DOKEZO Wagonjwa wanapewa magonjwa ambayo hawana ili Zahanati ziuze dawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Ujumbe huu ufike Serikalini hasa kwa Wizara ya Afya, sasa hivi baadhi ya vituo vya maabara vinafanya kitu kimoja, ukienda kupima hata kama huna Typhod majibu yao ni una-typhod, unajikuta unatumia dawa huponi.

Ukienda kupima tena bado majibu ni unatyphod, sasa hii ni hatari sana, watu wanakunywa dawa za typhod kumbe hawana changamoto hiyo.

Mimi ilinikuta mpaka nikaenda Mount Meru kupima ndio wakanambia sina typhode nina ‘uric acid’ nyingi sana kwenye mwili.

Nilipofuatilia kwa ndugu na watu wangu wa karibu nimegundua kuwa changamoto za aina hiyo zipo nyingi, zahanati zinafanya vipimo kama biashara ili wahusika waweze kuuza dawa, tena wagonjwa wengi wanauziwa anti biotic ili mradi tu biashara ifanyike, Serikali iangalie hicho kinachoendelea.


Majibu ya Mamlaka: Ofisi ya Msajili Bodi ya Maabara Binafsi za Afya yasema inafanyia kazi Madai ya Maabara kutoa majibu ya Uongo
 
Ujumbe huu ufike Serikalini hasa kwa Wizara ya Afya, sasa hivi baadhi ya vituo vya maabara vinafanya kitu kimoja, ukienda kupima hata kama huna Typhod majibu yao ni una-typhod, unajikuta unatumia dawa huponi.
...
Sidhani hii kitu kama Inahusu Hospitali.

Nadhani unazungumzia Maabara Binafsi.

Ambazo hata ukienda na homa ukalengesha Dalili za malaria lazma utaambiwa una wadudu Wa malaria 5..

Tujaribu kuweka Utaratibu wa kwenda kwenye Vituo vya afyaa na Hospitali na sio Kwenda kujipima bila kupewa rufaa kutoka vituo vya afya.

Kumbuka wao wanafanya biashara
 
Magonjwa ni biashara za watu. Usipokua makini utatoa sana pesa kutafuta afya njema. Kama wataalamu wa afya waliweza kutengeneza magojwa ili wafanye biashara ya dawa, sishangai hili.

Kuna kampeni wazungu wanataka waipige miaka ijayo. Ni kwamba, watoto wadogo wawe wanapewa ARV haijalishi hali ya afya yake, kampeni wataipiga kwa kuwaambia satu kuwa ARV zinaimarisha kinga za mwili asipate maambukizi na blaa blaa zingine. Ila uhalisia sio huo, wakishaanza kutumia inaweza iwe life time.

Magonjwa ni biashara. Amkeniii
 
Sidhani hii kitu kama Inahusu Hospitali..
Nadhani unazungumzia Maabara Binafsi...
Siyo kila mahala kuna vituo vya afya au hospitali, kingine ni urasimu mkubwa, juzi nilienda hospital kubwa tuu ya rufaa nikatumia siku nzima Mpaka kumuona daktari.

Pamoja na kuwa na Bima ya afya bado nikaambiwa hivi vipimo 2 itabidi ulipe cash!! Kila nikijaribu kujua ni vipimo gani hivyo sikupata jibu. Kwenda kulipia hivyo vipimo nikaambiwa 180,000, ambayo muda huo sikuwa nayo.

Kwenye bima nikaambiwa nipime full blood picture tuu, ambayo niliwaeleza kwamba nimeifanya few days ago Kwenye hospital nyingine. Yaani siku ikaisha hivi hivi...
 
Wanakupangia Ugonjwa sio 🤣🤣
Ila kuna tofauti kati ya zahanati na Duka la Dawa na pia maabara Binafsi
Our 3rd born ni daktari.
Kuna mahali alienda kufanyiwa usaili, usaili wenyewe aliambiwa akae chumba cha daktari afanye consultation. Basi bwana, mwenye zahanati naye ni daktari mzee, akawa anakagua prescriptions na vipimo dogo anavyoandika.

Mzee akaanza kumsema vibaya, sasa kwa style hii tutapata pesa kweli? Ikabidi nesi mmoja akamsanue dogo kimya kimya, mzee haridhiki na unachofanya huku. Wakija watu andika vipimo vingi/vya pesa nyingi na dawa unamtwanga dawa nyingi au za bei mbaya.

Ndipo pale una UTI ya kawaida unagongwa pawasef kwa siku 5🤣

Bongo nyoso!!!!!
 
