Wakili Mkuu wa Serikali: Uvunjaji Holela wa Mikataba chanzo cha Migogoro ya Madai

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1694613085285.png
W
Baadhi ya Taasisi za Umma ambazo zimekuwa zikivunja Mikataba au Kuingia Makubaliano na kampuni binafsi bila kuihusisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, zimetajwa kusababisha Migogoro ya Kibiashara.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende, ametaja changamoto za ofisi hiyo wakati akimpokea Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Pindi Chana na kueleza kuwa kutofuatwa kwa Sheria za Mikataba hufikia hatua ya kuisababishia Serikali hasara kwa kutozwa fidia.

Ikumbukwe, baadhi ya Migogoro imewahi kuigharimu Serikali ikiwemo kusababisha kukamatwa kwa Ndege za ATCL na Mashauri mengine ambayo Serikali ilitakiwa kulipa Fidia kutokana na Uvunjaji Holela wa Mikataba

============

Baadhi ya taasisi za umma kuvunja mikataba au makubaliano ziliyoingia na kampuni binafsi bila kuihusisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imetajwa kuwa mzizi wa migogoro mingi ya madai.

Hayo yamesemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Boniphace Luhende, jijini Dar es Salaam leo, Septemba 13, 2023 wakatika akitaja changamoto za ofisi hiyo katika hafla ya kumpokea Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Pindi Chana alipowatembelea.

Dr Luhende amesema kuwa changamoto hiyo haiishii kuwa mgogoro, aghalabu hufukia hatua ya kuisababishia serikali hasara kwa kutozwa fidia.

Kauli ya Dk Luhende inakuja kipindi ambacho Serikali imewahi kuingia hasara ya kulipa fidia kwa kuvunja mkataba na kampuni binafsi kwa kile kilichoelezwa kutofuata taratibu za kisheria katika kuvunja mikataba hiyo.

Mwaka 2016, Serikali ilivunja mkataba na kampuni ya Symbion Power Co Ltd wa uzalishaji umeme na baada ya shauri hilo kupelekwa katika Mahakama ya Kimataifa (ICC), Serikali ilitakiwa kulipa zaidi ya Sh10 bilioni.

Katika maelezo yake hayo, Dk Luhende amesema baadhi ya taasisi za umma hufanya uamuzi wa kuvunja mikataba hiyo bila kuishirikisha ofisi yake.

"Baadhi ya taasisi za umma zinavuvunja mikataba au makubaliano ziliyoingia na kampuni au taasisi mbalimbali binafsi bila kuihusisha ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na hivyo kusababisha wingi wa migogoro," amesema.

Mbali na hiyo, changamoto nyingine amesema ni baadhi ya taasisi za umma kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi pasi kuzingatia sheria.

Ameeleza hatua hiyo inasababisha kuzaliwa kwa utitiri wa migogoro ya ajira.

Usimamizi hafifu wa miradi hasa ya ujenzi, ni changamoto nyingine iliyotajwa na Dk Luhende inayosababisba migogoro mingi hasa ya usuluhishi.

Lakini, amesema zipo baadhi ya taasisi za Serikali zinachelewesha malipo ya huduma kwa wakandarasi na kusababisha mashauri mengi ya madai ya fidia.

Kwa mujibu wa Dk Luhende, ofisi hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi wabobevu wa kuendesha mashauri ya migogoro hasa ya Kimataifa na mashauriano katika eneo la mafuta na gesi.

Pamoja na uwepo wa changamoto hizo, amesema mafanikio lukuki yamepatikana ikiwemo kumaliza baadhi ya mashauri nje ya mahakama.

Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Chana amesema ni kiu yake kuona utendaji wa ofisi hiyo unakomesha hasara kwa taasisi za Serikali.

"Tunataka halmashauri zisipate hasara tena, ninyi ndiyo mnapaswa kwenda kutoa elimu ya kama wanataka kuvunja mkataba wanapaswa kufanyaje," amesema.

MWANANCHI
 
Kwani yeye anakuwa wapi wakati hayo mamikataba mabovu yanapo sainiwa?.

Mnasaini mikataba mibovu makusudi ili muibe kodizetu kupitia ushirika wa makubaliano mnaoingia na hao makampuni binafsi.

