Baadhi ya hospitali na zahanati huwa zinawanyima majibu ya vipimo wagonjwa wanaoshindwa kununua dawa kwao

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Serikali kupitia Wizara ya Afya na TAMISEMI komesheni hii tabia kwenye baadhi ya hospitali na zahanati
zinazowanyima majibu wale wagonjwa wanaofika kupima katika hospitali zao!

Wagonjwa hulipia gharama za vipimo kama kawaida, lakini inapofika hatua ya kupatiwa majibu nakala huwa hawapewi!

Kinachofanyika wao kwa wao hutumiana majibu kwa kompyuta hadi kwenye pharmacy yao (wakati mwingine dakitali hushauri kulingana na dawa zilizopo dukani kwao ili ziuzike)

Ukiachilia bei kuwa juu, Wagonjwa huwa wanakosa haki ya kupatiwa majibu wanapokosa pesa ya kulipia dawa.

Naomba Waziri wa Afya na kamati za afya toeni tamko kutokomeza tabia hii inayowatesa sana hasa watu mijini na vijijini.
 
Imewahi kunikuta hii kwenye hospitali ya watoto Sinza Kijiweni. Nimempeleka dogo halafu sikuwa na Bima ya Afya. Mchakato umeenda kama mdau alivyosema ila kila nikiulizia mtoto anasumbuliwa na nini siambiwi. Tulivyofika kwenye dawa gharama zake si haba. Nilikuja sanuka baada ya kukosa dawa moja nikaambiwa nikanunue pharmacy ya nje, nadhani wale wanaijua vizuri hiyo hospitali wakaanza kunihoji dawa nimeuziwa bei gani. Baada ya kuwaambia wakashangaa sana, yaani dawa ambazo ningenunua elfu 30 nimeuziwa elfu 90.

Naelewa wanafanya biashara lakini basi hizo hospitali zijitahidi kuwa fair kwenye uuzaji wa dawa ili zisiumize wasiotumia bima za afya.
 
Hili ni ttzo inawezekana sisi watafta uduma atujui labda wamiliki na wajuzi wa mambo watusaidie nn huwa ttzo je wako sawa wanaofanya ivyo au wanakosea wajuzi na wamiliki mtupe elmu kdg
 
Mimi hospitali zangu ni za serikali tu, huko majibu ni sahihi sana , kotoa usumbufu wa foleni uwa nakodisha nurse , mambo yanaenda fasta

Hawa binafsi watakupa dawa , yaani ukiweka kwenye sahani ni kama ugali wa buku mbili kwa mama ntilie.. Hapo dawa ya kukutibu ni moja au hakuna kabisa
 
Imewahi kunikuta hii kwenye hospitali ya watoto Sinza Kijiweni. Nimempeleka dogo halafu sikuwa na Bima ya Afya. Mchakato umeenda kama mdau alivyosema ila kila nikiulizia mtoto anasumbuliwa na nini siambiwi. Tulivyofika kwenye dawa gharama zake si haba. Nilikuja sanuka baada ya kukosa dawa moja nikaambiwa nikanunue pharmacy ya nje, nadhani wale wanaijua vizuri hiyo hospitali wakaanza kunihoji dawa nimeuziwa bei gani. Baada ya kuwaambia wakashangaa sana, yaani dawa ambazo ningenunua elfu 30 nimeuziwa elfu 90.

Naelewa wanafanya biashara lakini basi hizo hospitali zijitahidi kuwa fair kwenye uuzaji wa dawa ili zisiumize wasiotumia bima za afya.
Kwangu ilikuwa kinyume yako mkuu,dawa ambazo kituo cha afya X ningenunua kwa 14500/- niliuziwa kwa 25000/- maduka ya nje.Toka hapo. Ninaheshimu sana duka la Kituo hicho
 
Utoaji wa majibu ya vipimo unafanya watu watumie dawa ovyo ovyo!! Mfano UTI mgonjwa anaandikiwa dawa kulingana na kiwango cha bacteria lakini hawa bush doctors wanakushauri ukanunue dawa yoyote as long as ni antibiotics!!
 
Imewahi kunikuta hii kwenye hospitali ya watoto Sinza Kijiweni. Nimempeleka dogo halafu sikuwa na Bima ya Afya. Mchakato umeenda kama mdau alivyosema ila kila nikiulizia mtoto anasumbuliwa na nini siambiwi. Tulivyofika kwenye dawa gharama zake si haba. Nilikuja sanuka baada ya kukosa dawa moja nikaambiwa nikanunue pharmacy ya nje, nadhani wale wanaijua vizuri hiyo hospitali wakaanza kunihoji dawa nimeuziwa bei gani. Baada ya kuwaambia wakashangaa sana, yaani dawa ambazo ningenunua elfu 30 nimeuziwa elfu 90.

Naelewa wanafanya biashara lakini basi hizo hospitali zijitahidi kuwa fair kwenye uuzaji wa dawa ili zisiumize wasiotumia bima za afya.
si salama ki afya maana wagonjwa wanadulumiwa haki yao, vipimo wanalipia lakini wasipo nunua dawa wananyimwa
 
Utoaji wa majibu ya vipimo unafanya watu watumie dawa ovyo ovyo!! Mfano UTI mgonjwa anaandikiwa dawa kulingana na kiwango cha bacteria lakini hawa bush doctors wanakushauri ukanunue dawa yoyote as long as ni antibiotics!!
majibu kwa nini wasipewe ili wawe huru kutafta dawa au kwenda kukopa wanapopajua, maana hata kanuni za pharmacy inatakiwa mgonjwa aje na cheti kutoka kwa dakitali kuonesha dawa na ugonjwa...sasa unapowanyima then what
 
Back
Top Bottom