Wawekezaji wa dawa na vifaa tiba kutoka India wavutiwa kuwekeza Tanzania

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Wawekezaji wa bidhaa za dawa na vifaa tiba kutoka India wavutiwa kuwekeza Tanzania ambayo pia ni mlango wa sahihi wa kulifika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara lenye idadi ya watu zaidi ya Milioni 745.

Hayo yamesemwa na Waziri Ummy Mwalimu Julai 27, 2023 mara baada ya kufanya kikao na wafanyabiashara ambao wamewekeza katika sekta ya dawa na vifaa tiba nchini Tanzania kikao kilichoandaliwa na shirikisho la wenye viwanda la nchini India yaani Federation of India Chambers of Commerce and Industry. ( FICCI) Jijini New Delhi India.

“Tanzania inategemea na kuagiza zaidi ya asilimia 60 ya dawa na vifaa tiba kutoka nchini India. Hivyo kupitia kikao hiki, tumewahakikishia kuwa Serikali itatoa ushirikiano mkubwa kwa wafanyabiashara hawa pindi wanapotakiwa kuzingatia taratibu za ukaguzi, usajili na uingizaji wa dawa na vifaa tiba na kufanya uwekezaji nchini Tanzania” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amebainisha kuwa kwenye ziara yake hiyo ameambatana na Wataalam kutoka TMDA pamoja na Mfamasia Mkuu wa Serikali ambapo kwa pamoja wametoa ufafanuzi wa hoja zilizoibuliwa na wafanyabiashara hao jambo ambalo liliwafurahisha na kuwaongezea ari ya kufanya uwekezaji nchini Tanzania.

Hata hivyo Waziri Ummy ametumia fursa hiyo kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania na kuwahamasisha wafanyabishara hao kutembelea Tanzania kwa shughuli za utalii huku wafanyabiashara hao wakiomba Serikali kutangaza zaidi vivutio hivyo kupitia Ubalozi wa Tanzania mjini New Delhi tayari wameanza taratibu za kutangaza vivutio hivyo ambapo watashirikiana na Wizara ya Utalii katika kuhakikisha kuwa vivutio vyote vya utalii vinatangazwa ikiwa ni pamoja na taratibu zote za kufanya utalii.

IMG_20230728_202429_436.jpg
 
Walishawaona mazuzu

Hivi Mfalme wa Morocco alishajenga uwanja Dodoma?

Vipi huyu atakuja kuwekeza lini?
---

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Muigizaji Maarufu wa FilamuDuniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye ni Balozi wa hisani wa Umoja waMataifa wa IFAD alipokuwa Davos nchini Uswizi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Muigizaji Maarufu wa FilamuDuniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye ni Balozi wa hisani wa Umoja waMataifa wa IFAD alipokuwa Davos nchini Uswizi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Muigizaji Maarufu wa FilamuDuniani Idris Elba ambaye ni Balozi wa Hisani wa Umoja wa Mataifa wa IFAD pamojana Mke wake Sabrina Elba walipokuwa Davos nchini Uswizi.

Mfanyabiashara mkubwa na Mwenyekiti mwenza waTimu ya Manchester United ya Uingereza Avie Glazer akisikiliza kwa makiniwakati Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiitangaza Tanzania katika mkutanouliofanyika Davos, nchini Uswizi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa Kuitangaza Tanzania katikaSekta ya Uwekezaji kwenye ukumbi wa Mikutano wa Congress, Davos nchini Uswizitarehe 19 Januari, 2023. Wa kwanza kushoto aliyevaa miwani ni mfanyabiasharamkubwa na Mwenyekiti mwenza wa Timu ya Manchester United ya Uingereza AvieGlazer akisikiliza kwa makini wakati Mhe. Rais alipokuwa akiitangaza Tanzania.
 
Back
Top Bottom