Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,253
- 26,162
- Thread starter
- #141
Kisu gani? Kimegongaje?Swali Rahisi kwako:
Kama umeusoma waraka huo Kuna provision yoyote ambayo imeandikwa Kwa muktadha wa kidini au ukiitaka serikali izingatie matakwa ya kidini au kanisa Katoliki?
Kama hujausoma usicoment utadhihirisha ujinga wako.
Baraza la Maaskofu linaundwa nà Maaskofu ambao ni Watanzania, wanaaongoza waumini wa kanisa Katoliki Tanzania. Hivyo logically Maaskofu wanaongoza sehemu ya watanzania, na sio watanzania wote!
Watanzania ni wananchi wa Tanzania wanaostahili haki za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Maaskofu wametoa waraka kama viongozi wa kanisa Katoliki Tanzania ambapo Kuna watanzania wanaostahili haki za kiuchumi, na katika mkataba wa Bandari Kuna athari za kiuchumi Kwa watanzania bila kujali dini zao au kama hawana dini kabisa!
Kimsingi kisu kimegota mfupani