Baada ya video ya mhudumu wa afya kuosha vifaa tiba na maji baridi kusambaa, wamekurupuka na kutoa matamko mawili

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Baada ya video kusaambaa ikionesha mhudumu wa afya akiosha vifaa tiba kwa maji ya baridi na kunianika juani, serikali imekuja na majibu, ila kama kawaida inaonesha huwa hawawasiliani na hivyo kutoa matamko mawili mawili.

Waziri Ummy katoa tamko kuwa ameona video hiyo na kwamba atafatilia kujua ukweli wake, huku ofisi ya DED jana 7/7/2023 ilitoa tamko lake ikisema vifaa hivyo vilitolewa stoo kwa ajili ya uchambuzi wa kujua vifaa vipi vinafaa kwa matumizi na vipi havifai, na kwamba watu wasipotoshe.

Hapa utaona kabisa hakuna mawasiliano baina yao. Tukija kwa huyu wa pili aliyetoa tamko kuwa vifaa vilikuwa vinachambuliwa, utaona kabisa amekurupuka na anafanya tuulize zaidi.

- Vifaa vinachambuliwaje na kuoshwa moja kwa moja kwa moja hapo hapo?

- Kwanini kazi hiyo apewe dada wa usafi wanaosafisha mazingira ya hapo na vyoo na kadhalika na sio mhudumu wa afya anaeyejua taratibu husika?

- Kwanini vioshwe kwatika mazingira hayo na kuanikwa juani kama vimechambuliwa na kuonekana vinafaa kwa matumizi ya wagonjwa?

Wakuu mnaonaje hili?

Screenshot 2023-07-08 124841.png

Tamko la Waziri Ummy Mwalimu

Screenshot 2023-07-08 125135.png
Screenshot 2023-07-08 125205.png

Tamko la Mkurugenzi

Pia soma

Waziri Ummy: Nimeona Clip ya Mtumishi wa Afya Hospitali ya Kivule akiosha vifaa na kuanika juani. Tunalifanyia kazi!

Hospitali ya Amana, Kivule hutakasa vifaa tiba kwa maji ya Bomba na kuvianika juani
 
Back
Top Bottom