Mnatega kotekote mnajua mkataba mbovu Usipo vunjwa mnakula taratibu, ukivunjwa mnawaelekeza kwenda mahakamani ilimgawane fidia tunazolipa kwa kodizetu.

Kunasiku laana ya Mungu itawashukia.
 
Kabla hajazungumzia kuvunjwa Kwa mikataba angeanza na kuzungumzia mikataba mibovu inayoingiwa
 
View attachment 2748079W
Baadhi ya Taasisi za Umma ambazo zimekuwa zikivunja Mikataba au Kuingia Makubaliano na kampuni binafsi bila kuihusisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, zimetajwa kusababisha Migogoro ya Kibiashara.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende, ametaja changamoto za ofisi hiyo wakati akimpokea Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Pindi Chana na kueleza kuwa kutofuatwa kwa Sheria za Mikataba hufikia hatua ya kuisababishia Serikali hasara kwa kutozwa fidia.

Ikumbukwe, baadhi ya Migogoro imewahi kuigharimu Serikali ikiwemo kusababisha kukamatwa kwa Ndege za ATCL na Mashauri mengine ambayo Serikali ilitakiwa kulipa Fidia kutokana na Uvunjaji Holela wa Mikataba

============

Baadhi ya taasisi za umma kuvunja mikataba au makubaliano ziliyoingia na kampuni binafsi bila kuihusisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imetajwa kuwa mzizi wa migogoro mingi ya madai.

Hayo yamesemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Boniphace Luhende, jijini Dar es Salaam leo, Septemba 13, 2023 wakatika akitaja changamoto za ofisi hiyo katika hafla ya kumpokea Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Pindi Chana alipowatembelea.

Dr Luhende amesema kuwa changamoto hiyo haiishii kuwa mgogoro, aghalabu hufukia hatua ya kuisababishia serikali hasara kwa kutozwa fidia.

Kauli ya Dk Luhende inakuja kipindi ambacho Serikali imewahi kuingia hasara ya kulipa fidia kwa kuvunja mkataba na kampuni binafsi kwa kile kilichoelezwa kutofuata taratibu za kisheria katika kuvunja mikataba hiyo.

Mwaka 2016, Serikali ilivunja mkataba na kampuni ya Symbion Power Co Ltd wa uzalishaji umeme na baada ya shauri hilo kupelekwa katika Mahakama ya Kimataifa (ICC), Serikali ilitakiwa kulipa zaidi ya Sh10 bilioni.

Katika maelezo yake hayo, Dk Luhende amesema baadhi ya taasisi za umma hufanya uamuzi wa kuvunja mikataba hiyo bila kuishirikisha ofisi yake.

"Baadhi ya taasisi za umma zinavuvunja mikataba au makubaliano ziliyoingia na kampuni au taasisi mbalimbali binafsi bila kuihusisha ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na hivyo kusababisha wingi wa migogoro," amesema.

Mbali na hiyo, changamoto nyingine amesema ni baadhi ya taasisi za umma kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi pasi kuzingatia sheria.

Ameeleza hatua hiyo inasababisha kuzaliwa kwa utitiri wa migogoro ya ajira.

Usimamizi hafifu wa miradi hasa ya ujenzi, ni changamoto nyingine iliyotajwa na Dk Luhende inayosababisba migogoro mingi hasa ya usuluhishi.

Lakini, amesema zipo baadhi ya taasisi za Serikali zinachelewesha malipo ya huduma kwa wakandarasi na kusababisha mashauri mengi ya madai ya fidia.

Kwa mujibu wa Dk Luhende, ofisi hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi wabobevu wa kuendesha mashauri ya migogoro hasa ya Kimataifa na mashauriano katika eneo la mafuta na gesi.

Pamoja na uwepo wa changamoto hizo, amesema mafanikio lukuki yamepatikana ikiwemo kumaliza baadhi ya mashauri nje ya mahakama.

Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Chana amesema ni kiu yake kuona utendaji wa ofisi hiyo unakomesha hasara kwa taasisi za Serikali.

"Tunataka halmashauri zisipate hasara tena, ninyi ndiyo mnapaswa kwenda kutoa elimu ya kama wanataka kuvunja mkataba wanapaswa kufanyaje," amesema.

MWANANCHI
Migogoro mingi inazalishwa na wakuu wa taasisi wanaojichulia sheria kama zao binafsi!
 
Back
Top Bottom