Baada ya sheria ya haki ya dhamana kupitishwa, Serikali iangalie suala la Polisi kuvizia kukamata mtu Ijumaa ili akae rumande hadi Jumatatu

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Tunashukuru kwamba serikali hatimae imesikiliza kilia cha wananchi cha siku nyingi juu ya kuweka watu mahabusu bila kuwapa haki yao ya dhamana.

Udhaifu wa hili ulikuwa pande zote mbili, polisi na mahakama, kwa sababu mahakimu nao pia walikuwa wakiwaendekeza polisi kwa kuachia watu warudishwe rumande wakati polisi wamesema wazi upelelezi haujakamilika.

Ilifikia Tanzania mtu anawekwa mahabusu akiwa hana kosa, kwa kile polisi wanachokiita "kuisaidia polisi katika upelelezi wake"

Sasa basi tuende hatua moja mbele. Lipo hili suala la polisi kutaka kuwakomoa watu, pale ambapo wanaweza kukufuata siku yeyote ya wiki kutokana na tuhuma fulani, lakini watakufuata Ijumaa jioni ili ukae rumande hadi Jumatatu na kwenda mahakamani ambako unaweza kupewa dhamana.

Polisi wanafanya hili makusudi, na najua kwa roho mbaya ya askari wengi, wataendelea kulifanya japo hii sheria ya haki ya dhamana imepitishwa.

NImewahi kumsikia polisi akitishia kumkamata mtu Ijumaa jioni ili tu amkomoe!

Hivyo basi, kama tumesema kwamba dhamana ni haki ya mtuhumiwa, bas dhamana iweze kupatikana ndani ya muda unaotakiwa, bila kujali mtuhumiwa amekamatwa Ijumaa au Jumatatu.

Suala la kuangalia liwe ni vipi mtuhumiwa atapata dhamana ikiwa atakamatwa siku kama Ijumaa wakati saa za kazi za mahakama zimepita kuweza kutoa dhamana?
 
  • Thanks
Reactions: Ntu
Dhamana inatolewa hata Jumapili.

The legend Kangi Alphaxad Lugola alisema.
 
Hizi sheri aza Tanzania ziko kwenye makaratasi tuu. Wanao takiwa kuzitekeleza hawazifuati kabisa.
Kuna sheria ya mtu kuwekwa mahabusu kama sijakosea ni masaa 24/48/sina hakika vizuri.
Arusha kuna kituo kinaitwa cha wilaya ya kipolisi Muriet. Hiki kituo kuna siku nimepita hapo kuna watu wamekaa pale mahabusu wiki tatu. Hawapewi dhamana wala hawapelekwi mahakamani. Jamaa zetu polisi wanachotaka ni ndugu watoe rushwa ili waachiliwe. Mahabusu wengine hata hawajui wako pale kwa kosa gani?
Kuna takiwa reform kubwa sana ndani ya jeshi la polisi.
Mh. Rais ameunda task force nayo naona wamekaa kimya. Nadhani wanataka wawe wa kudumu kama ile ya Mukandala.
 
Back
Top Bottom