Baada ya mshahara kutoka watu wenye harusi wameanza simu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,816
106,546
Daaah,

Inakata stimu kwa kweli. Yaani hata mama sijamrushia muamala. Yaani hata kuhemea bado napotezea ili mshahara upoe kwanza.

Yaani hata hela haijampumzika kwenye akaunti. Yaani hata mwenyewe sijajipa pole na tulizo la nafsi.

Wenye maharusi tupumzisheni jamani, wekeni bajeti kulingana na uwezo wenu sio kutegemea mishahara yetu
 
Kama walijuchangia basi huna budi kufanya hivyo. Ule mchango ni deni.

Kama hawakuchanga na wala huna mpango huo hapo baadae ukioa, basi waambie tu ukweli.

Kuja kulalamika jukwaani wakati ungeweza tu kuandika 'Ndugu Mwanaharusi, acha hela yangu ipoe. Bado ni ya moto'.
Watanzania wengi ni wanafki, kumwambia mtu ukweli mbele ya sura yake hatuwezi tunaishia kumchekea

Nguvu tunamaliza kushusha uzi au kumsengenya pembeni
 
Watanzania wengi ni wanafki, kumwambia mtu ukweli mbele ya sura yake hatuwezi tunaishia kumchekea

Nguvu tunamaliza kushusha uzi au kumsengenya pembeni
Tujifunze kusema HAPANA. Wanaume tunalaani wanawake wasioweza kukataa anamvulia yoyote ila unakuta kwenye sekta yetu ni hivyo hivyo, huwezi kukataa ukasema "SICHANGI" unatoa miahadi inayokuumiza.
 
Back
Top Bottom