Our 3rd born ni daktari.
Kuna mahali alienda kufanyiwa usaili, usaili wenyewe aliambiwa akae chumba cha daktari afanye consultation. Basi bwana, mwenye zahanati naye ni daktari mzee, akawa anakagua prescriptions na vipimo dogo anavyoandika.
Mzee akaanza kumsema vibaya, sasa kwa style hii tutapata pesa kweli? Ikabidi nesi mmoja akamsanue dogo kimya kimya, mzee haridhiki na unachofanya huku. Wakija watu andika vipimo vingi/vya pesa nyingi na dawa unamtwanga dawa nyingi au za bei mbaya.
Ndipo pale una UTI ya kawaida unagongwa pawasef kwa siku 5🤣
Bongo nyoso!!!!!
Hii mkuu Hilo sikatai nilishafanya Sana kazi kwenye Hospitali za binafsi na Nilifanya hivyo pia..
Ila nilipokuwa Private tulifamya hivi ili kuongeza pesa..
Kwa mfano Mgonjwa atahitaji Amoxyciline..
Bhasi utampa antibiotic ambayo ni kubwa kuliko hiyo na inafanna kazi na hiyi kwa mfano Amoxicine Plus Clavulanic Amoclav...
NA ni kweli wanao ongoza ni Private..
Kwa hiki nakusuport sana na hata kwenye Bima tulikuwa tunachezesha sana
 
Kwa ushahidi ambao nimeshuhudia mwenyewe kwa matukio mawili.

1. Miezi ya katikati mwaka jana Kaka yangu aliumwa sana akawa anataka kununua mseto ameze. Mimi nikamshauri kuwa akapime kwasababu kunywa dawa bila kupima unaweza kujikuta kwenye hatari ya kunywa dawa ambazo hazihusiani na ugonjwa.

Kweli nikamchukua mpaka kwenye maabara iliyopo jirani na mtaa wetu. Kufika pale akapimwa damu na majibu yakaja kuwa ana Typhoid.

Palepale nikawa namkumbusha ndugu yangu kuwa jinsi ambavyo alitaka kunywa dawa za mseto kwenye ugonjwa ambao haumsumbui.

Wakati tunatoka maabara yule doctor akamshika mkono bro akamuambia dawa tunazo hapa hapa tena unapona baada ya siku mbili tu.

Bro akamjibu kuwa mimi kuna sehemu ambayo huwa dawa nachukua bure.

Tulipotoka tukaenda pharmacy tukamuambia mhudumu atupe dawa ambayo inaponesha haraka akatupatia.

Bro kameza zile dawa mpaka kamaliza dozi lakini hakuna mabadiliko, zaidi tukaona anazidi kudhoofika na kuwa katika hali ya hatari.

Hapo ndio ikabidi nimpigie rafiki yangu ambaye ni Doctor kumuomba ushauri akaniambia nenda kituo fulani ukapime hiyo itakuwa ni Maleria.

Tumepima majibu yamekuja ni Maleria madaktari wakawa wanamlazimisha kumchoma sindano na kumpa kitanda eti hali yake sio nzuri.

Dozi ya sindano ni 6 halafu kila sindano gharama ni 6,000, tukakataa.

Tukaenda kununua mseto akanywa na siku inayofuata tu akawa amepata nafuu. Dozi ilivyoisha tayari alikuwa yupo fresh kila kitu.
 
Siyo kila mahala kuna vituo vya afya au hospitali, kingine ni urasimu mkubwa, juzi nilienda hospital kubwa tuu ya rufaa nikatumia siku nzima Mpaka kumuona daktari. Pamoja na kuwa na Bima ya afya bado nikaambiwa hivi vipimo 2 itabidi ulipe cash!! Kila nikijaribu kujua ni vipimo gani hivyo sikupata jibu. Kwenda kulipia hivyo vipimo nikaambiwa 180,000, ambayo muda huo sikuwa nayo. Kwenye bima nikaambiwa nipime full blood picture tuu, ambayo niliwaeleza kwamba nimeifanya few days ago Kwenye hospital nyingine. Yaani siku ikaisha hivi hivi...
Ni vipimo Gani hivyo mkuu..
Unajua Kila level huwa ina matibabu na Vipimo vyake..
Na zilo lebeled kabisa..

Kwa mfano Dispensary na Kituo cha Afya Ni level A-B
Hospitali ya Wilaya ni Level C Wanasuport Dawa na Vipimo level A-C..
hospitali ya Rufaa ya mkoa na Kanda Kwenye specialist wana level S kwahyo Dawa huwa ni Level A-S..

Kila Daktari Ana level ya kutibu kuanzia Tabibu mpaka Daktari mshauri Super Specialist.. Na hizo level ndo A mpaka S hapo juu..
Kwahyo unaweza kukuta Daktari anakuambia kuwa Bima hailipi kumbe level yake hairuhusu kutoa Hiyo dawa kwenye Bima so lazma ulipie ili upate hiyo dawa
 
Ujumbe huu ufike Serikalini hasa kwa Wizara ya Afya, sasa hivi baadhi ya vituo vya maabara vinafanya kitu kimoja, ukienda kupima hata kama huna Typhod majibu yao ni una-typhod, unajikuta unatumia dawa huponi.

