Nachelewa sana kujua baadhi ya maneno yanayotamkwa na wasanii

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,736
Kuna nyimbo kadhaa nikisikiliza naweza nisijue ametamka nini huyo msanii mpaka inaweza chukua hata miezi au zaidi ndo nakuja kuelewa kilichotamkwa,

Kwa mfano kuna nyimbo nilikuwa nasikiliza nilichokisikia ni hichi,

Afrooo afrooo mtoto wa Msagenda, ilinichukua miaka kujakujua kumbe ni mtoto wa Msagana,

Na mstari mwingine ni omiyetu, imenichukua miaka sijui 7 ndo nimekuja kujua kuwa ni me ad you

Na mstari mwingine ni, rafiki gani huyu mdananda, imenichukua miaka 10 kulisikia hilo neno kwenye wimbo,

Na ule wimbo wa mshipi wa rc ndo sijui huwa wanaimbaje maana nyimbo za rc napenda kusikiliza lakini kuielewa mistari ndo inakuwa kazi,

Na mstari mwingine ni, chunga tamaa mayona chunga tamaa mayona, kumbe ilikuwa ni chunga tamaa mbayaa chunga tamaa mbayaaa

Kuna siku nikiwa nafanya kazi sehemu bosi wangu alinipigia simu na kuniambia nioshe gari yupo karibu anakuja, mimi nikawasha na alipofika akalikuta lipo selensa, alinishangaa sana,

Kuna matukio mengi sana ya kufanya vitu tofauti na nilivoambiwa lakini inakuwa ndivyo nilivyosikia

Hii hali sikumbuki ilianza lini ila kuna vitu nahisi viliongezea shida,

Kitu cha kwanza ni uvuvi wa kuzamia, yaani unaenda kina bila kitu chochote na baadae unahisi kama masikio yanataka kupasuka kwa mgandamizo wa maji, yanalia tfuuuu

Kitu cha pili niliwahi fanya kazi kwenye mashine ambayo ikiwa inafanya kazi hata mkiwa karibu hamsikilizani, na mkiizima hiyo mashine masikio hupiga kelele kama ya miluzi ya kuchoma masikio,

Swali langu hasa kuhusu nyimbo je ni mm tu ndo husikia tofauti na kilichoimbwa?
 
hata mm nipo kama ww sema nshakubakiana na hali tunaishi tu hvhvo tena mm na kuona pia ni chanagamoto
 
Nyimbo nyingi za Bongo Fleva huwa sizielewi wanaimba nini.

Nikisikiliza nyimbo za kingereza naelewa kinachoimbwa ila bongo huwa sielewi kabisa, sijui kwanini iko hivyo.
 
Kuna nyimbo kadhaa nikisikiliza naweza nisijue ametamka nini huyo msanii mpaka inaweza chukua hata miezi au zaidi ndo nakuja kuelewa kilichotamkwa,

Kwa mfano kuna nyimbo nilikuwa nasikiliza nilichokisikia ni hichi,

Afrooo afrooo mtoto wa Msagenda, ilinichukua miaka kujakujua kumbe ni mtoto wa Msagana,

Na mstari mwingine ni omiyetu, imenichukua miaka sijui 7 ndo nimekuja kujua kuwa ni me ad you

Na mstari mwingine ni, rafiki gani huyu mdananda, imenichukua miaka 10 kulisikia hilo neno kwenye wimbo,

Na ule wimbo wa mshipi wa rc ndo sijui huwa wanaimbaje maana nyimbo za rc napenda kusikiliza lakini kuielewa mistari ndo inakuwa kazi,

Na mstari mwingine ni, chunga tamaa mayona chunga tamaa mayona, kumbe ilikuwa ni chunga tamaa mbayaa chunga tamaa mbayaaa

Kuna siku nikiwa nafanya kazi sehemu bosi wangu alinipigia simu na kuniambia nioshe gari yupo karibu anakuja, mimi nikawasha na alipofika akalikuta lipo selensa, alinishangaa sana,

Kuna matukio mengi sana ya kufanya vitu tofauti na nilivoambiwa lakini inakuwa ndivyo nilivyosikia

Hii hali sikumbuki ilianza lini ila kuna vitu nahisi viliongezea shida,

Kitu cha kwanza ni uvuvi wa kuzamia, yaani unaenda kina bila kitu chochote na baadae unahisi kama masikio yanataka kupasuka kwa mgandamizo wa maji, yanalia tfuuuu

Kitu cha pili niliwahi fanya kazi kwenye mashine ambayo ikiwa inafanya kazi hata mkiwa karibu hamsikilizani, na mkiizima hiyo mashine masikio hupiga kelele kama ya miluzi ya kuchoma masikio,

Swali langu hasa kuhusu nyimbo je ni mm tu ndo husikia tofauti na kilichoimbwa?
Umenivunja mbavu
 
Afu hiyo mbona ipo kwa watu wengi sioni kama ni tatizo nadhani ni concentration tu

Ule wimbo wa Make it rain wa Fat Joe kuna mwanangu alikuwa ni mnyakyusa alikua anapenda ile chorus ya Lil Wayne

Alikuwa anaimba hivi "hamisi gakukina mosebo" hapo katikati nimesahau sijui alikuwa anamtaka maneno gani ila alikuwa anamalizia "hamisi goo"

Nilipowahi kumuuliza kwanini unaimba hivyo akajibu "mimi ndio navyo sikia"

View: https://youtu.be/4dPjONDN3ZI?si=2Q3kfMej2Bxdl-YN
 
Sasa kama si masihala,huoni wewe una tatizo? Unasubili nini kufika hospitali na kupatiwa matibabu? Kwa kazi ulizozifanya,ni wazi zimekuachia ugonjwa. Ila sasa unachanganya unaposema ingilishiii unaelewa vizuri
 
Cha kushangaza hii coment yako umeandika kwa kiswahili
Nyimbo nyingi za Bongo Fleva huwa sizielewi wanaimba nini.

Nikisikiliza nyimbo za kingereza naelewa kinachoimbwa ila bongo huwa sielewi kabisa, sijui kwanini iko hivy
 
Back
Top Bottom