Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Dkt. Medard Beyanga
Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Dkt. Medard Beyanga ameshauri jamii kuwa na kawaida ya kufanya vipimo kuanzia katika hatua za awali za ugonjwa na kuacha kujichukulia maamuzi ya kwenda kununua dawa bila kuwa na utaalam wa daktari.
Amesema jambo la kwanza la kufanikiwa kumaliza changamoto ya ugonjwa au Magonjwa ya Mlipuko ni kufanya vipimo vya maabara mapema kwa kuutambua ugonjwa husika ili kujua njia rasmi na sahihi za kuutibu.
Kutumia dawa bila vipimo, hufanya Vimelea vya Ugonjwa kuwa sugu na unaweza usipone tatizo.
Ameeleza kuwa anatoa wito kwa jamii kufanya vipimo katika sehemu sahihi kwa kuwa kufanya hivyo kunarahisisha njia za kukabiliana na changamoto husika, kwa kuwa kuendelea kutumia dawa bila kupima kunasababisha usugu ndani ya mwili na baadaye hali hiyo inaweza kuathiri mwili wakati wa matibabu rasmi.
“Mtu anapopata changamoto za awali kabisa anatakiwa kwenda kuanzia ngazi ya Zahanati kama ataona ni jambo dogo, lengo la kufanya hivyo ni kuwa hata anapotokea ugonjwa husika ni mkubwa kuliko sehemu aliyoenda kupata matibabu basi watampa mwongozo wa nini akifanye au kumpeleka katika ngazi za juu zaidi.
“Kufanya hivyo kunaweza kupungua hata magonjwa ya maambukizi, kuna wakati kumekuwa kukitokea changamoto za maambukizi kusambaa kwa kasi kwa kuwa tu hatua muhimu hazikuchukuliwa mwanzoni.”
Ametoa mfano maambukizi ya Ugonjwa wa Marburg yaliyotokea Mkoani Kagera miezi ya hivi karibuni, akieleza kuwa yaliripotiwa mapema na ndio maana hata matibabu yake yalidhibitiwa mapema pia.
Pia soma - Wizara ya Afya: Mtumishi mmoja wa Afya alifariki kwa Ugonjwa wa Marburg Virus