Ukienda kupima tena bado majibu ni unatyphod, sasa hii ni hatari sana, watu wanakunywa dawa za typhod kumbe hawana changamoto hiyo.

Mimi ilinikuta mpaka nikaenda Mount Meru kupima ndio wakanambia sina typhode nina ‘uric acid’ nyingi sana kwenye mwili.

Nilipofuatilia kwa ndugu na watu wangu wa karibu nimegundua kuwa changamoto za aina hiyo zipo nyingi, zahanati zinafanya vipimo kama biashara ili wahusika waweze kuuza dawa, tena wagonjwa wengi wanauziwa anti biotic ili mradi tu biashara ifanyike, Serikali iangalie hicho kinachoendelea.
Ni mtihani sana hasa vituo vya afya vile vya binafsi huwezi kupima ukaambiwa mzima either usingiziwe malaria, UTI au typhoid , hili ni tatizo sana kucheza na afya za watu
 
Kisa cha pili

Usiku mmoja niliumwa tumbo, asubuhi kulivyokucha tu nikaibukia kwenye kituo cha Afya.

Nikaandikishwa dirishani nikapewa maelekezo kuwa nikamuone daktari chumba fulani.

Daktari akaniuliza kinachonisumbua nikamjibu kuwa ni tumbo pale pale akaniambia hiyo ni Typhoid.

Nikambishia nikamuambia Typhoid haiwezi kuwa kwasababu nina miaka mingi nakunywa treated water na hata vyakula vibicho kama chumbari huwa sili.

Akaniambia hata kama unaepuka njia hizo bado njia za kuweza kupata Typhoid ni nyingi kwa mfano ukawa unakula migahawani.

Nikashangaa kusikia hoja ya aina hiyo kutoka kwa Doctor ikabidi nimuulize hao wadudu wanapenya vipi mpaka wakweza ku survive kwenye chakula ambacho kishakuwa boiled?

Maana yake hata ule ushauri wa kiafya kuwa tunywe maji yaliyo chemshwa basi hauwezi kuwa na impact yeyote kwenye kuzuia wadudu enezi wa Typhoid.

Doctor akaniambia Typhoid unaweza kuipata kwa njia nyingi hata kupitia maji ya chooni unayotumia kutawaza.

Hapo ndio nikabaki mdomo wazi. Akaniambia nenda maabara chumba kinachofuata ukapime.

Nikapima damu, majibu niliyosomewa na Doctor ni kuwa nina vidonda vya tumbo pamoja na Typhoid.

Wakanitajia gharama za dawa kuwa ni 25,000 nikawaambia sawa ila mi kwa saizi sina hiyo hela ila naombeni mnipe hiyo tipoti ya vipimo niondoke nayo ili nikipata hela niende duka la dawa niwaoneshe hiyo report wanipe dawa.

Wakakataa wakaniambia hawatoi ripoti ya vipimo na kama sina hela basi nirudi tu nyumbani nijipange, siku nikapata nitarrjea hapo wanipe hizo dawa.

Sikuridhika na majibu yao ya vipimo hususani ya kuniambia nina Typhoid. Nilipotoka hapo nikaenda kwenye kituo cha Afya Cha Arafa.

Sababu ya kwenda kwenye hicho kituo ni kutokana na kushawishiwa na rafiki yangu kuwa hicho ndio kituo kinachotoa huduma bora kwasababu mke wake alihudiwa hapo.

Kufupisha stori

Niliandikiwa vipimo viwili hapo Arafa

Kipimo cha kwanza kilisema nifanyiwe checkup ya Ultra Sound kuangalia damage ya tumboni

Kipimo cha pili kilikuwa ni damu. Vipimo vyote kwa ujumla niliambiwa nilipie 25,000.

Lakini nilipimwa kipimo kimoja tu ambacho ni cha damu. Hakukuwa na Ultra Sound na wala pesa yangu niliyolipia kwa ajili ya kipimo hicho haikurudishwa.

Nilipofika kwa daktari akaniambia vipimo vimeonesha nina vidonda vya tumbo akaniambia nenda dirisha la dawa

Nilipoenda kwenye dirisha la dawa niliambiwa nilipie 99,000.

Nikasema hiyo hela sina kwa sasa ila naombeni ripoti ya vipimo wakaninyima

Kwa bahati nzuri niliwahi kupiga picha ripoti ya maabara ila ile ya kwa Doctor sikuweza kuipata.

Almost Miezi minne now nimeweza kutibu vidonda vya tumbo kupitia maoni ya wana JF bila kutumia midawa yao ya kausha damu.
 
Back
Top Bottom