Nimeumia sana baada ya kuona mwanamke huyu akitafunwa na bodaboda

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,700
9,778
Na hili nalo ikiwezekana mkalitizame kwa jicho yakinifu

Nikiwa kwenye kituo fulani hivi cha bodaboda mida ya saa mbili nikiwa naelekea kazini kwangu, ghafla moyo wangu unashtuka baada ya kumuona mwanamke ambaye sijawahi kumuona maishani kwangu tokea nizaliwe

Nashindwa hata niandike nini ili mnielewe, lakini kiufupi mwanamke alikuwa na kasura fulani hivi ka kihindi mkozo, alikuwa na figure ambalo kiukweli dah, yaani ni nane mle mle! Yaani kile kigauni alichokuwa kakivaa kilimchora kiasi kwamba nashindwa kuelezea. Yote kwa yote, utamu ulikuwa kwenye sekta yetu ambayo wanaume tulikubaliana kwenye kikao chetu kilichopita itumike kama kigezo cha mpenzi mwenye tabia njema, yaani mtako, aisee. Sijawahi ona malaika kama yule

Basi bhana, akawa amemfikia boda boda mmoja na kuanza kujibizana naye, ghafla nikaona binti akitabasamu, baada ya hapo akapanda kwenye ile pikipiki kisha wakaanza safari

Akili yangu ikanituma kuwa uenda mwanamke yule anapelekwa kazini kwake, nikaona wacha nikapafahamu. Ndipo kuchukua boda boda nyingine na kumkabidhi elfu kumi, kisha nikamwambia "fuata ile bodaboda"

Basi bhana, tukaishika lami, ni mbele mbele yao hadi kieleweke, ghafla wakaingia barabara la vumbi, tukaunga nao, safari ya kama nusu saa wakawa wameibukia kwenye kigesti bubu fulani hivi. Binafsi nikamuamuru bodaboda wangu kusimama mita kadhaa kutoka eneo la tukio, baada ya hapo nilishuhudia muamala ukifanyika kwenda kwa mhudumu wa Guest, baada ya hapo wakawa wameingizana ndani

Nilibaki eneo lile juu ya siti ya pikipiki nikibubujikwa na machozi kiasi kwamba bodaboda akaamua kuniuliza, "Vipi mzee, umekuja kufanya fumanizi nini!?" Nikamwambia, "We acha tu", huku machozi laini yakinitiririka na kuambatana na kwikwi za hapa na pale

Kwa kuwa maeneo yale hayakuwa na bodaboda, sikuwa na budi kumwambia bodaboda wangu anisubiri kwa dakika kadhaa, hivyo tukaelekea kwenye kibanda kimoja cha chips na k vant tukaamua kushushia. Wakati nikiwa nimefumba macho huku kichwa kikielekea mbinguni, nilishtushwa na mkono wa bodaboda ukinishtua kuashiria kuwa kuna jambo la hatari mbele yetu. Ile kufumbua macho tu nikashtushwa na roho ya kushangaza ikiwa ndani ya mwili wenye kuvutia, "Samahani kaka, unaweza nisaidia chips mbili kavu? Changanya na makolokolo yote isipokuwa pilipili. Nipatie na K Vant moja". Baada ya kupatiwa bidhaa zote, alitutupia macho sote tuliokuwa maeneo yale, ghafla sauti ya lizee limoja kutoka kule nyuma ilisikika ikisema kwa mikwaruzo, "Mashaalah", baada ya hapo yule mzee aliinuka pale alipokuwa na kuingizana bafuni

Basi bhana, hakukuwa na namna ilibidi nisogee maeneo ya karibu sana na Guest ile kisha kulitazama geti kwa machungu yote huku nikitazama video za warumi kwenye simu yangu. Baada ya kama masaa mawili niliwashuhudia wakitoka mle Guest kisha kupanda boda boda yao tayari kuelekea kusikojulikana. Ndipo kumuita bodaboda wangu na kumpatia 10k kwa ajili ya kunirudisha kwangu, wakati narejea imenibidi nipitie dawa tatu kwa ajili ya maumivu ya kichwa

Ndipo yule bodaboda akanieleza kuwa hawa watu huwa wana mahusiano. Kila Jumapili huchukuana asubuhi asubuhi na kupelekana Guest kwa ajili ya kugegeduana

Muda huu niko ndani nimelala huku nikiwa na msongo wa mawazo na maumivu, tayari nimekwisha jichukulia sheria moja mkononi

Nimeumia sana
images%20(3).jpg
 
Back
Top Bottom