Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amepongeza hatua iliyochukuliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kwa kumsimamisha kazi Mtumishi wa Afya katika Kituo cha Afya Kivule, Dar es salaam kufuatia kuonekana kwenye video akiwa akisafisha vyombo vya Hospitalini kwa njia isiyofaa.
Kuhusu clip hiyo, soma
Waziri Ummy amesema hayo leo akiwa Bariadi, Simiyu kwenye ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo amesema kuwa kitendo alichofanya Mtumishi huyo hakikubaliki hata kidogo.
“Tumeona juzi kule Dar es salaam, Mtumishi anaosha vyombo vya Hospitali kwa maji ya baridi na kuanika juani, sijawahi kuona na nimefurahi kuona kuna hatua imechukuliwa, hivi ni kweli Mtumishi unafundishwa hivyo kuosha vyombo na kuanika juani?“
Kufuatia kusambaa kwa video ya Mtumishi huyo akisafisha vifaa vya Hospitalini kwa njia isiyo rasmi, mnamo Julai 8, 2023 Waziri Ummy alitoa tamko na kusema kuwa Mtumishi huyo alikuwa amefanya kosa kwa kukiuka Miongozo ya Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi wa Magonjwa (Infection Prevention and Control).
Waziri Ummy amewasisitiza Watumishi wa Afya kuzingatia weledi katika majukunu yao ya kazi, huku akiwataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwachukulia hatua za kisheria Watumishi wanaokiuka maadili na miiko ya kazi zao.
Millard Ayo
Kuhusu clip hiyo, soma
- Waziri Ummy: Nimeona Clip ya Mtumishi wa Afya Hospitali ya Kivule akiosha vifaa na kuanika juani. Tunalifanyia kazi!
- DOKEZO - Hospitali ya Amana, Kivule hutakasa vifaa tiba kwa maji ya Bomba na kuvianika juani