapenda uchochezi? Kuwa Mwinyi, Kikwete na sasa Samia wote hawalion hilo au wao si waislam swaf?
 
Serikali ilibugi kurasimisha tahasusi za dini bila kujua walimu watatoka wapi?
Kwa vigezo vya ajira serikalini, hakuna sheikh atakidhi hivyo vigezo bali mapadri waliosemea uislam ndo wataajiriwa kufundisha uislam mashuleni.
Hahahaaa! Eti hakuna sheikh atakidhi vigezo
 
Back
Top Bottom