Wachovu
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 1,227
- 565
Sioni mtu wa kuongoza nchi kwenye upinzani , Mbowe ? Lissu ? Sugu ? Halima Mdee , Msigwa ? Waliomo Ukawa hata kiganja hawajai , mawaziri utachagua wapi ,Kama wewe si mshabiki wa upinzani basi ni shabiki wa CCM, na kama ni hivyo basi ingeshangaza sana kama na wewe ungeona kwamba upinzani unafaa kutoa Rais iwe 2020 ama hiyo 2025. Mbali na U-CCM wako lakini pia kwa Makonda na Magufuli umepata sababu za ziada za kuwashabikia na siku hizi huoni haya kwa hilo!
Kama mpaka mwaka 2025 unaona ni CCM tu ndiyo inafaa kutoa Rais basi kuna tatizo, na tatizo la ziada ni pale unapoona anayefaa kugombea huo urais wenyewe. Hili na upinzani kuwa bado sana kwenye nafasi ya Urais ni kwa vigezo vya sayansi ya siasa ama ni kwa mtindo wenu wa kutumia kila zana haramu kuhalalisha ushindi wenu?
Toa sababu ni kwa nini Upinzani haujawa tayari kutoa Rais?