Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,653
119,267
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" boldness and sometimes unreasonably boldness ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, ila Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu mwenye boldness kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfanyia grooming huyo headhunted?.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea Magufuli ile 2025, kiukweli kabisa Tanzania itanyooka!.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do things bila kujijua!.

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje rais Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za rais Magufuli.

Hivyo 2025 rais Magufuli asipoongeza muda, Makonda atatufaa sana. Kwa vile Makonda ni Mkolomije, kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule chapombe, pale Kolomije na atashinda kwa kishindo na kupewa moja ya important portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli.

Kitendo cha mtu wa Kanda ya Ziwa kushika urais kama alivyo rais Magufuli, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi!. Hivyo baada ya rais Magufuli aje rais Makonda, na baada ya hapo tuendelee kule kule mpaka na makabila mengine nao wawe ni walio wengi ndipo nao watastahiki! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais wa Tanzania, upinzani ni bado sana.

Paskali.
Update,
Kumbe wanaoesema baada ya Magufuli, Makonda atatufaa, siko peke yangu,
Msikilize kiongozi huyu wa dini, msikilize mpaka mwisho

Viongozi wakuu wa dini, wanaletwa na MWENYEWE YEYE, hivyo baada ya kuisikia kauli kama hiyo ya kiongozi wako wa dini, wewe kama ni muumini safi na wa kweli, ni kuikubali, hiyo ni sauti ya Mungu ikinena kupitia vinywa vya Manabii, wewe ni nani upinge?.
P
 
Ninakubaliana na wewe hasa kwenye suala la inferiority complex.

Hahitaji kuwaonyesha wananchi kama yeye ni Mkuu wa Mkoa au anapata support kutoka kwa Rais Magufuli.

Afanye kazi yake tu, kazi ya kumchambua, kupima uwezo wake na kujua nguvu zake awaachie wananchi.

Aache kukimbizana na kelele za wapiga kelele kwa sababu wananchi wenye fikra pana watashindwa kumtofautisha na wapiga kelele.

Kwenye suala la Urais wa Tanzania sikubaliani na wewe kwa sababu atakuwa hajaielewa vizuri system ya nchi inavyofanya kazi. Miaka mitano bungeni haitoshi kumfanya awe Rais wa Tanzania. Kikubwa zaidi, sioni wazee wa CCM wakimpitisha kuwa mgombea wa tiketi ya CCM.

Uwaziri utamfaa kwa kipindi hicho.
 
Back
Top Bottom